Bonde la mto Boko via National

Frank King

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
1,311
2,000
Awali ya yote kabisa mimi si muandishi wa habari ni msamaria tu ktk hili hivyo msinihukumu km nitakosea kwa namna moja!

WAANDISHI WA HABARI MPO?
Basi kwa heshma kabisa nawaomba mfuatilie hili jambo.
Ukitoka Tegeta kuelekea Bunju kunakituo kinaitwa kwa MPEMBA mbele yake kidogo kuna Daraja..shuka chini ya Daraja kisha anza kutembea ukilifuata hilo bonde yaani panda kama unaelekea National housing upande wa kulia usiende kushoto.

Nenda tu fuata hilo bonde hatimae utakutana na MKATAPILA MKUBWA..kisha utawaona Wahindi wanaosimamia huo mradi..Ni Wahindi wenye kile Chuo cha Mt.Joseph Bunju.
Binafsi nilikuwa ktk pitapita zangu nikakutana na hawa jamaa,Nimejaribu kuwahoji kwanini wanachimba huo mto vibaya namna hiyo?wakasema wamepewa tenda na Serikali yakuusawazisha huo mto wote kipindi cha mvua pasiwe na uharibifu kwenye makazi ya watu

Sikuishia hapo bali nilihoji aliyewapa mamlaka hiyo ni nani..wakasema Ni Serkali kupitia Manispaa ya kinondoni inajua na Mkuu wa Mkoa anajua..
kwamba wanatengeneza huo mto/Bonde

Sasa ugonvi wangu ulikuja pale nilipo hoji hivi:
Kama mmepewa tenda yakutengeneza Bonde..mbona sasa haya magari yote zaidi ya ishirini yameunga foleni kubeba mchanga na hii ipo ndani ya tenda?hapo ndipo wahindi walipokuwa mbogo yaani wakali kama pilipili

Nilishindwa kupiga hata picha walinishtukia nikaamua kuondoka huku nikisindikizwa

Nia yangu nikuwajuza waandishi muende hapo km inawezekana illi muhoji kwa undani Watanzania tujue isije ikawa ni kale kamchezo ka Tanzanite one!!

Muhubiri Injili ya
Yesu wa Nazareth.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom