Bombadier imetia hasara Taifa?

Bombadier imetia hasara Taifa?

Hii ni ripoti ya CAG ambayo imeanika kuhusu hii hasara kubwa. Huyu ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali unadhani atakurupuka na kuja na hasara kutoka kichwani kwake bila ya kuvikagua vitabu vya ATCL kwa kina ili aweze kufikia accurate conclusion!?

Ndugu yangu tunashukuru kwa taarifa yako. Lakn taarifa hii ina mapungufu fulani japo ni muhimu kuyaweka sawa.
Hebu fafanua na tuwekee hapa data zinazoonyesha hiyo hasara imetokanaje, sio kututajia amount tu ambazo hatujui zimetokana na hasara ya nmna gani.
 
Even though, he seems to lack wisdom and patience
If your passion is to ready people you need three lots in your mind
1. Knowledge
2.wisdom
3. Understanding
No matter what will happen you will meet their dreams and be blessed.
 
Tulisema biashara ya ndege si biashara ya matikiti maji, au mchezo wa kupanda na kuvuna. Baadhi wa wasomi uchwara wakasema tuna hila na Rais Magufulii , hatuna uzalendo na blablaa nyinginezo.

Nikasema maendeleo si ununuzi wa ndege, kwangu hayo ni maendeleo bandia, maendeleo yasiyo walenga wananchi ni sawa tu na kupulizia marashi umaskini .
Nikasema wanaharibu nchi hii si wale wanao ona mambo yanakwenda hovyo na kusema waziwazi bila woga, Bali ni wale wanao ona mambo yanakwenda mrama na kuamua kukaa kimya, na wakati mwingine kumshangilia, coz wanajua anapenda sifa .

Ununuzi wa ndege aina ya Bombardier ndani ya miaka miwili kwa mujibu wa mwenyekiti wa uwekezaji mitaji ya Umma Mh.Albert Ntabaliba, shirika LA ndege ATCL limepata hasara ya zaidi ya billion 223, ambazo ni zinatokana na hasara ya mwaka wa fedha 2015/16 hasara ya billion 109.3, mwaka wa fedha 2016/17 hasara ya billion 113.8 ambazo zinakupa jumla ya hasara ya billion 223.1 na ukijumlisha na billion 94.3 hasara ya mwaka wa fedha 2014/15 utapata jumla ya hasara billion 317.4!

Tuache hasara ya 2014/15! Tupigie hesabu zaidi ya billion 223. Zingeweza kufanya nini angalau wananchi wanufaike.

Kati ya nchi zenye ubovu wa huduma za afya duniani basi Tanzania ni moja wapo, na huwa nasema siku "nikitangaza nia" kipau mbele changu ni afya. Watanzania wengi wanakufa kwa sababu ya huduma mbovu na za hovyo za afya.

Ukichukua billion 223.1 ungeweza nunua CT-scan zaidi ya 120 kwa wastani wa CT-scan moja dollar million 850, ambazo ni sawa na tsh.billion 1.8.
Mashine hizi zingeweza kuwekwa katika hosptali zote za rufaa nchini hadi katik hospital za wilaya, na ingepunguza msongamano wa kutegemea CT-scan moja ya Muhimbili ambapo hadi watu kutoka Namtumbo, Chato, Tandahimba, Nakapanya nk hutegemea mashine moja iliyopo muhimbili.

Billion 223 zingeweza kujenga vyumba bora vya majengo ya upasuaji, takribani ya vyumba 450 kwa wastani wa sh. Million 420 ( Rejelea jengo jipya la hospitali ya mwananyamala) .
Vyumba hivyo vingekuwa ni msaada katika huduma za uzazi na mtoto,. Ila tumewekeza katika "biashara hasara"

Kama hukuwahi pata adha ya afya huwezi elewa haya masuala. Gari za kubebea wagonjwa katik nchi hii hazitoshelezi hata kidogo.

Mathalani hosptali ya mkoa wa morogor ina ambulance moja, bahati mbaya ikiwa inataka kumpeleka mgonjwa katika hospitali ya taifa, mtalazimishwa kusubiriana angalau mfike wagonjwa watatu hadi watano ndio iondoke kwenda Dar,. seriously???? Na huko mikoani yamkini hakuna kitu kinaitwa Gari la kubeba wa wagonjwa.

Ambulance moja kwa makadirio ya juu ni million 300, ukichukua billion 223 ungeweza nunua takribani ambulance 700, ambazo tungeweza ziweka katika hospital zote za wilaya hadi katika maeneo muhimu mjini kama serikali ya JK ilivyo nunua Pikipiki maalumu kwa ajili ya kusafirisha wagongwa wa dharura.

Pamoja na hayo pesa hiyo ingeweza maliza matatizo ya elimu ikiwemo malalamiko ya walimu, upungufu wa mabweni, madawati na tatizo la wanafunzi kukosa mikopo. Tatizo la ukosefu wa maji safi na salama, nk.

