bongo fleva ziinaboa sana

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Hivi inakuwaje msanii wa kiume anaamua kuimba kama mwanamke. Mfano wimbo wa msanii mmoja ambaye hata simjui eti analalamika anateswa na mumewe kwa hiyo anaona bora arudi kwao kijijini akaendelee kukata mkaa, halafu eti anasema labda atayempenda hajazaliwa (realistically mwanamke hawezi kuwa na mawazo kama haya maana wao wanazeeka haraka kuliko wanaume kwa kawaida) muziki unatungwa bila kufikiri, halafu utashangaa eti wimbo kama huo una vuma na kuchukua nafasi kwenye chati zetu za kichovu za kibongo.

Kwa zamani nisingeshangaa kwa sababu hatukuwa na wasanii wa kike ndo maana hata kina Remmy ongala waliimba kama wanawake, lakini sio leo ambapo mtu unaweza kutunga wimbo na kuajiri mwimbaji wa kike.
Am so frustrated.
Jadili.
 
Seriously..frustrated?? Why...are u a music producer or?
 
Muziki kama sanaa unakazi ya kuburudisha na kuelimisha iwe kwa kukanya,kufunza,kuonya na keleza yaliopo ktk jamii iwe mabaya au mazuri.
Wimbo unao usemea unaburudisha na unafunza kwa kueleza hali hali huku ukitumia maneno ya kimapenzi ya kufikirika yanayotumiwa na jamii kama you're my angel,usiku silali nakuota wewe nk.
Sanaa haina miiko unayolalamikia wewe kwa mwanamme kuimba kwa nafasi ya kike nk,
Nilitegemea utatatizwa na nyimbo za kusifia bangi na mikasi na kujirusha kwa sana lakini unatatizika na jamaa kuimba nafasi ya kike.
Mwanamuzi bongo uli upate walau chochote lazima ubuni kitu kitawashika watu waupende wimbo wako na ndicho alichofanya jamaa na hii ni duniani kote watu wanafanya hivyo.
 
Kweli mkubwa, maana huelewi ni kitu gani wanaimba mfano ule wimbo wa shikide wa dully to me hauna maana wala ladha, just rubbish or gabbage to be precise.

Hivi ninyi mnajua sanaa kweli? Nakuombeni fanyeni utafiti wa nyimbo toka waliko endelea kama USA na usiishie kumsikiliza R kelly tu nenda ndani tafuta manyimbo ya house, country nk ndio utajua dully kaimba kitu
 
Mkuu la msingi sasa hivi ni kuangalia soko,sauti sio ishu,ingawa siwatetei lakini kama hana hiyo kipaji
ya kuimba kivingine atafanyaje?hivi bongo wanaume wangekuwa wanaimba nyimbo laini kama
boys to men au blues za kina R.Kelly tungewachukuliaje.
 
Unapozungumzia Bongofleva ni sawa na kuzungumzia Mdundiko, tena anona mdunduko unaafadhali kuliko huu Uchafu wa Bongofleva. Kama wanataka wawe wanamuziki waende shule wakasomee Music.
 
Ukisha sem neno msanii basi hana kosa kosa litakuwa kwako wewe ambae hujui maana ya msanii
 
Utaendelea kulalamika bongofleva huku mwenzako inapata kipato na hatemei ajira za Jk alizoahidi miaka 6 iliyopita
 
Mbona kina Eminen wanaimba vya ajabu, tena na matusi lakini ndo mnazipendaaa. Acheni unazi.
Jamaa kaimba, mwenyewe alidhani kaoa kumbe kaolewa. Ametoka ameingiza chake mfukoni, maisha yake yanaendelea. Wewe endelea kukereka.
 
Mkuu la msingi sasa hivi ni kuangalia soko,sauti sio ishu,ingawa siwatetei lakini kama hana hiyo kipaji
ya kuimba kivingine atafanyaje?hivi bongo wanaume wangekuwa wanaimba nyimbo laini kama
boys to men au blues za kina R.Kelly tungewachukuliaje.[/QUOTE

Tungewachukulia poa as long as hawasemi 'my husband. Return me home' sisemi wanaume wasiimbe nyimbo za mapenzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom