Bomoa bomoa yaacha kilio Kibamba

Bomoa bomoa yaacha kilio Kibamba

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
ZOEZI la kubomoa nyumba zaidi ya 100 za mtaa ya Mbezi Centre kata ya Mbezi na mtaa wa Msigani kata ya Msigani, Jimbo la Kibamba katika wilaya ya Ubungo limeacha vilio kwa mamia ya wananchi, wakiwemo wamiliki wa nyumba, wapangaji na wafanyabiashara.

Ubomoaji huo uliosimamiwa na Jeshi la Polisi umefanyika juzi na jana huku ukidaiwa kukiuka amri ya mahakama iliyoweka zuio la ubomoaji kupitia kesi Na. 716 ya mwaka huu, iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.

Katika zoezi lililofanyika jana baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walifanikiwa kuokoa mali zao huku wengine wakiambulia patupu baada ya kushitukia tayari gari ya ubomoaji maarufu kama ‘kijiko’ imefika katika makazi yao na hivyo kulazimika kuondoka ili kunusuru uhai wao.

Kabla ya bomoa bomoa hiyo, tarehe 18 Agosti mwaka huu Wakala wa Barabara (TANROADS) walitoa notisi ya kuwataka wakazi wa maeneo hayo kubomoa kuta/majengo yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi wa barabara ya Goba-Mbezi.

Notisi hiyo iliyosainiwa na Ndyamukama, J. ambaye ni meneja wa TANROADS Jijini Dar es Salaam ilisema, “Nyumba yako/Ukuta/shimo la maji taka/uzio/fremu za biashara vimo ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kinyume cha Sheria za Barabara ikiwemo The Highway Ordinance Cap.167 kifungu Na. 52 ya mwaka 1932, The Highway Act ya mwaka 1967, Ilani ya serikali Na. 161 (G.N), Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 na kanuni za hifadhi za barabara za mwaka 2009 kifungu (2) (d) hivyo unaombwa kubomoa.

Lakini Abasi Makuwani, katibu wa wananchi 73 waliofungua kesi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupinga notisi hiyo anasema kesi hiyo Na. 716 inaendelea kusikilizwa tena tarehe 7 Desemba, mwaka huu na hivyo wanashangaa kuona ubomoaji huo ukifanyika.

“Ni mgogoro wa muda mrefu kwani mwaka 2004 tulipewa notisi ya kubomoa nyumba na TANROADS lakini tarehe 4 Desemba, 2005 tukafungua kesi Na. 80/2005 kati ya Proches E. Tarimo na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo mahakama iliamua kuwa wananchi ndiyo wamiliki halali wa eneo hilo.

“Serikali iliambiwa kama inalihitaji eneo hilo kwa matumizi yoyote basi ifuate taratibu za kulipa fidia, baadaye serikali ilikata rufaa kwa kuomba muda wa nyongeza (extension of Time). Maombi yao yalikubaliwa lakini hatimaye yalifutwa kwa kukosa nia ya kuyaendesha (dismissed for want of prosecution),” amesema Makuwani.

“Nyumba yangu iliyobomolewa ina thamani ya Sh. 100 milioni. Mpaka sasa sina pa kwenda, nipo nalala na kushinda juani na familia yangu ya watu nane,” amesema Juma Mkombozi, alyekuwa mkazi wa mtaa wa Msigani.

Mkombozi anasema wakazi wa eneo hilo si wavamizi kwani seikali yenyewe ndiyo iliwahamishia hapo, mwaka 1971 kupitia mpango wa vijiji vya ujamaa na kwamba mwaka 1976 E.F.B Sengati, aliyekuwa msaidizi Msajili wa Vijiji alitoa hati Na. DSM.VC.8 ya kuthibitisha hadhi ya halmashauri ya kijiji cha Mbezi.

Humphrey Sambo, Diwani wa kata ya Mbezi amesema, “Serikali ndiyo wasimamizi wa sheria lakini wanakaidi amri ya mahakama. Jana (juzi), Humphrey Polepole, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo alisitisha zoezi la ubomoaji lakini leo (jana) limeendekea. Kuna kitu kimejificha.

Sambo amesema amelazimika kuwanunulia chakula baadhi ya wakazi waliombomolewa nyumba zao baada ya kushinda bila chakula.

Hata hivyo Polepole ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo alipofuatwa ofisini kwake hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, hali inayozua sintofahamu zaidi.

Jimbo la Kibamba linaongozwa na Mbunge John Mnyika wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku madiwani wa kata zote sita za jimbo hilo wakiwa wanatokana na chama hicho pia.
 
