PreGE2025 Boni Yai afuturisha mamia ya Wananchi Pwani, ahimiza mshikamano na harakati za 'No reforms No Election'

PreGE2025 Boni Yai afuturisha mamia ya Wananchi Pwani, ahimiza mshikamano na harakati za 'No reforms No Election'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani Boniface Jacob maarufu Boni Yai amefuturisha mamia ya Wananchi wa Kanda ya hiyo katika Iftari maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Hall Sinza jijini Dar es Salaam tarehe 22 Machi 2025.

Akizungumza Baada ya iftar hiyo, Boni Yai amewaeleza wanachama wa Chadema kuwa, dhumuni la kuleta Iftari hiyo wakati huu wa Mwezi wa Ramadhani ni kuleta mshikamano baina ya waumini wa Kikristo na Waislam.

Aidha, amewataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi pindi kampeni ya "No reform No Election" itakapofika kwenye Kanda ya Pwani.

 
Back
Top Bottom