Bomu la Arusha : Utawala wa CCM kwa sasa una mapungufu


makoye2009

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,644
Likes
502
Points
280
makoye2009

makoye2009

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,644 502 280
Baada ya mlipuko wa Bomu la Arusha na kuua watu 3 kwa uchache na kujeruhi kadri ya watu 70 ni dhahiri kwamba kwa sasa CCM wameamua kuitawala nchi kwa mabavu kwa kuminya Demokrasia na kugandamiza wapinzani kadri iwezekanavyo ili waendelee kuwepo madarakani kama anavofanya Bwana Bashar al-Assad ni Rais dikteta wa Syria.

Tangu Uchaguzi Mkuu wa Rais na Bunge mwaka 2010 na matokeo kuonyesha kwamba CCM imeanza kupoteza mvuto walipopoteza majimbo muhimu katika Miji na Wilaya nyingi nchini kwa kuchukuliwa na CHADEMA sasa CCM wameamua kuwashughulikia CHADEMA kwa kila mbinu. Hapa chini ni viashiria vya namna CCM wanavyowabana CHADEMA ili wasifurukute.

Tumeshuhudia matukio mengi sana mpaka sasa yanayofanywa na Serikali ya CCM dhidi ya Kambi ya Upinzani katika kila kona ya nchi hii. Tumeshuhudia Wabunge na Viongozi wa CHADEMA wakikamatwa na kubambikiwa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu na zisizokuwa na mbele wala nyuma.

Tumeshuhudia milipuko ya Mabomu kwenye Mikutano na Maandamano ya Upinzani hasa kwa CHADEMA.

Tumeshuhudia hoja na mawazo ya Wabunge wa CHADEMA zikizimwa,kukataliwa au kutolewa nje ya Ukumbi wa Wabunge kwa visingizio vya kufanya vurugu.

Tumeshuhudia sera na ilani za CHADEMA zikitekwa na kugeuzwa na CCM kama sera zake ili kuwashawishi Wananchi kuwa Serikali ya CCM ni sikivu.

Kwa shuhuda na viashiria hivi ni wazi kwamba tunakoelekea kutakuwa kugumu zaidi na Uchaguzi Mkuu wa 2015 utakuwa mgumu sana ambavo haijawahi kutokea tangu nchi hii ipate Uhuru. Kuna hatari ya kumwagika damu nyingi sana kwenye Uchaguzi Mkuu ujao na hali itakuwa mbaya zaidi kama CCM wataondolewa Madarakani kwa njia ya sanduku la kura na Wananchi na hivo kushindwa kuingia Ikulu!!!

Kwa aina ya Watawala walioko ndani ya CCM kwa sasa, kina Nepi Nauye, Mwigulu Nchemba,Steven Wassira,William Lukuvi,Edward Lowasa,Emmanule Nchimbi,Andrew Chenge na wengineo hakika naona nchi kutumbukia kwenye lindi la giza nene!


Wasaalamu.
 
Lekakui

Lekakui

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,448
Likes
54
Points
145
Lekakui

Lekakui

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,448 54 145
Yote hayo mbona mwisho wake umekaribia?nadhani cha kwanza ni kumake sure daftari la wapiga kura linafanyiwa uptodate na kuingiza vichwa ambavyo vilikuwa havijaqualify kwa umri,secondly ni kujitokeza kwa wingi sana kujiandikisha na kupiga kura 2015,baada ya hapo majibu ya maswali haya yoooteeeeeeeeee yatakuwa yamepata majibu
 
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Messages
764
Likes
2
Points
33
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2012
764 2 33
Ccm shimo la mavi hata nikipewa life ban hio sio dawa
 

Forum statistics

Threads 1,273,108
Members 490,297
Posts 30,471,653