Bombadier imetia hasara Taifa?

Bombadier imetia hasara Taifa?

Uwezi kuwa na shirika ambalo lina wafanyakazi wengi kuliko nyenzo za uzalishaji.

Nakumbuka enzi za JK awamu ya pili shirika lilikuwa na ndege 1 Bombardier Q-300,lakini ukitembelea ofisi zao mtaa wa Ohio Downtown,ofisi zote unakuta zimejaa watu.Nikawa najiuliza hawa watu wanalipwa kwa mapato yapi?Ya ndege hii ambayo aibebi ata abiria 60.

Kwa mazingira hayo,sishangai shirika linaendelea kuoperate kwa mazingira hayo.Kilichoongezeka ni ndege tu hila business aa usual.
 
Any nation to prosper should have at least four pillars if not mistaken
1/ rule of law
2/ inclusive decision-making
3 / respect for human right
4 / democracy.
Which of the above is being practised in Tanganyika at the required level?
 
Ukichukua billion 223.1 ungeweza nunua CT-scan zaidi ya 120 kwa wastani wa CT-scan moja dollar million 850, ambazo ni sawa na tsh.billion 1.8.

Sidhani kama dola milioni 850 ni bilioni 1.8,au ni dola ya nchi ingine na siyo ya kimarekani.
Weka vizuri hesabu zako tafadhali.
CT Scan moja wastani wa dollar million 850?
 
Kukurupuka na kutaka sifa. Mishahara yenyewe midogo wanawalalia Wafanyakazi kwa miaka chungu nzima wakati wenyewe wakilipana mamilioni. Kama mishahara ya Wafanyakazi wengi haitoshi kwenye gharama zao za kila siku za maisha hiyo pesa ya ziada ya kupandia ndege wataitoa wapi!?

Na si ajabu mwenye chuki za kutisha na roho mbaya akahoji mishahara yenu Wafanyakazi naijua mnapata wapi pesa za kupanda ndege kila mara na familia zenu!?

Tatizo ni ushamba na umbumbumbu!
 
Kukurupuka na kutaka sifa. Mishahara yenyewe midogo wanawalalia Wafanyakazi kwa miaka chungu nzima wakati wenyewe wakilipana mamilioni. Kama mishahara ya Wafanyakazi wengi haitoshi kwenye gharama zao za kila siku za maisha hiyo pesa ya ziada ya kupandia ndege wataitoa wapi!?

Na si ajabu mwenye chuki za kutisha na roho mbaya akahoji mishahara yenu Wafanyakazi naijua mnapata wapi pesa za kupanda ndege kila mara na familia zenu!?
Na hakuna malipo ya likizo pamoja na kwamba ni peanuts.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndugu yangu tunashukuru kwa taarifa yako. Lakn taarifa hii ina mapungufu fulani japo ni muhimu kuyaweka sawa.
Hebu fafanua na tuwekee hapa data zinazoonyesha hiyo hasara imetokanaje, sio kututajia amount tu ambazo hatujui zimetokana na hasara ya nmna gani.
 
Wewe mleta uzi hutaki nchi iwe na Shirika la ndege au?Naomba jibu kuna kitu nataka kukuuliza ukishanijibu
 
Nashauri tufute ruzuku ili tujenge vyumba vya upasuaji
 
Jamaa anawatia roba na kuwasachi wapanda ndege halafu unamsikia kesho yake anahamasisha ununuzi wa ndege.

Yaani Pogba hajui kama hajui, siku akijua hajui atakuwa mtu mzuri kweli kweli.
 
Mkuu Shao, hesabu imekuwa tatizo kubwa kama sio upotoshaji wa makusudi. Hasara ya 2014/15 ni 94.3, 2015/16 ni 109.3 maana yake hasara ni 15 bilioni ya huo mwaka, 2016/17 ni 113.8 yaani hasara ya mwaka ni 4.5 bilioni. Kwa faida yako hasara ya mwaka uliopita ndio hufungulia mahesabu ya mwaka uliopo. Toa ufafanuzi wako sasa kwa kutumia mahesabu hayo halisi kuhusu CT scan.

yaanQUOTE="Noel C Shao, post: 25635315, member: 410574"]Tulisema biashara ya ndege si biashara ya matikiti maji, au mchezo wa kupanda na kuvuna. Baadhi wa wasomi uchwara wakasema tuna hila na Rais Magufulii , hatuna uzalendo na blablaa nyinginezo.

