Ni wimbo huu.
Jamaa anaitwa Omari Dimples akishirikiana na Ali KIBA. Video yake ni nzuri sana,hasa kwa kuwa ni wimbo ambao umempatiaa tuzo mbili kwenye KTMA, ina pozi tofauti miksa costume za humo sio zile za ki-Cabo Snoop, something I like, pia Kiba na Omari wamecheza vizuri na kamera miksa vocals za hatari sana.
Dimpoz amependeza, kisasa zaidi na Ali Kiba kama kawaida yake, huwa haongozwi na hisia za fashion, anavaa vinavyompendeza siku zote, and he's good. Mercedez Benz za humu ni hatari sana, kama sio Bongo vile, plus pozi flani za kimamtoni za kutembea na '
pet dog' zimeifanya video ikae kimamtoni zaidi. Dancers wa mule, ambao nimeambiwa kuwa wanaitwa
Dimpoz kwa Poz wametisha ile mbaya, kitu kinachoipa mvuto wa ziada video hii.
Tatizo langu lipo kwenye model wa video, hana kabisa viwango vya wimbo wenyewe, to be honest!
Ni demu wa kawaida, anaonekana ameenda umri kuliko kawaida, halafu amejichubua plus muonekano wa kikahaba, she ruined the video kwa kweli.
Tuishie hapo, next time nitawaeleza jinsi Hemed Ph.D alivyoboa kadiri ya uwezo wake.
Ingekuwa ni ratings hii ningeipa 8/10.