Unajua unapoongea kuhusu flyover hapa Bongo, watu wengine huwa wanadhani ni hadithi za Abunuwasi...Dar es Salaam ni kati ya miji iliyojichanganya na bado inataka iitwe Metropolitan.Makazi ya watu yamechanganyikana na sehemu za biashara, viwanda, stand za mabasi n.k kimsingi hakuna mpangilio mahsusi wa mji kwa maana halisi ya jina jiji.
Hizi habari za flyovers, na treni za mijini nimekuwa nikizisikia tokea enzi za John Samuel Malecela(yes Malecela yuele alikuwa Waziri Mkuu), tulishapewa ahadi lukuki lakini hayo yote yaliishia kwenye majukwaa ya kisiasa na vyumba vya pale Habari Maelezo.
Kwa miji ya wenzetu huko ng'ambo, UBT au ile terminal ya stand pale Tanesco huwezi hata kuipa hadhi ya Terminal maana ni vurugu tu na hata position yake sio rafiki kwa mazingira ya kibarabara. Zote zile mbili ilipaswa tu kuwa ni sehemu za kushusha abiria na wala sio kupaki mabasi na kurundikana.