Bomoabomoa yaacha simanzi Mabwepande, nyumba za matajiri zaachwa

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Imezuka taharuki kwa baadhi ya wakazi wa Mabwepande Wilaya na Kinondoni wanaodaiwa kujenga eneo lisiloruhusiwa, baada ya nyumba zao kubomolewa huku wakiwa hawajui la kufanya na familia zao.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi kuhusu ubomoaji huo ulioanza Julai 4, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Hamza alisema ubomoaji unafanyika kwa wale waliovamia maeneo ya Serikali huku akieleza notisi ya kufanya hivyo waliitoa tangu Aprili mwaka huu.

“Tulifika Mabwepande kama Serikali ya Wilaya tukazungumza na wananchi, nao walieleza malalamiko yao na tuliwataka wote waliovamia maeneo wahame kwa sababu yanatakiwa kuendelezwa,” alisema.

Kuhusu baadhi ya nyumba kutokuvunjwa, Mkurugenzi huyo alisema hafahamu hilo isipokuwa anatambua wale wote waliovamia nyumba zao zinapaswa kuvunjwa. “Kama kuna watu hawavunjiwi suala hilo nitawasilisha kwenye kikao chetu cha kamati ya ulinzi na usalama, manispaa tunasimamia sheria wote lazima waondoke,” alisema.

Wananchi waeleza

Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia wananchi wakiwa wamekaa vikundi na familia zao huku nyuso zao zikiwa na huzuni huku baadhi wakilia wakidai wametumia gharama kubwa kujenga nyumba hizo ikiwemo kuchukua mikopo benki.

“Ndoto ya kumiliki nyumba kuishi na familia yangu ilishatimia. Nimetumia Sh30 milioni hadi kukamilisha, cha ajabu zimekuja kuvunjwa bila taarifa, tena kwa kupigwa mabomu. Nimebaki kama nilivyo na watoto wangu wanane,” alisema Saimon Nkya.

Alisema walianza kuishi eneo hilo mwaka 2003 na Serikali ya wilaya iliwapimia maeneo hayo na kuwapelekea huduma muhimu kama maji na umeme.

Alfonsia Kisanga, mama wa watoto watano alisema amelazimika kuwasafirisha watoto wake kwenda mkoani kuishi kwa ndugu ingawa bado wanasoma.

“Watoto wangu wanasoma chuo sitaki waendelee kupata shida hapa, sina makazi tena na mpango wa kuwasomesha nimesitisha kwa muda hadi nipate makazi ya kudumu . Serikali haitutendei haki hata kidogo.

“Tunaiomba Serikali ichukue hatua, kwani tunahangaika na familia zetu na hatuna sehemu ya kujihifadhi. Matajiri nyumba zao zimeachwa, ila sisi wa hali ya chini ndiyo nyumba zetu zimebomolewa.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyo DED aache uongo kuwa hajui. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ni DC, na siku ya uvunjaji DC Gondwe alikuwepo. Hivyo huyo DED anayesema ataitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama nikupotezea hilo swala kisiasa.
Ukweli ni kwamba wenye mijengo ya maana iliyokamilika haikuvunjwa, waliovunjiwa ni wale wenye chumba kimoja, viwili na nyumba ambazo hazijakamilika au ambazo siyo kali.

Bomoa bomoa ililenga eneo la NSSF. Ila wazito wanaoishi kwenye eneo hilo na eneo jirani linalopakana na nssf wakaamua kuwaondoa maskini katikati yao ili mji ujengeke (noble neighbour hood)kwa madai kuwa nako ni eneo la serikali(nssf). Kote kulikobomolewa ni maeneo ya uvamizi hivyo hata hao vigogo nao walivamia au kuuziwa na wavamizi ila hawakuguswa
 
Mabwepande mwezi uliopita Gondwe alienda na meneja wa psssf kuwaeleza wananchi waliovamia na kujenga kwenye uwanja wa psssf bila wao kujua maana wengi waliuziwa na madalali matapeli.

Ila ukweli wa mambo ni hata hao psssf hakuna aliyewahi kuwa na taarifa kuwa wanamiliki maeneo makubwa sana mabwe pande.

Nadhani wenye eneo wanaondoa wavamizi sasa.
 
Kimara walibomolewa na fedhuli hatukusikia vigelegele leo huu utu wa kujali watu unatoka wapi???
Unafiki huu
Jamaa ana bidii sana ya kuponda kila kinachofanywa na serikali kipindi hiki, wakati kipindi kile alikuwa anasifia kila kitu na kufikia kusema wanaoisema serikali ile ni aidha wapinzani, mafisadi, waliotumbuliwa kwa vyeti feki na wengineo. Nadhani alikuwa mnufaika na sasa hanufaiki.
 
Ukweli ni kwamba wenye mijengo ya maana iliyokamilika haikuvunjwa, waliovunjiwa ni wale wenye chumba kimoja, viwili na nyumba ambazo hazijakamilika au ambazo siyo kali.
Mara nyingi maskini ndiyo wanajenga kiholela na hawafuati taratibu za majenzi..

Naunga mkono wenye chumba kimoja kimoja kivunjiwa. Unajengaje chumba kimoja?
 
Hii nchi watu wamezoea kufanya mambo kimagumashi. Japo serikali inabeba lawama kwa kutosimamia sheria na baadae kukurupuka lakini wananchi nao wamezoea kufanya mambo kienyeji. Bora wabomoe ili wapate akili.
Serikali ijenge nyumba za bei na nafuu iwauzie wananchi walipe kdg kdg hata kwa miaka 20, mbona wamepewa pesa na mwarabu wameweza kule Tanga?
 
Huyo DED aache uongo kuwa hajui. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ni DC, na siku ya uvunjaji DC Gondwe alikuwepo. Hivyo huyo DED anayesema ataitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama nikupotezea hilo swala kisiasa.
Ukweli ni kwamba wenye mijengo ya maana iliyokamilika haikuvunjwa, waliovunjiwa ni wale wenye chumba kimoja, viwili na nyumba ambazo hazijakamilika au ambazo siyo kali.

Bomoa bomoa ililenga eneo la NSSF. Ila wazito wanaoishi kwenye eneo jirani linalopakana na nssf wakaamua kuwaondoa maskini katikati yao ili mji ujengeke (noble neighbour hood)kwa madai kuwa nako ni eneo la serikali(nssf). Kote kulikobomolewa ni maeneo ya uvamizi hivyo hata hao vigogo nao walivamia au kuuziwa na wavamizi ila hawakuguswa
Polen wahanga wa mabwepande hii ndio TZ kama unamaisha magumu haki ni yako lakin huwez kuidai.
 
Back
Top Bottom