Bongo flavor- punguza maneno makavu - maoni

Bongo flavor- punguza maneno makavu - maoni

Ulimba

New Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
4
Reaction score
2
Napenda kutanguliza pongezi kwenu wasanii wa kizazi kipya a.k.a Bongo flavor kwa kazi nzuri ya muziki mnayoifanya kila siku hasa kwa kuielimisha jamii hasa kwa Watanznia na ulimwengu kwa ujumla.

Mimi ni mdau wa muziki japokuwa napenda nikiri kuwa sifahamiki sana kwa wanamuzi ni wachache sana ambao nimepata bahati ya kukutana nao si lazima kuwataja majina yao hapo ila wakiona jina hili watajua na napatikana kinondoni maeneo ya MANYANYA nimeingia kwenye mambo ya Burudani muda wa miaka tisa iliyopita kwenye suala zima la burudani kwa leseni ya kufanya EVENTS MANAGEMENT.


Lengo langu kubwa hapa sio kuitambulisha kampuni bali nikiwa mdau wa muziki naomba kutoa maoni yangu kwa wasanii wetu hasa kutokana na lugha ambayo baadhi ya wasanii huwa wanazitumia katika baadhi ya tungo zao, ki ukweli ni za kawaida tu lakini maneno yanayotumika yanakuwa ya wazi mno hayatumiki kama fasihi kwani kutokana na maadili yetu kuna maneno yanatakiwa yatumike kama mafumbo ili watoto wasiweze kujua ya maanisha nini hadi watakapokuja kuwa watu wazima pia kuna maneno yanatumika ni yakibaguzi kiasi kwamba baadhi ya watu wanaonekana hawafaii katika jamii yetu.
Hapa nitanukuu baadhi ya maneno katika nyimbo nne tofauti samahani sitataja nyimbo kaimba nani kwaa wewe mtuzi au mdau wa muziki utakuwa unafahamu ni nani kaimba hicho kipande naanza kwa kwa kunukuu

  • "NDUGU ZANGU MSINICHEKE MIMI MPENZI WANGU BUBU"
  • "NZELA UMEPEWA MIMBA TENA NA MPIGA DEBE"
  • "UKIWA MJANJA KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI"
  • "MPENZI WANGU NIPE KAVU WEWE MTAMU ZAIDI YA ASALI"
Mwisho wa kunukuu, hayo ni baadhi tu ya maneno yaliyotumika katika hizo nyimbo sielewi hata baraza ambao wana wajibika katika kupitisha hizi nyimbo kweli wapo?
Ukianza na sentesi ya kwanza huyu ni mwanamuzi kwa mtazamo wangu ni mtu mwelewa sana tu je unadhani kwa sababu gani wewe uchekwe kisa umempenda BUBU? Kuna umbaya gani jamani?? Sio kituko ni mtu ana haki sawa na mtu mwingine yeyote huu ni ubaguzi je bubu anajikiaje kuhusu kauli kama hiyo??

Pili hapa mtuzi analalamika kuwa dada yake kaacha masomo kapewa mimba TENA NA MPIGA DEBE kweli dada mtu kafanya makosa kukimbia nyumbani kauli ya tena mpiga debe hapo ndio kuna nipa utata mimi kwani mpiga debe sio mwanaume je mwanaume gani alifaa kumpa hiyo mimba???

Nenda sokoni kariakoo pale kwenye ma dala dala ya kwenda mwenge, tegeta na kunduchi kuna wapiga debe wengi wanafamilia zao wanasomesha watoto kwa kazi hiyo, nenda ubungo stand ya mkoa kuna wapiga debe wengi tu wanaishi na kulea familia zao kwa kupiga debe. Katika jumuhia yoyote kuna watu imara na wadhaifu pia, kuna walevi, wavuta unga mbona hata baadhi ya wasanii ni mateja kama baadhi ya wapiga debe mbona hamuowaoni sio kweli kwamba wapiga debe wote wana vitendo viovu.

Kipengele cha tatu dunia ya sasa hivi imejaa utandawazi neno KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI hakika linaeleweka sana na hata vijana wadogo jamani punguzeni ukali wa maneno.Umeisha sema siri ya ndani je unadhani kwa akili ya kawaida tafsiri ya kawaida kuna kitu kinafichaka hapo ??.

NNE hakika hapo ni aibu kubwa sana kusikiliza maneno hayo mbele ya watoto, wakwe na wakubwa wetu wote kiujumla kauli kama hii -NIPE KAVU??

WEWE MTAMU??? ZAIDI YA ASALI tutafika kweli jamani tutalea kweli watoto kwa misemo kama hiyo?? Tubadilike hii miziki inasikilizwa na watu wengi sio mnavyodhania kuwa ni vijana tu ila maneno kama hayo watu wanaojiheshimu yanawavunja moyo na kushindwa kununua kazi zenu,watu wengi wamepata mafanikio makubwa ya muziki sio kwa kutumia maneno kama hayo.

MWISHO najua kila mtu anamtazo wake tofauti yangu ni hayo kama kuna mtu amekwazika pole sana lakini uhuru huo ninao wa kutoa maoni ili mradi sijavunja sheria ya nchi yetu na wala sijamtukana mtu, wasanii mnakaribishwa tufanye kazi tumejipanga kufanyakazi ya muziki wasiliana nasi
 
Back
Top Bottom