Bongo kuliko uijuavyo ya Ubungo waachie vigogo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo kuliko uijuavyo ya Ubungo waachie vigogo...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, Sep 20, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,101
  Likes Received: 4,057
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana-JF,

  Hivi solution ya msongamano pale Ubungo ni kuondoa kile kituo tu? kwa uwezo wetu woote wa kufikiri, ni lazima Ubungo bus terminal iondoke kuninusuru Dar na msongamano? na itapelekwa wapi kwenye nafasi kama ile ndani ya Dar? na vipi kuhusu mali za wenye mabasi waliowekeza mle ndani kama wenye vituo binsafi na vituo vya mafuta na hotel? watafidiwa?

  Na suali nyeti zaidi nani atapewa ile nafasi pale baada ya kituo kile kuhama? tunaambiwa kuna vigogo wanapigana vikumbo kuchukua ile nafasi na hii ndo sababu kubwa zaidi ya kukiondoa kile kituo! Kwanini basi kama kuna mpango wa kujenga flyover Ubungo sioni sababu ya kushindwa kuunganisha junction ya kituo cha mabasi katika hiyo flyover! Kiufupi tu na kwa haraka nathani UBT haiihitaji kuwa na mlango wa kuingia na kutoka upande mmoja bali kuangaliwe uwezekano wa mlango wa kuingia kuwa upande wa Sam-Nujoma Road kwa maana ya mkango uwe kwa nyuma ya kituo kile na hii itasaidia ku-incorparate road exit katika fly-over itakayojengwa na kwa upande wa Morogoro Road basi kujengwe by-pass itakayohepa muingiliano wa mabasi kwa matumiaji wengine wa barabara! Hivi vitu vinahitaji wasanifu kukaa na ku-design si wanasiasa wenye madhumuni ya kufaidika na ile nafasi pale! Ikumbukwe the likes of Simba wako wengi tu wananyemelea ile nafasi na creativity kwao ni kuamishwa kwa kile kituo! na kwa kukisia tu kile kituo kitapelekwa Msoga na kukosesha jimbo la Ubungo mapato wanayopata kutokana na kituo kile! tusubiri tuone!

  Hii ndio serikali ya Kikwete tuijuavyo imekosa ubunifu kabisa! naomba Mnyika asikubali kituo kile kihamishwe pale kabisa ila kiboreshwe na kuwa cha kisasa yaani waiting room iwe indoor na parking za mabasi ziwe underground!  http://dailynews.co.tz/index.php/local-news/9703-dar-es-salaam-bus-terminal-cost-irks-kikwete
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,484
  Likes Received: 5,868
  Trophy Points: 280
  Nielewavyo mimi haihamishwi bali Mabasi yote yaendayo Kaskazini kupitia SEGERA stand yao itakuwa mahala ambapo kwa sasa pana milikiwa na DAWASA pale Boko. Mabasi ya kusini (LINDI na MTWARA) nayo yatakuwa na stand yao Mbagala. hapo ayatabaki mabasi yatakayokuwa yanapitia CHALINZE
   
 3. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Same thing itatokea hata kihamishiwe Mabwepande kama hakutakua na miundo fasaha ya barabara hapa DSM, Labda wakipeleke Singida ial kwa hapahapa DSM ni kuhamisha foleni toka hapa kwenda pale.
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,351
  Likes Received: 2,694
  Trophy Points: 280
  Unajua unapoongea kuhusu flyover hapa Bongo, watu wengine huwa wanadhani ni hadithi za Abunuwasi...Dar es Salaam ni kati ya miji iliyojichanganya na bado inataka iitwe Metropolitan.Makazi ya watu yamechanganyikana na sehemu za biashara, viwanda, stand za mabasi n.k kimsingi hakuna mpangilio mahsusi wa mji kwa maana halisi ya jina jiji.

  Hizi habari za flyovers, na treni za mijini nimekuwa nikizisikia tokea enzi za John Samuel Malecela(yes Malecela yuele alikuwa Waziri Mkuu), tulishapewa ahadi lukuki lakini hayo yote yaliishia kwenye majukwaa ya kisiasa na vyumba vya pale Habari Maelezo.

  Kwa miji ya wenzetu huko ng'ambo, UBT au ile terminal ya stand pale Tanesco huwezi hata kuipa hadhi ya Terminal maana ni vurugu tu na hata position yake sio rafiki kwa mazingira ya kibarabara. Zote zile mbili ilipaswa tu kuwa ni sehemu za kushusha abiria na wala sio kupaki mabasi na kurundikana.
   
 5. n

  ngala moja Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli serikali yetu ni sikivu.basi likitoka boko maana yake ni bagamoyo msata arusha. je mimi wa mailimoja kibaha siku naenda arusha maana yake nikalale tegeta kama sio bunju kabisa. si ndo mnamanisha hiyo au sijelew vizuri?????
   
 6. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Dah,kweli humu kuna magrit thinka,ebwana mimi sijui hawa wazee wa mabwepande kama huwa wanafikiria.....
   
Loading...