Bongo na barabara za juu

Playboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
1,170
Reaction score
945
Hivi ndivyo inavyotarajiwa kuwa mwonekano wa barabara ya juu eneo la Tazara, baada Serikali kutiliana saini ya makubaliano ya mkopo wa Sh52.5 bilioni na Serikali ya Japan kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo itakayokuwa na urefu wa kilomita 1.2.
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1371806276214.jpg
    18.5 KB · Views: 403
Kuna wimbo sijui walipiga Ddc,Msondo
Unaitwa "Naota naota Nadanganywa"


Acha tuone kama kuna ukweli maana
misaada itatuuwa bila hiyo kitu watu
wataiba wapi maana hapo lzm 10%
 
Tunashukuru kwa taarifa....wenzetu Zambia, Nigeria, Ethiopia n.k walishakuwa na hizi njia muda mrefu...Kenya nao wamejenga njia kama hizi hizi karibuni.
Ila najua kwa hapa kwetu hizo kilomita 1.2 ndio zitatumiwa na kina Nchemba kujitambishia kwenye majukwaa ya siasa
 
Tunashukuru kwa taarifa....wenzetu Zambia, Nigeria, Ethiopia n.k walishakuwa na hizi njia muda mrefu...Kenya nao wamejenga njia kama hizi hizi karibuni.
Ila najua kwa hapa kwetu hizo kilomita 1.2 ndio zitatumiwa na kina Nchemba kujitambishia kwenye majukwaa ya siasa.
Btw bado ninaona kuna watumiaji wa njia moja wataendelea kuwa wahanga wa foleni...na kwa haraka nahisi ni watumiaji wa Barabara ya Mandela...kwa kuwa hapo chini ya daraja sio a one way passage.
 
Kuna wimbo sijui walipiga Ddc,Msondo
Unaitwa "Naota naota Nadanganywa"


Acha tuone kama kuna ukweli maana
misaada itatuuwa bila hiyo kitu watu
wataiba wapi maana hapo lzm 10%
Broda,
Hayo mambo yana wenyewe!
Huyo ni Mbaraka Mwinshehe na Morogoro Jazz!
 

mbona barabara zenyewe hizo sio za viwango vya kimataifa, hata haziwezi kufananishwa na za Kenya.Hakuna hata design ya maana ni kama wanafuatisha ile ya chini wanairudia tena. Si walitaka wajenge Ubungo?Wanazijenga hapo ili wale wanaotoka uwanja wa ndege, watoa misaada wakija wazione,kujipendekeza tu na ufisadi uliotukuka.Ovyoooo kabisa.
 
Kwa ninavyo fahamu AZAM uliowataja hapo juu hawajajenga yale majengo bali wameyaboresha..iliyokua National Milling ndiyo walijenga!
mkuu Adrian Stepp sileti hoja kishabiki bali hata ukarabati wa Mandela rd umepelekea 'X' kwenye majengo yaliyoongezwa ukiondolea yale yaliyokuwepo awali. Mfano angalia kutokea uwanja wa ndege kuelekea mjini kuanzia maeneo ya Vingunguti, DT Dobie kuja kwenye makutano service rd ni kubwa na imekuwa blocked na majengo yaliyoongezewa karibuni tofauti na upande wa TAZARA walioacha nafasi. Labda kwa vile sijaja huko siku nyingi
 
Azam hakujenga pale mdau, alizawadiwa pale na serikali wakati wa che Nkapa walipochemka wakamwaga ngano ya bahresa wakisingizia haina ubora. Kumbe walichemka msafirishaji alikuwa hajakabidhi rasmi kwa bahresa si akafungua kesi ya kimataifa akashinda so ili kumpooza bahresa ndo akapewa hiyo mill. Kisa eti don bahresa alimsuport mrema enzi zile
 
Wabongo tusivyowezekana utaona au kusikia kuwa kuna Hiace imedondoka kutoka barabara ya juu hadi dauni. Na tutaenda mbali kidogo kwa kumtaka mkandarasi atuwekee matuta huko huko kwenye barabara ya juu. Hatuna nidhamu ya kuheshimu vivuko maalum vya pundamilia (hii ni kwa wote madereva na watembea kwa miguu).
 
Kuna wimbo sijui walipiga Ddc,Msondo
Unaitwa "Naota naota Nadanganywa"


Acha tuone kama kuna ukweli maana
misaada itatuuwa bila hiyo kitu watu
wataiba wapi maana hapo lzm 10%


Huo wimbo ni "Mashemeji" ulitungwa na kuimbwa na Mbaraka Mwinshehe.
Kiitikikio: Naota naota nadanganywa
Naota naota nadanganywa, ohoooo

Mbaraka: Kila mtu ni shemeji, imani nawe imeshanitokaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…