Hivyo vijumba navyo unaviita nyumba?
Well, ni wangapi Tanzania wanaoweza kumiliki hizo HSEs kwa kutumia riziki halali? Na hata hao wanaozimiliki, iwe kupitia njia halali au haramu, ni asilimia ngapi ya Watanzania? Inafikia hata asilimia 2? Sidhani!
Ni Watanzania wangapi ambao wako Tanzania wanaomiliki biashara, ofisi, na makampuni yao wenyewe? Tuzizungumzie hizo fursa kwa takwimu. Tuanzie na unemployment rate. Kwa Tanzania ni asilimia ngapi?
Lakini...iweje kila mara watu wanatusumbua tuwanunulie vitu huku majuu? Yaani hata manukato watu wanapenda ya huku. Kuna watu wanafanya biashara za kununua manukato na biadhaa zingine za Victoria's Secret, kwa mfano, na kuzituma huko bongo nyoso. Kwa nini unadhani?
Nami mtazamo wangu ni kwamba Tanzania bado ni nchi ya dhiki sana. Tu wategemezi wa mambo mengi sana. Hata vinywaji baridi vingi bado ni vya kigeni. Hiyo Coca Cola na products zake zingine ni za Kimarekani. Yes, Atlanta, Georgia's very own. Walau Azam wamekuja na cola yao lakini hata wao ni kuiga tu. Hakuna ubunifu hata kidogo.
Bottomline Tanzania opportunities bado sana. Kama mtu hauko well connected na/au kama huna deep pockets kwa kiasikikubwa we ulie tu. Lakini Marekani huhitaji kuwa na jina kubwa. Waweza kuitwa Nyani Ngabu na uka-make it vile vile. Hata usipokuwa milionea, if you work hard enough, if you play by the rules, and if you are disciplined , then you will lead a very decent life.
Halafu, hivi kwa nini huko bongo nyoso watu wanafuatilia sana yatokeayo majuu. Yaani unakuta mtu anajua kinachoendelea Marekani kuliko hata walio Marekani! Watu wanafuatilia TV series utadhani sijui nini. Hivi huko hamna TV series zenu hadi mfuatilie za Marekani na kwingineko?
Na mashauzi ya kujifanya hujui Kiswahili. Mtu akiongea maneno matatu basi ya Kiingereza lazima yawe mawili. Kwa nini iko hivyo?
kiongozi,asante kwa hoja zako,japo nimejiuliza hukuwa na chochote cha kuzungumza kuhusu nilichokizungumza ktk no 1?
well,sina hakika unakuja tanzania mara ngapi au hata ukija unachukua hata nusu sekunde kutathmini mabadiliko yanayotokea kila siku,cha muhimu ni hali ya kubadilika bila kujali yametokea kwa kiasi gani!najisikia vibaya kukuambia una mawazo na mitizamo isiyoendana na tanzania ya sasa!mambo yamebadilika mno kiongozi
1.siku hizi karibia kila kitu unachokitaka unapata tanzania,iwe kwa kuagiza mwenyewe au kununua dukani,kuna tofauti ndogo tu ya muda toka kitu kinatoka na kupatikana hapa!mfano hapa arusha product yoyote ya apple iliyoko sokoni huko kwenu inapatikana benson!hao wanaowasumbua kutaka muwaletee vitu toka mtoni wangewasumbua kutaka kununuliwa vitu hata kama mngekuwa hapa bongo!
2.kazi za sanaa za mtoni,kaka kama uliondoka tz enzi zile za vibanda vya kanda vimejaa album za kina rkelly na aaliyah na mikanda ya kina chuck norris na kinaijeria mambo yamebadilika mno kiongozi,siku hizi tunasikiliza nyimbo za kina diamond,tunaangalia movie za kibongo,hakuna tena comedy za steve tunaangalia futuhi na ze comedy,na karibuni wabongo wataanza kutoa tamthilia zinazobamba nitakujulisha tu,lakini siku hizi za ulaya na marekani yenu hatuangalii kaka,tunamalizia kuangalia za marekani ya kusini na asia kisha tutajikita kwenye zetu!mark my words!
3.kuhusu kufuatilia yanayojiri marekani ni ktk kutaka kujifunza kaka,wabongo siku hizi tunafyatua vitu vyetu wenyewe baada ya kujifunza sana toka huko,mfano sioni umuhimu tena wa kuangalia oprah show wakati ipo inayonigusa na kunibamba zaidi ya mboni show!hata video za music za bongo ni za ukweli sana lakini hiyo ni baada ya kujifunza toka huko walikoendelea zaidi walikokuendeleza wenzako ambako kwa hakika huna haki ya kujivunia maendeleo yaliyofanywa na wenzako katika nchi zao!
4.bongo ya sasa kufanikiwa huhitaji support au connection kama bongo uliyoiacha zamani,leo hii mtoto wa mkulima ni waziri mkuu,no wonder kesho mtoto wa mfugaji akawa rais!diamond mtoto wa tandale anamiliki assets za mamilioni ya tzs,na tena ninakuambia tena kwa herufi kubwa USISHANGAE NDANI YA MIAKA 20 IJAYO JINA LA TILLY CHIZENGA UKALIKUTA KTK LEVEL ZA ALIKO DANGOTE!tena nikifikia huko nikiwa hapahapa bongo!hapa ni kupambana tu ukiwa na malengo huku ukijua njia ya kuelekea mafanikio utafanikiwa tu kama ilivyo marekani
kwa kumalizia,opportunities zilizopo ulaya na kila kitu ambacho kipo ulaya na marekani hata kama leo hatuna au tunavyo kwa uchache na uhaba na uduni ni jukumu la kila mtanzania kuzitengeneza na kutengeneza yaliyo bora kwa nchin yetu!kuwa kwetu mbali na nchi yetu hakutufanyi tukaacha kufanya vitu kwa ajili ya nchi yetu,nikiwa kama mtanzania niliyeko ndani ya nchi yangu nahitaji kuiendeleza nchi yangu sio peke yangu bali kwa ushirikiano na watanzania wenzangu popote walipo DUNIANI ukiwamo wewe NN,hivyo ninaomba ushirikiano nawe/nanyi ktk kutekeleza adhma hiyo.KARIBU KATIKA UMOJA NA USHIRIKIANO