Kama ukijaribu kupika wali ukashindikana kuiva vizuri ukabaki umegandamana kama liugali fulani uswahilini tunaita wali huo bokoboko, ndio neno boko linakotokea, na mpishi anaaibika sana kwa kushindwa kuivisha wali hivyo husemwa ametoa boko.
Msemo huu wa kutoa boko ukawa ni equivalent na kuharibu jambo, au kufanya hovyo fulani...
Hivyo wanaosema sitoi boko wana maanisha hawata haribu...
Usitoe boko = usiharibu