Noel Shao
Member
- Jan 19, 2017
- 89
- 185
Tulisema biashara ya ndege si biashara ya matikiti maji, au mchezo wa kupanda na kuvuna. Baadhi wa wasomi uchwara wakasema tuna hila na Rais Magufulii , hatuna uzalendo na blablaa nyinginezo.
Nikasema maendeleo si ununuzi wa ndege, kwangu hayo ni maendeleo bandia, maendeleo yasiyo walenga wananchi ni sawa tu na kupulizia marashi umaskini .
Nikasema wanaharibu nchi hii si wale wanao ona mambo yanakwenda hovyo na kusema waziwazi bila woga, Bali ni wale wanao ona mambo yanakwenda mrama na kuamua kukaa kimya, na wakati mwingine kumshangilia, coz wanajua anapenda sifa .
Ununuzi wa ndege aina ya Bombardier ndani ya miaka miwili kwa mujibu wa mwenyekiti wa uwekezaji mitaji ya Umma Mh.Albert Ntabaliba, shirika LA ndege ATCL limepata hasara ya zaidi ya billion 223, ambazo ni zinatokana na hasara ya mwaka wa fedha 2015/16 hasara ya billion 109.3, mwaka wa fedha 2016/17 hasara ya billion 113.8 ambazo zinakupa jumla ya hasara ya billion 223.1 na ukijumlisha na billion 94.3 hasara ya mwaka wa fedha 2014/15 utapata jumla ya hasara billion 317.4!
Tuache hasara ya 2014/15! Tupigie hesabu zaidi ya billion 223. Zingeweza kufanya nini angalau wananchi wanufaike.
Kati ya nchi zenye ubovu wa huduma za afya duniani basi Tanzania ni moja wapo, na huwa nasema siku "nikitangaza nia" kipau mbele changu ni afya. Watanzania wengi wanakufa kwa sababu ya huduma mbovu na za hovyo za afya.
Ukichukua billion 223.1 ungeweza nunua CT-scan zaidi ya 120 kwa wastani wa CT-scan moja dollar million 850, ambazo ni sawa na tsh.billion 1.8.
Mashine hizi zingeweza kuwekwa katika hosptali zote za rufaa nchini hadi katik hospital za wilaya, na ingepunguza msongamano wa kutegemea CT-scan moja ya Muhimbili ambapo hadi watu kutoka Namtumbo, Chato, Tandahimba, Nakapanya nk hutegemea mashine moja iliyopo muhimbili.
Billion 223 zingeweza kujenga vyumba bora vya majengo ya upasuaji, takribani ya vyumba 450 kwa wastani wa sh. Million 420 ( Rejelea jengo jipya la hospitali ya mwananyamala) .
Vyumba hivyo vingekuwa ni msaada katika huduma za uzazi na mtoto,. Ila tumewekeza katika "biashara hasara"
Kama hukuwahi pata adha ya afya huwezi elewa haya masuala. Gari za kubebea wagonjwa katik nchi hii hazitoshelezi hata kidogo.
Mathalani hosptali ya mkoa wa morogor ina ambulance moja, bahati mbaya ikiwa inataka kumpeleka mgonjwa katika hospitali ya taifa, mtalazimishwa kusubiriana angalau mfike wagonjwa watatu hadi watano ndio iondoke kwenda Dar,. seriously???? Na huko mikoani yamkini hakuna kitu kinaitwa Gari la kubeba wa wagonjwa.
Ambulance moja kwa makadirio ya juu ni million 300, ukichukua billion 223 ungeweza nunua takribani ambulance 700, ambazo tungeweza ziweka katika hospital zote za wilaya hadi katika maeneo muhimu mjini kama serikali ya JK ilivyo nunua Pikipiki maalumu kwa ajili ya kusafirisha wagongwa wa dharura.
Pamoja na hayo pesa hiyo ingeweza maliza matatizo ya elimu ikiwemo malalamiko ya walimu, upungufu wa mabweni, madawati na tatizo la wanafunzi kukosa mikopo. Tatizo la ukosefu wa maji safi na salama, nk.
Nani wa kuhoji hayo, washauri wa raisi wanalinda ugali wao, mbaya zaidi serikali imesha jiondoa katik mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi "Open Government Partnership" hivyo tutegemee maovu mengi yaliyo fichika huko hasa ubobevu wa kupika takwimu.
Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]