Mvua kubwa iliyonyesha hapa Jijini Mwanza imesababisha madhara makubwa ya mali na kifo kimoja cha mtoto wa shule na inasemekana watu wengi zaidi wamepoteza maisha. Mto Mirongo kwa Miongo kadhaa umeleta maafa kwa wakazi wanaoishi kingo za mto Mirongo. Tunaiomba na kuitaka serikali kuvunja nyumba zinazozuia mto huu ili kuokoa maisha ya watu na mali.