Nani wa kuhoji hayo, washauri wa raisi wanalinda ugali wao, mbaya zaidi serikali imesha jiondoa katik mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi "Open Government Partnership" hivyo tutegemee maovu mengi yaliyo fichika huko hasa ubobevu wa kupika takwimu.

Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]
Ikiwa Rais hataki takwimu ziwe wazi na Mh Nrabaliba kaamua kuzitoa basi ujue hasara ya ATCL ni zaudi ya bil 500.

Hebu turudi nyuma kwana ile bombadier ilinunuliwa bei gani hadi ituletee hasara kubwa namna hiyo?
 
Swala la ndege ni gumu sana angewekeza katika kilimo na utalii ili mapato yanayopatikana huko na kukuza ajira huko kodi yake baada ya miaka kadhaa iboreshe huduma za afya na si hicho alichofanya sema ndio uwezo wetu wa kufikiri ulipoishia acha tuendelee kuburuzwa tuu maana na bunge lipo kimya kama hakuna kinachoendelea...
Utalii angewekezaje mkuu?

Au ujui ndege na utalii ni mtambuka mkuu?
 
Misasa utalii unawekezwa kwa kupunguza gharama za ndege kwanza kutua KIA na matangazo kwa Nchi zilizoendelea kuhusu vivutio vyetu na pia kutumia mashirika ya ndege kutangaza vivutio tulivyo navyo kama Zambia na Zimbabwe wanavyoitangaza Victoria falls...SA wanavyoutangaza Table mountain wakati ni wa kawaida tuu ila wameweka lift na ipo chopa inayoweza kuwafikisha watalii kileleni...
 
Bombardier za kweli zilizobaki ni zile alizoziimba mkongwe Dully Sykes tu hizo nyingine fake fake fake mda unapita sijui zipo foleni kwenye mataa ndo zinachelewa
 
Ununuzi wa bombardier ulikuwa ni sifa za kisiasa na utawatokea puani sikh si nyingi
inaelekea unafurahia hujuma iliyofanywa...zisifanye kazi (kushikiliwa kwa baadha ya ndege hizo), ili upate cha kuikebehi serikali kwa maamuzi yake sahihi ya kutaka kufufua shirika letu wananchi la ndege. Ndiyo, nakuona unavyoikejeri serikali mitandaoni!!!

Tanzania ni nchi yetu sote mimi na wewe (kama ni raia wa Tanzania), mambo yanapoenda mrama kwa upande wa serikali yetu, tutafute namna bora ya kuondoa 'mrama' huo badala ya kejeri mitandaoni na kwingineko.
 
Tulisema biashara ya ndege si biashara ya matikiti maji, au mchezo wa kupanda na kuvuna. Baadhi wa wasomi uchwara wakasema tuna hila na Rais Magufulii , hatuna uzalendo na blablaa nyinginezo.

Nikasema maendeleo si ununuzi wa ndege, kwangu hayo ni maendeleo bandia, maendeleo yasiyo walenga wananchi ni sawa tu na kupulizia marashi umaskini .
Nikasema wanaharibu nchi hii si wale wanao ona mambo yanakwenda hovyo na kusema waziwazi bila woga, Bali ni wale wanao ona mambo yanakwenda mrama na kuamua kukaa kimya, na wakati mwingine kumshangilia, coz wanajua anapenda sifa .

Ununuzi wa ndege aina ya Bombardier ndani ya miaka miwili kwa mujibu wa mwenyekiti wa uwekezaji mitaji ya Umma Mh.Albert Ntabaliba, shirika LA ndege ATCL limepata hasara ya zaidi ya billion 223, ambazo ni zinatokana na hasara ya mwaka wa fedha 2015/16 hasara ya billion 109.3, mwaka wa fedha 2016/17 hasara ya billion 113.8 ambazo zinakupa jumla ya hasara ya billion 223.1 na ukijumlisha na billion 94.3 hasara ya mwaka wa fedha 2014/15 utapata jumla ya hasara billion 317.4!

Tuache hasara ya 2014/15! Tupigie hesabu zaidi ya billion 223. Zingeweza kufanya nini angalau wananchi wanufaike.

Kati ya nchi zenye ubovu wa huduma za afya duniani basi Tanzania ni moja wapo, na huwa nasema siku "nikitangaza nia" kipau mbele changu ni afya. Watanzania wengi wanakufa kwa sababu ya huduma mbovu na za hovyo za afya.

Ukichukua billion 223.1 ungeweza nunua CT-scan zaidi ya 120 kwa wastani wa CT-scan moja dollar million 850, ambazo ni sawa na tsh.billion 1.8.
Mashine hizi zingeweza kuwekwa katika hosptali zote za rufaa nchini hadi katik hospital za wilaya, na ingepunguza msongamano wa kutegemea CT-scan moja ya Muhimbili ambapo hadi watu kutoka Namtumbo, Chato, Tandahimba, Nakapanya nk hutegemea mashine moja iliyopo muhimbili.

