Mahekalu ya vigogo Dar yabomolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahekalu ya vigogo Dar yabomolewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 11, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,482
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mahekalu ya vigogo Dar yabomolewa [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 10 July 2012 20:21 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Mwananchi

  NI NYUMBA, KUTA ZA MABILIONI ZILIZOJENGWA UFUKWENI, MMOJA AKIMBILIA KORTINI KUZUIA JUMBA LAKE LA SH1.5 BILIONI
  Geofrey Nyang’oro


  SERIKALI jana ilikunjua makucha yake kwa vigogo waliojenga nyumba za kifahari kando ya Mito ya Mbezi Beach, Mndumbwe na eneo la Hifadhi ya Mikoko, Dar es Salaam baada ya kuzibomoa katika operesheni iliyosimamiwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi.

  Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais la mwaka 2004 ambalo lilitaja maeneo tengefu ambayo yalipaswa kuhifadhiwa zikiwamo fukwe za bahari ambazo zina mikoko ambayo ni mazalia ya samaki baharini. Licha ya tamko hilo na sheria mbalimbali, bado maeneo ya fukwe za bahari yamekuwa yakivamiwa.

  Katika kusimamia sheria na tamko hilo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kitengo cha Hifadhi ya Misitu, Baraza la Taifa la Kuhifadhi Mazingira (NEMC) na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ziliamua kuratibu bomoabomoa hiyo ya nyumba za kifahari zilizojengwa maeneo tengefu ya bahari.

  Bomoabomoa hiyo ambayo iliendeshwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wa FFU chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela na kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa NEMC, Dk Robert Ntakamulenga, jumla ya nyumba 27 kati ya hizo 15 zikiwa zimekamilika ujenzi, nane uzio (fence) na nyingine katika hatua za awali za ujenzi, zilibomolewa.

  Kazi ya kubomoa nyumba hizo iliyofanywa na kampuni ya Majembe Auction Mart, ilianza huku wakazi wa nyumba hizo wakiwekwa chini ya ulinzi mkali wa FFU na polisi wengine waliokuwa wamesheheni mabomu ya machozi, bunduki na gari la kumwaga maji ya kuwasha.

  Bomoabomoa hiyo ilianzia katika eneo la Hifadhi ya Mikoko, Mbezi Beach mnamo saa 2:00 asubuhi na watu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo walilazimika kutoa vitu vyao nje huku kububujikwa machozi.

  Mmoja wa wakazi wa eneo hilo na Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Christian, George Makala alisema kitendo hicho kinasikitisha kwa kuwa muda uliotolewa kwao ni mdogo na wasingeweza kujiandaa kuhama.

  Akizungumzia tukio hilo muda mfupi baada ya kubomolewa nyumba yake na kanisa hilo, Mchungaji huyo alisema kitendo hicho hakikufuata taratibu na kimesababisha hasara ya mali nyingi kwa wakazi wa eneo hilo akisema kama wangeachwa wahame zingeokolewa.

  “Ninasikitika sana kwani kitendo hiki hakikufuata taratibu, alikuja Waziri wa Nyumba, Ardhi na Makazi Profesa Anna Tibaijuka, Mbunge wetu, Halima Mdee na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda wakatuambia eneo hilo siyo la hifadhi, bali ni hatarishi, sisi tuliwaambia tuna uwezo wa kukabiliana nalo ndipo waziri aliposema atatoa tamko,” alisema Mchungaji Makala na kuongeza:

  “Tukiwa tunasubiri tamko kutoka kwa waziri na vibali tunavyo, tumeshangaa (juzi) Jumapili tunaamka na kukutana alama za X. Hatukujua nani ameweka, leo (jana) ghafla tunashangaa tingatinga zimekuja na kubomoa.”

  Alisema walichofanyiwa siyo haki kwa sababu hawakupewa muda wa kujiandaa kutafuta mahali pa kuhamia lakini pia wangebomoa nyumba zao kuokoa mali zao.
  “Kwa sasa tutawasiliana na mwanasheria wetu kuona kama kuna uwezekano wa kuchukua hatua ili twende mahakamani, lakini hilo litategemea nini mwanasheria atatushauri,” alisema Makala.

  Wananchi washangilia
  Wakati Mchungaji Makala akielekeza kilio chake kwa waratibu wa shughuli hiyo, baadhi ya watu waliofika kushuhudia tukio hilo waliisifu Serikali wakisema sheria sasa imeanza kufanya kazi.
  Mmoja wa wakazi hao, Samuel Laizer alisema kilichofanywa sasa na Serikali kinaonyesha kuwa sasa inafanya kazi na hakutakuwa na mtu atakayekuwa juu ya sheria.
  “Tukio hilo limenifurahisha sana, tumezoea kuona Serikali ikituonea sisi maskini, lakini kitendo cha kubomoa nyumba hata za vigogo waliovunja sheria, sasa tunaamini watu wote tutakuwa sawa,” alisema Laiser.

  Katika eneo la Mto Mbezi Beach, kikosi hicho cha ubomoaji kilivunja kuta kadhaa zilizokuwa zimezungushwa katika viwanja saba vilivyokuwa karibu na mto huo pamoja na Mto Mndumbe inayomwaga maji katika Bahari ya Hindi.

  Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema baadhi watu wanaomiliki viwanja hivyo waliendelea kujenga majumba ya kifahari licha ya zuio hilo lilitolewa zaidi ya mara tatu.

  Heche pia alisema bomoabomoa hiyo ilikuwa iikumbe moja ya nyumba ya kifahari katika Mto Mbezi lakini mmiliki wake ameweka pingamizi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi. Kwa mujibu wa watu waliokuwa katika eneo hilo, nyumba hiyo inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh1.5 bilioni.

  Akizungumzia shughuli hiyo ya jana, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi Rasilimali na Wakala wa Huduma za Misitu, Zawadi Mbwambo alisema kazi hiyo imechelewa kutokana na kuhusisha idara, wizara na taasisi tofauti katika utendaji wake.

  Alisema kazi hiyo itakuwa endelevu na itawahusu watu wote waliojenga katika maeneo ya fukwe za bahari na kusisitiza kuwa umbali unaoruhusiwa kujenga nyumba kutoka eneo la bahari ni meta 60.

  Kwa upande wake, Dk Ntakamulenga alisema kazi hiyo ya kubomoa nyumba katika maeneo ya hifadhi za taifa, fukwe za bahari na kando ya mito ni endelevu na akatoa wito kwa watu wote waliojenga katika maeneo hayo kuchukuka tahadhari mapema kuondoa usumbufu.
  “Tumechelewa kuchukua hatua kutokana na zoezi hili kushirikisha mamlaka zaidi ya mmoja, tulikutana kujadili na kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu ili utekelezaji wake usiingilie mamlaka nyingine,” alisema Dk Ntakamulenga.

  Alisema kazi hiyo pindi itakapomalizika katika jiji la Dar es Salaam ambako kuna viwanja zaidi ya 100, vinavyopaswa kurudishwa katika mamlaka husika, itahamia mikoani na itawahusu pia watu wote waliojenga nyumba zao kwenye hifadhi za taifa, kando ya mito na kwenye fukwe za bahari kitendo kinachosababisha uharibifu wa mazingira.

  Polisi Kinondoni yatoa onyo
  Kamanda Kenyela aliwataka watu wote waliojenga nyumba zao katika maeneo yanayokatazwa na Serikali, kuzibomoa wenyewe ili kukwepa mkono wa sheria.

  “Tukio la leo ni kwamba tumewasha taa, sasa watu wote waliojenga nyumba zao kinyume na sheria katika jiji la Dar es Salaam na hata wenye migogoro ya ardhi ambao Mahakama ilishatoa hukumu ni vyema wakabomoa wenyewe, watii sheria pasipo shuruti,” alisema.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Na nyumba ya Waziri Mwinyi inasemekana kuwa ipo ndani ya eneo pale Mbezi Beach.

  Je nayo imebomolewa??????


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,482
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Hapana.........ile alijimegea kutoka kiwanja cha Tanganyika Packers
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  BAK, walalahoi hawajengi beach, leave alone kujenga mahekalu.

  Wanagawana viwanja, wanagombana wenyewe kwa wenyewe, wananyang'anyana, wanavunjiana na mwishoni wanalipana fidia at the expense of the taxpayer.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ile hotel ya golden tulip kule masaki inakuaje? Maana sehemu yote ya ufukweni kule kuna majengo mawili tu hiyo hotel na ile ya polisi. Wataivunja lini na hiyo?
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,954
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Ngoja nisogee site naweza kupata masalio kwa bei nafuu nami nijidai huku kwangu Tandale kwa Tumbo
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mama Mchungahji Mheshimiwa Lwakatare amejenga jumba kwenye mdomo wa mto Ndumbwi na ameuzuia mto kwa kuweka mawe makubwa sana; je hilo jumbalimepona? Jumba lenyewe limejengwa express ndani ya miezi miwili na hekalu limekwisha!!
   
 8. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Tutaona mengi mwaka huu!!!
   
 9. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NYumba ya MH. MCH. Getrude Lwakatare nayo imeachwa hali walijenga nyuma yake wamebomolewa hii nchi kwa ubaguzi na ufisadi inaongoza.


   
 10. M

  MUNYAMAKWA Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa maji mmesha yavulia nguo lazima muyaoge. HAKUNA kurudi nyuma ili wanchi warudishe imani kwa serikali yao
   
 11. t

  testa JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mama mchunguja nasikia kakimbilia mahakamani kusimamisha zoezi hapo ndo atakapojua mh mbunge wetu wa Kawe ana msimamo usioyumba,lazima abomolewe yy ni nani kwenye nchi hii
   
 12. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo tutakapojua kuwa Mh. Anna Tibaijuka ni moto wa Petrol au wa Kifuu.

  Sheria haitakiwi kuchagua cheo au umaarufu wa mtu. Hata ikiwa ni nyumba ya J. Kikwete kama ipo sehemu isiyoruhusiwa yabidi sheria ifuate mkondo wake na kame haiwezi kupindishwa.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...