Bongo wataalamu wa michongo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo wataalamu wa michongo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Aug 7, 2010.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Ee bana eh! Nilikua nafuatilia mkutano wa mgombea urais wa jamhuri ya Tanzania kwa tiketi ya chadema, na macho yangu yakamwangukia sheikh mwaipopo akiwa amekaa kwenye viti vya wageni waalikwa. Hebu tusaidiane jamani na hasa kwa wale waliokaribu na protokali ya Chadema, amefikafikaje pale? Amealikwa tu kama kiongozi wa kidini ambayo ni haki yake au ni kwa maslahi ya kisiasa? Kama ni ya kisiasa basi chadema mkoa muwe macho huyu jamaa ni mtaalamu wa kula na mikono yote miwili tena bila hata kunawa. Yeye kwa mwezi mmoja anawezakuwa mwanachama wa vyama vinne tofauti. Ukija ugomvi wa matajiri kama wakati fulani huko nyuma kati ya Mengi na RA huyu mwaipopo alilamba mshiko kote kote. Kwenye sakata la mfanya biashara mmoja jijini na kiwanja cha waislamu alilamba toyota korolla. Hivyo watu wa namna hii ni wa kuwa nao makini kwani mwaka huu wa uchaguzi ni wa mavuno kwao.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mhhhh....

  Huu uchaguzi na uje upite...
  Nishachoka na habari za kijinga za uchaguzi...
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Napepata ufafanuzi wa kile kilichokua kinaendelea Dar kuhusu Mwaipopo. Mie sipo Tz nilimwona tu katika ITV habari. Hivyo nikaharakisha kutuma tread kumhusu maana namfahamu sana. Kumbe alikua pale kama kiongozi wa kidini ambae alisoma dua kwa upande wa dini ya kiislamu na basi. Hivyo naomba radhi kwa usumbufu uliowezajitokeza kwa hii tread hapa jamvini.
   
Loading...