Bomoa bomoa D'salaam kuhamia kwa vigogo. Madudu ya Manispaa ya kinondoni hadharani

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
1422436_1017505018313956_6555258964911926677_n.jpg
 
Acha huu mtindo wa kuleta vichwa vya habari kutoka gazetini. Soma hiyo habari yote kisha uiweke hapa!
 
Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani tunaambiwa ameanza kwa kasi kubwa ya kutumbua majipu.
Kweli amesimamisha kazi vigogo katika idara za serikali kama vile TRA, Takukuru, Rahaco na kwingineko.
Kuunda baraza la mawaziri dogo na makatibu lukuki wa wizara hayo sio mada ya leo.
Leo nataka yuangalie hii bomoabomoa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kama mabondeni, maeneo oevu na ya wazi.
Kwanini Rais Magufuli asingewapa muda wa angalau miezi 6 watu hao na kuwatafutia sehemu mbadala ya kuhamia?
Tunaambiwa kuna nyumba 8000 Dar peke yake zitabomolewa. Kwani kuna haraka gani ya kubomoa nyumba kiasi hiki?
Naomba nieleweke, siungi mkono uvamizi wa maeneo yaliyokatazwa, lakini sidhani kama kulikuwa na haja ya kufanya haraka kiasi hiki.
Angalau basi wqngeangaliwa wale masikini waliojenga mabondeni wakapewa viwanja vingine au kukopeshwa nyumba maeneo mengine. Lakini sio kuwabpmolea nyumba halafu wasijue pa kwenda.
Au hiki ndio kipaumbele cha kwanza cha Magufuli baada ya kuingia madarakani?
 
Namuunga mkono magufuli, waache waisome namba, nchi lazime itawaliwe kwa mujibu wa sheria
 
Mliwahi kuinanga serikali ya ccm kushindwa kuzuia kipindupindu Dar.

watu wamejenga kwenye mikondo ya maji unataka waachwe?
 
Usifikiri wamependa kujenga mabondeni, ni umasikini tu. Mbona kina Magufuli wameuziana nyumba za kifahari za Oysterbay na Masaki?
Huu sio wakati wa malalamiko, huu ni wakati wa kutekeleza ilani ya chama tawala ambacho hata wao walikipigia kura, kwa hiyo wakati wa malalamiko umepita wasubiri 2020
 
Tatizo ni city master plan ya 2012-2032 naona hii haina mashiko

mji na rdhi siyo DSM tu, mji huu uhamishwe na serikali yote, iende kibaha, chalinze, kisarawe au dodoma; mji ushaharibika huu

na ni makosa ya serikali yenyewe na hasa hawa watendaji wa chini

Namuunga mkono meta maada, kuwa kama kuvunjiwa ni watu wa mabondeni, wavamizi wa open space na other public areas ni sawa

ila kama ni kupisha hiyo masterplan, I am afraid wako wrong
 
Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani tunaambiwa ameanza kwa kasi kubwa ya kutumbua majipu.
Kweli amesimamisha kazi vigogo katika idara za serikali kama vile TRA, Takukuru, Rahaco na kwingineko.
Kuunda baraza la mawaziri dogo na makatibu lukuki wa wizara hayo sio mada ya leo.
Leo nataka yuangalie hii bomoabomoa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kama mabondeni, maeneo oevu na ya wazi.
Kwanini Rais Magufuli asingewapa muda wa angalau miezi 6 watu hao na kuwatafutia sehemu mbadala ya kuhamia?
Tunaambiwa kuna nyumba 8000 Dar peke yake zitabomolewa. Kwani kuna haraka gani ya kubomoa nyumba kiasi hiki?
Naomba nieleweke, siungi mkono uvamizi wa maeneo yaliyokatazwa, lakini sidhani kama kulikuwa na haja ya kufanya haraka kiasi hiki.
Angalau basi wqngeangaliwa wale masikini waliojenga mabondeni wakapewa viwanja vingine au kukopeshwa nyumba maeneo mengine. Lakini sio kuwabpmolea nyumba halafu wasijue pa kwenda.
Au hiki ndio kipaumbele cha kwanza cha Magufuli baada ya kuingia madarakani?
Wakipata maafa ya mafuriko wanalalamika serikali tusaidie kujenga wamejenga wenyewe kwani maeneo Tz ya kujenga yaliisha? Wabomolewe tu maana hakuna namna
 
Hizi mada zimejaa humu. Nyie Ndo wakwanza kulalamika maafa yakitokea, uvamizi wa maeneno yasiyo halali ni kosa. Hawa watu hawana hata hati za nyumba. Viwanja walipewa na Bado hawakuhama sasa inabidi nguvu itumike Hakuna namna. Wachukulie kama zimesombwa na maji wakajipange upya

Mwishowe itakua mchezo kila anaetaka kiwanja anajenga sehemu isiyokubalika ili apewe kiwanja bure sehemu nzuri tena washukuru hata walipewa viwanja. Muafrika haendi bila fimbo
 
Umasikini wako siyo ticket ya wewe kuvunja sheria.

Hata vibaka wanaiba sababu ya umasikini tu wala siyo hobby yao.
 
Watanzania tumekuwa wakaidi na wabishi sana! Ni muda mrefu watu wanao ishi sehemu hatarishi na maeneo ya wa wazi kuondoka kwa hiyari yao lkn wamekuwa wakipuuza, sasa safari hii sioni haja ya kuongezewa hata siku Moja! Muda walio ishi hapo unatosha sana!, Serikali isi rudi nyuma kabisa iendelee na zoezi hilo. Watanzania bado hatujawa na utamaduni wa kutiii sheria bila SHURUTI, ulilegeza watajemga hadi katikati ya barabara.
 
Hivi hakukuwa na namna ya kuwaondoa kwa phase kabla ya kubomoa?au kuna utaratibu gani hapa,naona kama shagalabagala tu,masikini wanalala wapi?watoto shule je.Lowasa asingefanya huu upuuzi
 
Usifikiri wamependa kujenga mabondeni, ni umasikini tu. Mbona kina Magufuli wameuziana nyumba za kifahari za Oysterbay na Masaki?
kuwa masikini isiwe sababu ya kuvunja sheria za Nchi na wala usitumie hicho kama kisingizio cha kuonewa huruma.
 
Hakuna haja ya kungoja miezi 6, waliambiwa wahame tangu enzi za mzee wetu Ruksa lakini wanazidi kujenga tu. Tanzania ni kubwa kwa nini tubanane hapa Dar tu.
 
Akili bwana haya wamepewa miezi sita halafu wakaja kubomolewa lengo silile lile wamebomolewa

Tuache hayo nani kawauzia hivyo viwanja kunaserikali inatoa hati kiwanja kilicho ndani ya bonde

Pia tuache hilo hawa watu tokea wakati mkuu wa mkoa makamba waliambiwa wahame badala yake wakazidi kuiona serikali mafala wakaendelea kujenga...kipindi cha meck sadiki wakaambiwa tena na baadhi wakapewa viwanja,mabati,mifuko 100 ya cement bado wakauza nakurudi palepale kisa karibu na mjini

Kuchekeana,kubebana kumeisha sasa ni kazi tu WAVUNJIWE TU MAANA HAKUNA NAMNA
 
Hivi kila panapoitwa mita 60 kutoka kingo ya mto pakiendelea kubonolewa, eneo kama Kimara au Mbezi kuna nyumba itabaki?
 
Back
Top Bottom