Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 11,572
- 16,047
Umofia kwenu wadau,
Yaani ni maajabu kwa upinzani wa Tanzania.
Enzi zile Mh. Mbowe aliwahi kusema anao ushahidi wa aliyerusha bomu pale Arusha, na tena alienda mbali zaidi kwa kusema anao ushahidi wa video. Ila huo ushahidi haukuwahi kutolewa, na watu waliumia. Sasa kwenye hili sakata la Mh. Lisu iko hivyo hivyo, anasema eti ushahidi anao. Yaani hivyo hivyo hata kwenye uchaguzi, wakishindwa wanasema ushahidi wa kuibiwa kura wanao, yaani hivyo hivyo hata kwenye wizi na ufisadi wa Mh. Lowasa waliwahi kusema wanao ushahidi.
Basi naamini hata ktk hili wanawadanganya wafuasi wao, Mh. Mbowe hana ushahidi kabisa. Tusubiri polisi ndiyo watakaotupatia majibu ya wahusika baada ya upelelezi kukamilika.
Pia nadhani wanasiasa kama Mbowe ni hatari sana kwa usalama wa taifa!
Mbowe alisema "...Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,baada ya kutembelea majeruhi katika Hospitali ya Selian, Mbowe alisema chama chake kina ushahidi wa kutosha juu ya askari huyo kurusha bomu.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,alisema wamefanikiwa kupata ushahidi wa kutosha juu ya tukio hilo baya linalochafua taswira ya nchi.
Alisema chama chake kipo tayari kuweka ushahidi huo hadharani, iwapo Serikali itaendelea kufanya siasa na kuficha ukweli.
“Tunao ushahidi wa kutosha, ikiwamo wa picha za video unaoonyesha shambulio la bomu na risasi lilivyofanyika katika mkutano wangu jusi eneo la Soweto."
“Picha zinaonesha wazi aina ya silaha zilizotumika kwenye shambulio lile ni tatu, bomu la gurumeti ambalo lilitupwa na askari wa FFU aliyekuwa kwenye uniform.
“Kutokana na ushahidi huu tulikuwa tumewaeleza Polisi kama wataendelea kuficha tutaueleza umma na tutaiambia dunia, kwani aina ya silaha zilizotumika ni SMG na bastola.
“Makasha ya risasi kama ushahidi wa jambo hili zilizotumika tuliyaokota eneo la tukio na tayari tumeyarekodi na kuyakabidhi kwa askari waliokuwa wakichunguza tukio lile,” alisema Mbowe....."
Soma zaidi: JESHI LA POLISI NDIYO WALIORUSHA BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA,ASEMA MBOWE NA USHAHIDI ANAO. ~ KAHAMA FM 90.8