Billion 223 zingeweza kujenga vyumba bora vya majengo ya upasuaji, takribani ya vyumba 450 kwa wastani wa sh. Million 420 ( Rejelea jengo jipya la hospitali ya mwananyamala) .
Vyumba hivyo vingekuwa ni msaada katika huduma za uzazi na mtoto,. Ila tumewekeza katika "biashara hasara"

Kama hukuwahi pata adha ya afya huwezi elewa haya masuala. Gari za kubebea wagonjwa katik nchi hii hazitoshelezi hata kidogo.

Mathalani hosptali ya mkoa wa morogor ina ambulance moja, bahati mbaya ikiwa inataka kumpeleka mgonjwa katika hospitali ya taifa, mtalazimishwa kusubiriana angalau mfike wagonjwa watatu hadi watano ndio iondoke kwenda Dar,. seriously???? Na huko mikoani yamkini hakuna kitu kinaitwa Gari la kubeba wa wagonjwa.

Ambulance moja kwa makadirio ya juu ni million 300, ukichukua billion 223 ungeweza nunua takribani ambulance 700, ambazo tungeweza ziweka katika hospital zote za wilaya hadi katika maeneo muhimu mjini kama serikali ya JK ilivyo nunua Pikipiki maalumu kwa ajili ya kusafirisha wagongwa wa dharura.

Pamoja na hayo pesa hiyo ingeweza maliza matatizo ya elimu ikiwemo malalamiko ya walimu, upungufu wa mabweni, madawati na tatizo la wanafunzi kukosa mikopo. Tatizo la ukosefu wa maji safi na salama, nk.

Nani wa kuhoji hayo, washauri wa raisi wanalinda ugali wao, mbaya zaidi serikali imesha jiondoa katik mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi "Open Government Partnership" hivyo tutegemee maovu mengi yaliyo fichika huko hasa ubobevu wa kupika takwimu.

Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]
Hii ishu inasikitisha sana, tunaangalia hasara baada ya hasara, na hatuna la kufanya. na katika uzi huu ambao kila kitu ni wazi kabisa kwamba tumekula wa chuya, wala huoni wana-Lumumba wakijisumbua kupitia. wataunda thread zao kuhusu matibabu ya Tundu Lissu, watauliza maswali na kujibu wenyewe. mtu aliyevunjiwa nyumba yake, pamoja na fremu alizokuwa anategemea, halafu anasoma taarifa kama hizi, ndio anazidi kupoteza matumaini. ndiyo raha ya kuongozwa na wendawazimu.
 
Sizonje anatia huruma Sana. Ila kakobe alimshauri vizuri tu ATUBU.

Shauri zake

Jay One

Rais wetu ana nia njema sana ktk kujenga nchi yetu..

One thing people failed to understand ikiwepo wasomi au wabunge ni kuwa ukiwekeza hela kubwa ktk business kubwa hasa kama za Airline, RETURN ON INVESTMENTS ( ROI ) inachukua muda kuanza kupata faida.. ATCL itaanza kupata faida after 3yrs na kuendelea, sijui kwanini watu wameshindwa kuelewa hili, big investments usitegemee eti first or second year of operation utaanza kupata faida.. But pamoja na ROI niseme ukweli pia ATCL management must be overhauled..!! Kuna matatizo ktk uongozi pale..
 
Kwani walisema zitaanza kutengeneza faida immedietly? Mbona watanzania tunapenda kuvuna ambavyo hatukupanda?
 
Return gani on inverstment mkuu?the company was in operation for a long time with at least one airplane(bombardier q300)toka wakati wa JK.JPM alichokifanya ni kuwakodishia ndege(hizo ndege ATCL wamelease kutoka serikalini).Nilitegemea kama wangekuwa business mind oriented wangepaswa kutengeneza faida,kwani hamna investment cost yoyote waliyoingia isipokuwa kulipa rental fee kwa serikali.

Inshort,revenue ni ndogo kuliko operational expenses.ATCL inahitaji restructure kubwa ya organization kuendana na uwezo wake.
 
Kwani walisema zitaanza kutengeneza faida immedietly? Mbona watanzania tunapenda kuvuna ambavyo hatukupanda?
Kuliko kununua ndege kisiasa heri hizo hela zingeenda kwenye miradi iwagusao wengi kwa pamoja mfano kujenga vyuo vya veta kila kata,watu wajifunze ujasiliamali.Huwezi kuleta ndege wakati umebana uchumi hela haizunguki.Au kusoma namba walidhani haitawahusu na wagawa namba. Chochote uwafanyio wengine lzm kitarudi kwako pia.Shida ya Atcl sio ndege ni management.
 
Shirika la ndege ATCL limepata hasara ya zaidi ya billion 223, ambazo ni zinatokana na hasara ya mwaka wa fedha 2015/16 hasara ya billion 109.3, mwaka wa fedha 2016/17 hasara ya billion 113.8 ambazo zinakupa jumla ya hasara ya billion 223.1 na ukijumlisha na billion 94.3 hasara ya mwaka wa fedha 2014/15 utapata jumla ya hasara billion 317.4!
Leo tunaongeza hasara nyingine.
 
Back
Top Bottom