Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Hali siyo shwari polisi wanalipua mabomu watu wamejeruhiwa

Bomu lililolipuka limejeruhi watu sana. Inaonekana bomu lilitegwa karibu na gari la matangazo.

Mtoto aliyelipukiwa na bomu amefariki uwanjani.

================
Kutoka kwa Dr. Slaa:
================

Wana Arusha,

Kwa masikitiko makubwa, Mimi na mama Slaa tumepokea tukiwa Munich Ujerumani kwa masikitiko makubwa tukio la kulipuliwa Bomu katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Arusha.

Tunatoa pole kwa familia zote za waliopoteza maisha katika tukio Hilo na pia tunamwomba kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioumia kwa namna mmoja au nyingine na kuwapa faraja na neema kubeba maumivu waliyopata.

Chadema tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tunamaliza na Mungu. Kama mtu asiye na dhamira na ubinadamu, awaye yeyote, na kwa sababu yeyote ile amefanya hivyo, katika hatua hii ni Imani yangu kuwa Damu ya ndugu zetu hao haitapotea bure. Kwa damu hiyo watanzania tushikamane zaidi, kuwaombea waliotutangulia mbele ya haki, lakini damu hiyo ituunganishe zaidi katika kupigania Tanzania isiyo na maonevu ya aina yeyote ile.

Hali hii sasa haivumiliki tena. Nchi inayoyoma, na hatuwezi kuendelea kutazama nchi inaporomoka. Tukiisha kutoa tahadhari miaka miwili iliyopita hawakutusikiliza. Hakuna Maisha ya Mtanzania hata mmoja kupotea katika mazingira yanayopaswa kuwa ya Amani. Uchaguzi kimsingi unapaswa kuwa tukio la Amani. Jukumu la kuhakikisha Amani ni la serikali na hakuna sababu ya kigugumizi Serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa msingi.

Roho za Marehemu zipumzike kwa Amani.

===========================
Updates toka kwa Washiriki
===========================

Mkutano ulishaisha, Mbowe akaanza kukusanya michango kama ilivyo kawaida kwa mikutano ya CHADEMA, ndipo ghafla kijana mmoja aliyekuwa amevaa kaptula ya jeans iliyoraruka kidogo akarusha bomu wakafa watatu

"kijana mdogo kabisa ameuwawa. Ana tundu sehemu ya kifuani kushoto. Kwenye moyo. Inadhaniwa ni risasi. Hospitalini Mount Meru wanasema wamempokea akiwa amekufa tayari.

Kijana mwingine mdogo amejeruhiwa sana kichwani, kiasi kwamba ubongo unatoka yuko Mount Meru. Watu walioumia ni wengi sana sana. Mwenyekiti Mbowe amekwenda Selian Hospitali na Mount Meru Hospital na sasa pamoja na Lema wako eneo la tukio.

Mwenyekiti wa BAWACHA Kata ya Elerai, Judith Molley naye amethibitika kufa. Yuko AICC Hospitali. Ana majeraha makubwa kichwani na mguu wa kushoto. Hapa ICC pia wamepokea vijana wengine 2 wamejeruhiwa vibaya, miguuni ma mikononi.

Mmoja ana miaka 5.5 na mwingine ana miaka 14. Wamekimbizwa KCMC.

Hii ni taarifa ya msemaji wa jeshi la Polisi.

" kufuatia tukio lililotokea maeneo ya Soweto mkoani Arusha la mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, ametuma timu maalum kutoka Makao Makuu ya Polisi ikiongozwa na kamishina Chagonja na kamishina Mngulu kwenda kuongeza nguvu mkoani Arusha. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa eneo la tukio mkoani Arusha.
Advera Senso- Msemaji Jeshi la Polisi".

Bomu limelipuliwa leo katika Mkutano wa CHADEMA Arusha watu kadhaa wamekufa na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa. Wananchi walimuona mlipuaji walipojaribu kumfukuza ili kumkamata polisi wakaanza kuwatawanya kwa mabomu ya machozi hatimaye mhalifu akatokomea kwa msaada wa mabomu ya machozi ya polisi. Tutawaletea taarifa zaidi kadri tutakavyozipata
Katika Mlipuko huu wa Bomu Arusha wamefariki watu wawili mpaka sasa. Mtoto mmoja na Mama Judith Moshi ambaye aliwahi kuwa M/Kiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Wilaya ya Arusha Mjini na mpaka mauti yanamkuta alikuwa ni Katibu wa Chama Kata yaSokoni 1
Huko Ulanga Katika Kata ya Minepa yenye Uchaguzi CCM wamevamia ofisi ya Kata ya CHADEMA na kuwakata kwa Mapanga Viongozi waliokuwa ofisini humo wakipanga maswala wa Mawakala wa kesho. Waliokatwakatwa na Mapanga na kujeruhiwa vibaya ni M/Kiti wa CHADEMA Jimbo la Ulanga Magharibi Mh.Mohamed Kibamu na Katibu wake Mh. Lucas Lihambalimu hivi sasa wamelazwa hospitalini hawajitambui. TULAANI UNYAMA HUU. "CCM ACHIENI MADARAKA KWA AMANI. TU WAPOLE LAKINI SIO WADHAIFU NA TUNA NGUVU"
Huko Iringa Katika Kata ya Ng'ang'ange Wilaya Kilolo M/Kiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Lunyiliko Nyaulingo amevunjwa Mkono na kutobolewa na kitu kichwani. Na katika Kata ya Mbalamaziwa huko Mufindi Mwanachama wa CHADEMA amekatwa kichwani na vijana wa CCM na kushonwa nyuzi nane.


attachment.php

attachment.php


PICHA ZAIDI TEMBELEA HII POST -> https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-wahofiwa-kupoteza-maisha-25.html#post6590788
 

Attachments

  • arusha-bomb.jpg
    arusha-bomb.jpg
    90.8 KB · Views: 21,586
  • maiti.jpg
    maiti.jpg
    62.9 KB · Views: 26,230
Sababu nn hasa??weka na picha kidogo km hupo eneo la tukio au tupe source of that information!
 
Ni kwenye Mkutano wa Kampeni wa CHADEMA leo hii.Nawatafuta Viongozi pamoja na Mbunge kwenye simu muda huu sijawapata ila nimeongea na Mungi ambaye ni member wa hapa JF muda huu.Ameniambia majeruhi ni wengi,watu wamezirai.Naendelea kutafuta updates

Haijulikani Mlipuko huo umetokeaje hadi muda huu maana alishindwa kunieleza kutokana na kelele na taharuki zilizokua eneo hilo
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida bomu la kurusha kwa mkono limerushwa baada ya kamanda Mbowe kumaliza kuhutubia na hatimaye limeua watu kadhaa. Hali ni ya hatari kwa sasa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Watakuja na propaganda CHADEMA waliwategeshea wananchi wao bomu kwenye mkutano wao...
 
Ndio maana baba mwenye nyumba kakimbia ili watu wake wafanye wanavyotaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom