BOMU la LISSU jijini ARUSHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BOMU la LISSU jijini ARUSHA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Sep 3, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Wakili Msomi Tundu Antipas Mughwai Lissu ameacha mwangwi kwenye Mkutano wa Mawakili-AICC Arusha. Ameonesha jinsi asivyotetereka na kusimamia anachokiamini. Amethubutu kusema na kuwaita Mawakili 'waoga' na watetezi wa vibovu.

  Katika moja ya michango yake,Wakili Lissu alimuumbua Jaji Dr.Feuz Twaib(ambaye pia Mwalimu Shule ya Sheria ya Tanzania na Wakili) kwa kumwambia kuwa punde tu,miezi michache iliyopita,aliandika hukumu 'mbovu' na isiyostahili ambayo 'imechanwachanwa' na Majaji wa Mahakama wa Rufani na kutupiliwa mbali.Hukumu a Jaji Twaib ilikuwa ni kwenye kesi ya Yusuph Manji dhidi ya Kampuni moja ya Saudi Arabia.

  Uchunguzi wa nyaraka za Wakili Tundu Lissu unaonesha kuwa katika kesi hiyo iliyokuwa mbele ya Jaji Rugazia wa Mahakama Kuu,pande husika za kesi zilikubaliana nje ya Mahakama( Settlement out of Court) na Jaji Rugazia akaridhia makubaliano hayo na kuyafanya Amri ya Mahakama. Ni utaratibu unaokubalika kisheria.

  Siku si nyingi,Wakili Majura Magafu alijitokeza Mahakamani,kwa niaba ya Manji kuomba Marejeo(Review) ya Makubaliano hayo. Kisheria, Marejeo hufanywa na Jaji aliyeamua kesi husika.Jaji Twaib anajua hilo fika. Jaji Twaib,akiwa hausiki na Amri ya mwanzoni,alitengua Makubaliano ya pande za kesi. Akafanya 'blanda'. Akafanya jambo haramu kisheria.

  Wakili Lissu hakuogopa uwepo wa Majaji na Mawakili Waandamizi kama vile Jaji Dr.Feuz Twaib,Prof. M.K.Wambali,Jaji Joseph Sinde Warioba,Jaji Mstaafu Thomas Mihayo,Jaji Victor Makaramba,Wakili na Rais wa Mawakili Tanganyika Francis Stolla na wengineo. Mkutano ukageuzwa Semina. Lissu akatoa mafunzo thabiti.

  Aliposimama Jaji Twaib, ambaye alionekana mnyonge, aliwaomba Mawakili waende wakaisome hukumu husika na kujiridhisha na tuhuma za Lissu.Katika siku nilizojiona sina maana katika jamii hii,siku hii ya Lissu inaoongoza. Wakili Lissu akanifanya nirudi Dar kwa basi badala ya ndege kama nilivyopanga.
   
 2. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,657
  Trophy Points: 280
  aisee kumbe majaji na mawakili wapo jando arusha eenh!
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa ni Mkutano wa Mawakili.Umeshaisha.Kuna Majaji ambao pia ni Mawakili.Ndio maana wakawepo Mkutanoni
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Tuwekee hotuba nzima ya huyu mteule na mtetezi wa wanyonge
   
 5. M

  Mgengeli Senior Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chezea LISU weye
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  bravo lissu hajaogopa vituko vya majaji kama watamfanyia makusudi katika kesi zake
  amekuwa mkweli na hajaogopa kwa vile yeye ni mtu wa haki na mkweli
  muda wa kuwanyenyekea majaji wanaoandika hukumu 3 kwa mwaka umeisha
  muda wa kuwanyenyekekea majaji wanaoahirisha kesi hata kama ni mention kwa miezi 4 umeisha
  muda wa kuwanyenyekea majaji wanaopanga kesi kwa siku bila kuweka muda maalumu umeisha
  kwani mawakili wanajikuta wanafika asbh mahakamani na kuondoka saa 10 kwa kusubiri
  pawepo sasa tume ya kuratibu utendaji wa majaji na kuwawajibisha wazembe wanaopenda kuitwa waheshimiwa
  lakini utendaji wao kazi ni zero.
   
 7. M

  Malova JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Amesha zoea kutoa makavu kama yalivyo
   
 8. M

  Mgengeli Senior Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chezea LISU weye
   
 9. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Utamu ukiijua mizania ya sheria bwana, hivi kwanini tusiwe tunaiga vitu kama hivi vya msingi? Tuachane na mambo yasiokua na tija maishani, kama vile kumaliza mzinga wa konyagi, kula mbuzi mzima na mkia maini sijui kuku na mayai manyoya takataka kibao.
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu hapa nimejifunza kumbe kuna Majaji ambao ni mawakili!! ok i read between the line learned Brothers.
   
 11. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  dah kwakweli nimesikitika sana , jaji twaibu namheshimu sana pia kama mwalimu wangu, anauwezo mzuri sana, hili suala nalazimika kulifuatilia kiundani.
   
 12. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Fanya hivyo kijana.Amekufundisha UDSM au Law School of Tanzania?
   
 13. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  unadhani kuitwa jaji ni ujanja ujanja,wajibu sasa risasi za bwana lisu,ujanja hautakiwi jamani,sasa familia za hao majaji zinajifunza nini
   
 14. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ..." Heri Dr Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge...." !

  JK Campaign Rally 2010.
   
 15. s

  souvenir Senior Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 24, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuvaa kofia mbili kutakuwa na conflicts of interest walikuwaga mawakili kabla hawajateuliwa kuwa majaji so ile kofia ya uwakili wameivua kwenye mkutano wanaenda kama waalikwa
   
 16. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mhe, Wakili Antipas Tundu Lissu (MB)-Huyu ndiye waziri wangu wa sheria na katiba,chezeya lissu wewe
   
 17. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Baba kaenda kazini Arusha,kumbe wasijue lissu yuko anampiga makwenzi
   
 18. K

  Kiguu na njia Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  akili the brain....!! Mhe. Lissu big up..!
   
Loading...