Mkuu kwanza poleni sana na yaliowakuta. Kama mna vielelezo vya kihalali, basi enndeleeni kupambana na serikali kisheria kupitia mahakama. Pili, sijaelewa unamaana gani kwa hili...uhusiano kati ya Mhe Mnyika, Madiwani na bomoa bomoa inayofanywa na serikali.
 
WAKUMBUKE WALIMPIGIA NANI KURA 2015 ?? NA ALIYEPATA NI NANI? BAAS
 
Tuache siasa Jamani Ili eneo liwe na hadhi Barabara ni Muhimu!! Sasa watu wamejenga hadi kwenye ukingo wa barabara hii ni hatari? Tufike Mahali tuseme sasa hii basi!! Na watu waheshimu sheria bila kusuguana na mamlaka husika!
 
Mkuu kwanza poleni sana na yaliowakuta. Kama mna vielelezo vya kihalali, basi enndeleeni kupambana na serikali kisheria kupitia mahakama. Pili, sijaelewa unamaana gani kwa hili...uhusiano kati ya Mhe Mnyika, Madiwani na bomoa bomoa inayofanywa na serikali.
Anajaribu kuweka siasa kwenye masuala ya kisheria. Anajaribu kuigombanisha serikali na mbunge.

Utadhani hiyo sehemu ndio pekee ambayo imebidi nyumba zibomolewe kwa sababu ya kujenga ndani ya hifadhi ya barabara.
 
Nionavyo mimi kama ubomoaji huo umefanyika kwa kufuata matakwa ya kisheria basi sawa. Endapo kweli kesi ipo mahakamani, na kama mtoa hoja alivyoidhinisha kwamba mahakama ilishawapa haki hao mabwana, basi kuna shida ktk utekelezaji wa hilo.

All in all, tuwaombee wote waliokumbwa na maswahibu hayo. Mungu awape nguvu na njia mbadala za kukabiliana na hali ngumu inayowakabili
 
Tuache siasa Jamani Ili eneo liwe na hadhi Barabara ni Muhimu!! Sasa watu wamejenga hadi kwenye ukingo wa barabara hii ni hatari? Tufike Mahali tuseme sasa hii basi!! Na watu waheshimu sheria bila kusuguana na mamlaka husika!
Hoja yao iliyoko mahakamani ni kwamba barabara/serikali imewafuata hao wananchi wakiwa wameishajenga nyumba zao. Sasa hapa nani wa kuambiwa afuate sheria; serikali au wananchi? Kama ni kufuata sheria serikali ilitakiwa iheshimu mahakama!
 
serikali imewahamisha 1971 halafu leo 2016 wanasema wavamizi teh teh teh teh
 
Kujenga pembezoni mwa barabara ni kujitakia umasikini mwenyewe!
Sheria za barabara ziko wazi ila sisi wananchi siku zote tumekuwa wakaidi! Hatupendi kutii sheria bila shuruti!

Sasa tuhame wenyewe kabla ya kupata hasara
 
Hakuna jema litafanyika ndani ya nchi hii. Kariakoo Machinga wameziba barabara na njia za watembea kwa miguu, watu wanalalama, wameanza kuondoshwa nongwa.Eti Serikali itafute pa kuwapeleka, yeboh!Wewe unafanya shughuli zako eneo lolote hata ambalo ni wazi hapatakiwi kufanya shughuli, uondoshwe alafu udai fidia au pa
kupelekwa?

Huu ujinga hauitakiwi kuendekezwa tena.Watu makaidi ndo serikali iwajali zaidi ya wale ambao ni humble? Mtu ujenge kwenye hifadhi ya brbr kisha udai fidia kwa kuondoshwa kisa huna pa kwenda.Wapo watu wanalala mitaroni na kwenye mabaraza lakini wanatii taratibu, mbona hamdai serikali iwaangalie hawa?
 
Halafu eti bado kuna mbururaz zinaendelea kuiombea hii kitu? Labda kwa shetani na siyo kwa Mungu ninayemwamini!!
 
Mkuu kwanza poleni sana na yaliowakuta. Kama mna vielelezo vya kihalali, basi enndeleeni kupambana na serikali kisheria kupitia mahakama. Pili, sijaelewa unamaana gani kwa hili...uhusiano kati ya Mhe Mnyika, Madiwani na bomoa bomoa inayofanywa na serikali.
Thinking capacity. .ya chadema is real atomic
 
Tuache siasa Jamani Ili eneo liwe na hadhi Barabara ni Muhimu!! Sasa watu wamejenga hadi kwenye ukingo wa barabara hii ni hatari? Tufike Mahali tuseme sasa hii basi!! Na watu waheshimu sheria bila kusuguana na mamlaka husika!
 
Jimbo la wapinzan hilo,ukumbuke Magu hawapend kbsa!!!
 
Back
Top Bottom