Bomoabomoa kuanza barabara ya Mwenge-Morocco (Dar)

Bomoabomoa kuanza barabara ya Mwenge-Morocco (Dar)

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,629
Reaction score
6,812
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli ameitaka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kuanza kuvunja nyumba zilizopo ndani ya hifadhi ya Barabara ya Mwenge hadi Morocco, Dar es Salaam ili kupisha ujenzi wa barabara nne za lami.

Pia, ameitaka Tanroads kuacha kigugumizi katika ujenzi wa barabara za juu jijini Dar es Salaam (flyovers) kwa kuwa fedha kwa ajili ya kazi hiyo zipo.

Waziri Magufuli alitoa wito huo Dar es Salaam jana, alipokuwa akizindua bodi mpya ya Mfuko wa Barabara na Bodi ya Tanroads.


“Barabara ya Mwenge- Morocco nyumba zinatakiwa kubomolewa. Zibomolewe haraka ili kupisha ujenzi. Nasema Tanroads acheni kigugumizi kwenye masuala haya,” alisisitiza Dk Magufuli.

Ingawa hakuzianisha nyumba zilizotakiwa kubomolewa katika barabara hiyo, sehemu kubwa ina nyumba za thamani kubwa hasa ghorofa jambo ambalo linatarajiwa kuwaweka katika wakati mgumu wamiliki wake.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroads, Patrick Mfugale alisema: “Nyumba zitakazobomolewa siyo nyingi. Ni zile zilizojengwa ndani ya mita 30 ya hifadhi ya barabara. Kinachotuchelewesha ni kuondolewa kwa nyaya za umeme pamoja na mfumo mkubwa wa maji ili tuweze kuanza ujenzi.”

Waziri Magufuli alisema fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo zipo na hata za kuwalipa wamiliki wa nyumba hizo zipo, hivyo akasisitiza kuwa kazi ya kuzibomoa inapaswa kuanza mara moja.

“Wanaostahili kulipwa fidia walipwe na ambao hawastahili waondoke. Suala la kwamba mko kwenye mchakato life na libaki kuwa neno la wanasiasa tu,” alisema Magufuli.

Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2012/13, imeonyesha kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3, ujenzi wake unafadhiliwa na Serikali ya Japan.

Kuhusu ujenzi wa barabara za juu, Waziri Magufuli alisema ni jambo linalowezekana na halihitaji kufanyiwa mchakato wowote.

Alisema ni muhimu bodi hiyo mpya ikasimamia ujenzi wa barabara hizo ili kupunguza msongamano wa magari Dar es Salaam.

“Tengenezeni ‘flyovers’ nyingi nyingi, ni kazi ndogo lakini inashangaza kwa nini Tanroads inakuwa na kigugumizi,” alisema Magufuli na kuongeza:

“Wahandisi wa Tanroads fanyeni hivyo, mbona kule Kenya mambo yamefanyika bila tatizo? Acheni kigugumizi na siasa mfanye kazi.”

Magari ya Serikali
Waziri Magufuli pia alizungumzia mchakato wa kukamata magari ya Serikali yanayotumika vibaya na kuzitaja Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) kuwa vinara wa tatizo hilo.

Dk Magufuli alisema tangu kuanza kwa operesheni hiyo, magari 974 yalikamatwa baada ya watumishi wake kuyageuza kuwa ya kiraia kwa kubandika namba binafsi.

Alisema pamoja na kukamata kiasi hicho, bado kuna magari 746 ya Serikali ambayo hayajasajiliwa na mengi yako Wizara ya Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia pamoja na Tamisemi.

“Hawa ndiyo wanaoongoza kwa magari yao kutokusajiliwa kiserikali. Tutaendelea na mpango huo hadi magari yote yatakapokamatwa na kusajiliwa.”

Awali, operesheni hiyo ilionekana kusuasua tangu waziri huyo alipotangaza kuanza kwake kwa washirikisha polisi.

Hivi karibuni, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, John Ndunguru alivieleza vyombo vya habari kwamba Serikali iliweka utaratibu unaozuia matumizi ya namba za kiraia kwenye magari yake isipokuwa kwa kibali maalumu.

Alisema hali ya kuzuia huko kuliibuka baada ya kubainika kwamba kupitia namba hizo, magari ya umma yamekuwa yakitumika vibaya na baadhi kupotea.

