Kwani hawajalipwa? au hao ni wapangaji walikuwa wanasubiri kodi iishe?
Lakini hao si ndiyo wapenzi wa ccm? Kwa nini Kikwete asiagize wajengewe nyumba kama wale wa Bwagamoyo wanaopisha ujenzi wa bandari/bomba la gesi?
Kwani hawa watu hawakulipwa? Nadhani walilipwa na baada ya hapo walipashwa kuanza kuondoka. Tatizo ni kwamba baada ya kutoa malipo, serikali ukaa muda mrefu bila kuanza ujenzi hivyo kuwafanya waliolipwa au kuamua kuwauzia watu hizo nyumba na wao kuondoka au kujisahau kwamba kuna siku watatakiwa kuondoka. Wanaonunua wanakuwa hawaelewi kinachoendelea kwamba muuzaji aliisha lipwa ili ahame. Utakuta wengi wa waliovunjiwa sio wenye majumba original. Hii ilitokea hata kwa wale waliohamishwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege kule Kipawa, watu waliliwa kweli kweli.
Tiba
Kwahiyo hapo wapo kinyume na sheria
hizi nchi zetu za dunia ya tatu bila kuwa kadikteta na ukatili kidogo mambo hayaendi,utakuta wamelipwa siku nyingi lakini kuhama hawahami hadi waje kubomoa ndio watu wataanza kulaumu kwa nini wanabomolewa...mfano yule mzee wa greenacres pale victoria....hawawezi kuja kubomoa tu bila taarifa au kuwalipa
Sheria inasema tii mamlaka na utawala bila shuruti.
Unacheza na maisha eeeeh?hivi umelipwa milion 20 alafu unasikia wenzio wanalipwa mil 300 utaona raha.
Unaweza hata ukafa....wameongezewa pesa mwaka huu mara laki2,wenye nyumba nzur mpaka mil1.Hali za wananchi ni mbaya huko,nawaonea huruma sana.
haswaaa! Toka 2009 walitakiwa wahame na walishapewa stahili zao sasa hapo nadhani walijisahau ndo yamewakuta haya. Si kitu kizuri ila hawajafanyiwa uvamizi ni kwamba ilikuwa iko waz na wangehama mapema dhahama hii isingewakuta.
kwanini ulipokea??
Thubutuuuuu hivyo viwanja vyenyewe walivyoandaliwa kimbiji wanatakiwa walipe mil 6......
Mimi si mkazi wa huko ingawa najua historia ya hilo eneo vizur sana tu.
Hizo pesa watu walipokea tu wafanyeje lakin w pesa zilipigwa sana watendaj wa serikal wa mtaa.
Wazir walimrekodi akisema kuwa tathimin iliyofanyika kipind hicho tunaifuta na kuanza upya,watu walifurahia sana lakin kabla yakufika kwa wananchi akaekwa mtu kati nakutoa tamko lingine kuwa hataongeza pesa zaid wale waliokataa kupokea pesa kipind kile ndo watalipwa pesa nzur hizo mil300.
Wanapozungumza wakazi hao wanasema ya kuwa pesa walizolipwa zilikuwa chini ya kiwango. Kuna mama mmoja alisikika akisema alilipwa shilingi milioni 27, na hajapewa kiwanja. Maana yake ni kwamba katika hiyo milioni 27 anunue kiwanja na ajenge nyumba ya kuishi yeye na familia yake. Halafu wiki iliyopita wakapewa siku saba wawe wamehama, wakati huenda hata hiyo milioni 27 wameshaitumia hata kama si yote kwa matumizi mengine. Kweli kama sio kuwapa watu ufukara wa kudumu ni nini?
Ama kweli maisha bora kwa kila mtanzania tunayaona. Naona ccm imeamua kama alivyosema Pinda, Liwalo na Liwe!
Mwenye nacho ataongezewa na yule asiye nacho hata kile kidogo atanyang'anywa.Kwani sheria ina semaje
[/B]
Basi acha wakome maana wakazi wa DSM ndiyo wanajifanya wana mahaba na CCM!!!!!!!!!!!!!!