Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
Ubomoaji wa myumba za ufukweni ni danganya toto maana tayari watu wameshalipwa stahili zao, kinachofanyika ni danganya toto kama ni kweli mbona wamiliki hawaja onekana kwenye nyumba zao? wameonekana wapangaji na vibaka waliokuwa wanajichukulia mabati.
zamu ya matajiri imewadia tumelalamika sana kuwa ni masikini tu wanaguswa sasa maghorofa yameangushwa na tingatinga
Ni wazi kuwa ubomoaji wa majumba ya kifahari kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi,Dar es Salaam inavuta hisia za wengi.Wengine tunafuatilia tukishangaa namna wahuni wachache wa nchi hii walivyojilimbikizia mali na kujenga majumba ya thamani kubwa. Serikali inafanya kusudi kuvuta 'attention' ya watu ili wasahau mambo muhimu kama ya migomo na maisha bora.Serikali inajipalilia moto zaidi.Inaongeza chuki kwa wananchi.Kwanini isifanye sirini?
Tunafaidikaje kuangalia matingatinga yao? Ukweli ni kwamba,kila anayevunjiwa nyumba yake ameshalipwa. Serikali pale inafanya maigizo.Fahamuni kuwa Serikali iko kwenye harakati za kuwaaminisha watanzania kuwa yenyewe na viongozi wake si dhaifu.
Ubomoaji wa myumba za ufukweni ni danganya toto maana tayari watu wameshalipwa stahili zao, kinachofanyika ni danganya toto kama ni kweli mbona wamiliki hawaja onekana kwenye nyumba zao? wameonekana wapangaji na vibaka waliokuwa wanajichukulia mabati.
kuna ule mjengo mweupe wa kifahari zaidi, mbona sikuona ukibomolewa? Itv walionyesha yale mengine tu. Umebolewa kweli?
Tena hii open space ya ya mbele ya double view mbona kashindwa kuibomoa najamaa sasa wanaendelea na ujenzi!!hao matajiri wameshalipwa fidia ya bilions, ndo maana wako kimyaa, hawalalamiki. Tibaijuka akitaka kufanya kweli avunje majumba yaliyojengwa kwenye open space huku sinza na eneo lote la kinondoni. viwanja vinavyopimwa visitolewe kwa kupendelea yaani kwa wakubwa kama tunavyo witness viwanja vya gezaulole, mabwepande nk. majina ya wanaopewa viwanja na ya vigogo; wabunge, maRCs, mawaziri na watoto wao...
Mama Tiba kaanza kuwatiba wagonjwa sugu...... thanks mama.
Hakika ni ngumu kumridhisha binadamu kama ilivyo vigumu ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
Hata kama unaichukia serikali inayoitwa dhaifu lakini ikifanya jambo jema tunahitaji kuinga mkono.
Mmmmh, lile jengo la TANESCO , Ubungo watalibomoa lini?
Inaelekea huyu hajakubaliana na malipo waliyomlipa.nyumba zimevunjwa zikiwa na vitu ndani baada ya kukaidi kuhama... mama Dr Gerudi Lwakatare kakimbilia mahakamani kupinga sio jambo dogo kama unavyodhani kwamba serikali imewalipa kisirisiri. Huyu ni mbunge lakini kaguswa na bomoa bomoa ya mama Tiba.
Hapo siungi mkono hoja 1000%! Hapo red, una ushahidi japo kidogo, zaidi ya hisia zako? Serikali haipaswi kumlipa yeyote aliyejenga pasipotakiwa, kinyume chake, mwenye nyumba alitakiwa avunje mwenyewe au kulipia gharama za uvunjaji.Tunafaidikaje kuangalia matingatinga yao? Ukweli ni kwamba,kila anayevunjiwa nyumba yake ameshalipwa. Serikali pale inafanya maigizo.Fahamuni kuwa Serikali iko kwenye harakati za kuwaaminisha watanzania kuwa yenyewe na viongozi wake si dhaifu.
@MAMA POROJO kwanza binafsi ninaiunga mkono serikali kwa hatua zake hizo, vyenginevyo nchi itakuwa haitawaliki kwani kila mtu atakuwa anafanya atakavyo. Hongera serikali kwa hilo. Lakini sitaacha kukiri kuwa SERIKALI NI DHAIFU.Kasema bungeni juzi kwamba hata kama hatalibomoa yeye bado litakuja kubomolewa bila fidia kwa sababu liko kwenye hifadhi ya barabara.
Mama Tiba kaanza kuwatiba wagonjwa sugu...... thanks mama.
nyumba zimevunjwa zikiwa na vitu ndani baada ya kukaidi kuhama... mama Dr Gerudi Lwakatare kakimbilia mahakamani kupinga sio jambo dogo kama unavyodhani kwamba serikali imewalipa kisirisiri. Huyu ni mbunge lakini kaguswa na bomoa bomoa ya mama Tiba.