CHANZO: Mwananchi | Disemba 18, 2012
 
mmh pale ndo kwanza nilivyokuwa nasepa walikuwa wanajenga majengo mapya kama GEPF, Spanish Tiles etc na majengo kama ya ABLA yapo tayari..sasa watabomoa hadi hayo?
 
Kutengeneza barabara si kubaya ila kuwabomlea watu nyumba na vitega uchumi vyao na hali uliwapa building permit kujenga sijui kam ainaleta maana kwani mipango miji hawajui watafanya nini miaka kumi ijayo hadi waache watu wajenge ili waje wawabomolee badae. Hili jambo linakera sana.

Watu hata kama watalipwa fidia ambazo nazo hutolewa kwa gumashi wanapotezewa muda mwingi sana kuhama na kwenda kujenga maeneo mengine na kutumia nguvu nyingi sana.

Kwa hili serikali iwe inajipanga vizuri. Sio kama vile mtu anakurupuka kesho tunataka kujenga barabara fulani tutabomoa chochote kitakachokuwa katika eneo hili niniiiiii?
 
jengo la tanesco ubungo limemshinda kulibomoa..magufuli mkurupukaji
 
inashanga kuondoshe watu vitega uchumi vyao ikiwa barabara zinaendelea kujengwa upana ule ule.

Tushuhudie huu ujenzi wa barabara ya Magomeni - Ubungo, itakuwa tofauti ndogo sana na ya zamani
 
Sasa Abla ikibomolewa sijui M/kiti atalala wapi?au ule mjengo wa Mbezi tayari?
 
Kutengeneza barabara si kubaya ila kuwabomlea watu nyumba na vitega uchumi vyao na hali uliwapa building permit kujenga sijui kam ainaleta maana kwani mipango miji hawajui watafanya nini miaka kumi ijayo hadi waache watu wajenge ili waje wawabomolee badae. Hili jambo linakera sana.
ndugu inaelekea wewe ndiye hujui. Unadhani mtu anayeangalia usawa wa tumbo lake na mdomo anaweza kuona hata kitu gani kitatokea siku mbili zijazo achana na hiyo miaka 10 unayoisema!???
Ndio maana unakuta watu asubuhi mpaka jioni mpaka asubuhi watu wanahangaika na kufikiri ni jinsi gani waibe pesa za umma lakini ukiwauliza kwa umakini hawajui hata hizo pesa watazifanyia nini mbali na kuongeza magari na majumba wasimoishi!

 
jembe magufuli bomoa tu sheria ni msumeno! Walijua wanajenga barabarani
 
Umeona eeh! Ubungo - Kimara ina miezi sasa toka ibomolewe, ila wanajenga Magomeni. Kwa nini wasibomoe na kujenga kabla ya kwenda kubomoa sehemu nyingine wakati wanajua plan ya kupajenga ni baada ya miezi sita?
maghuguli hana ubavu wa kuwakemea strabag! wako likizo ujerumani wakila krismasi, barabra imefungwa, hata njia a kuchepuka, diversion ambazo ni jukumu la mkandarasi kuzikarabati na mabonde matupu!
 
wewe na akili yako unaona barabara ni nyembamba then unakuja unajenga kigorofa hapo. Unategemea nini?
 
ndugu inaelekea wewe ndiye hujui. Unadhani mtu anayeangalia usawa wa tumbo lake na mdomo anaweza kuona hata kitu gani kitatokea siku mbili zijazo achana na hiyo miaka 10 unayoisema!???
Ndio maana unakuta watu asubuhi mpaka jioni mpaka asubuhi watu wanahangaika na kufikiri ni jinsi gani waibe pesa za umma lakini ukiwauliza kwa umakini hawajui hata hizo pesa watazifanyia nini mbali na kuongeza magari na majumba wasimoishi!


si magari na majumbo wasimoishi tu kaka kibaya zaidi wanaenda kuhonga vimada unakuta mtu kamjengea demu nyumba ya kifahari kamnunulia na gari nzuri kisa apate ngono tu hii ni akili kweli au matope afadhali pesa zenyewe zingekuwa zake ambazo amechuma kwa jasho lake lakini pesa kaiba za walala hoi inauma sana
 
tanzania tunaishi kwa kuviziana. yani unasubiri afanye amalize umkomeshe.
 
Back
Top Bottom