Bongo mchezaji bora wa mchezo mnaangalia vigezo gani?

Bongo mchezaji bora wa mchezo mnaangalia vigezo gani?

Papillon 1906

Senior Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
198
Reaction score
672
Jana katika mchezo wa Simba na Coastal Union mchezaji bora kapewa Chilambo, lakini kipa wa Coastal alikuwa bora zaidi japo aliconced goli moja.

Chuma Ramadhan golikipa wa Coastal kasevu mashuti saba kati ya nane yaliyo lenga lango.

Ni sawa na mechi ya laliga jana usiku kati ya Barcelona na Athletic Bilbao,Barca alishinda goli mbili lakini uyo unai Simon golikipa wa Bilbao alikuwa na savu bora kabisa.

Katika mashuti kumi yaliyo lenga lango kasevu nane japo mtu kama lamine yamal,pedri,lopez na wengine kuwa na kiwango bora lakini mchezaji bora kapewa kipa wa Bilbao.

Watu wa mpira watakubaliana na mimi
 
Chilambo alistahili ukiangalia save nyingi alizofanya kipa wa Coastal ni ilichangiwa na uzembe wa wachezaji wa Simba.
 
Chilambo alistahili. kumbuka alizima namba mbili. na muda mwingi alikuwa maeneo sahihi
 
Tanzania kipa akishafungwa hawezi kuwa bora nimeangalia mechi ya Barcelona pamoja na kushinda goli mbili mchezaji bora alikua kipa Unai na wachezaji wa Barcelona washambuliaji walienda kumpongeza kwa kuokoa magoli magumu baada ya mechi kuisha wenzetu wana vigezo vipo kwenye mashine na kila kitu ukifanya mikimbio yote inaongeza points sio hapa tunataka kuwachagua kwa upendeleo tu..
 
Back
Top Bottom