Nikasema maendeleo si ununuzi wa ndege, kwangu hayo ni maendeleo bandia, maendeleo yasiyo walenga wananchi ni sawa tu na kupulizia marashi umaskini .
Nikasema wanaharibu nchi hii si wale wanao ona mambo yanakwenda hovyo na kusema waziwazi bila woga, Bali ni wale wanao ona mambo yanakwenda mrama na kuamua kukaa kimya, na wakati mwingine kumshangilia, coz wanajua anapenda sifa .

Ununuzi wa ndege aina ya Bombardier ndani ya miaka miwili kwa mujibu wa mwenyekiti wa uwekezaji mitaji ya Umma Mh.Albert Ntabaliba, shirika LA ndege ATCL limepata hasara ya zaidi ya billion 223, ambazo ni zinatokana na hasara ya mwaka wa fedha 2015/16 hasara ya billion 109.3, mwaka wa fedha 2016/17 hasara ya billion 113.8 ambazo zinakupa jumla ya hasara ya billion 223.1 na ukijumlisha na billion 94.3 hasara ya mwaka wa fedha 2014/15 utapata jumla ya hasara billion 317.4!

Tuache hasara ya 2014/15! Tupigie hesabu zaidi ya billion 223. Zingeweza kufanya nini angalau wananchi wanufaike.

Kati ya nchi zenye ubovu wa huduma za afya duniani basi Tanzania ni moja wapo, na huwa nasema siku "nikitangaza nia" kipau mbele changu ni afya. Watanzania wengi wanakufa kwa sababu ya huduma mbovu na za hovyo za afya.

Ukichukua billion 223.1 ungeweza nunua CT-scan zaidi ya 120 kwa wastani wa CT-scan moja dollar million 850, ambazo ni sawa na tsh.billion 1.8.
Mashine hizi zingeweza kuwekwa katika hosptali zote za rufaa nchini hadi katik hospital za wilaya, na ingepunguza msongamano wa kutegemea CT-scan moja ya Muhimbili ambapo hadi watu kutoka Namtumbo, Chato, Tandahimba, Nakapanya nk hutegemea mashine moja iliyopo muhimbili.

Billion 223 zingeweza kujenga vyumba bora vya majengo ya upasuaji, takribani ya vyumba 450 kwa wastani wa sh. Million 420 ( Rejelea jengo jipya la hospitali ya mwananyamala) .
Vyumba hivyo vingekuwa ni msaada katika huduma za uzazi na mtoto,. Ila tumewekeza katika "biashara hasara"

Kama hukuwahi pata adha ya afya huwezi elewa haya masuala. Gari za kubebea wagonjwa katik nchi hii hazitoshelezi hata kidogo.

Mathalani hosptali ya mkoa wa morogor ina ambulance moja, bahati mbaya ikiwa inataka kumpeleka mgonjwa katika hospitali ya taifa, mtalazimishwa kusubiriana angalau mfike wagonjwa watatu hadi watano ndio iondoke kwenda Dar,. seriously???? Na huko mikoani yamkini hakuna kitu kinaitwa Gari la kubeba wa wagonjwa.

Ambulance moja kwa makadirio ya juu ni million 300, ukichukua billion 223 ungeweza nunua takribani ambulance 700, ambazo tungeweza ziweka katika hospital zote za wilaya hadi katika maeneo muhimu mjini kama serikali ya JK ilivyo nunua Pikipiki maalumu kwa ajili ya kusafirisha wagongwa wa dharura.

Pamoja na hayo pesa hiyo ingeweza maliza matatizo ya elimu ikiwemo malalamiko ya walimu, upungufu wa mabweni, madawati na tatizo la wanafunzi kukosa mikopo. Tatizo la ukosefu wa maji safi na salama, nk.

Nani wa kuhoji hayo, washauri wa raisi wanalinda ugali wao, mbaya zaidi serikali imesha jiondoa katik mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi "Open Government Partnership" hivyo tutegemee maovu mengi yaliyo fichika huko hasa ubobevu wa kupika takwimu.

Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG][/QUOTE]
 
Hili suala limezungukwa na porojo, hasara inatoka wapi wakati abiria wanalipa nauli?

Hizo ndege sio za atcl ni za serikali zimekodishwa atcl, ukisema hasara haimaanishi abiria hawakulipa nauli au ilikuwa inasafiri tupu.
 
Biashara hazitaki amri zina kanuni zake. Utawala wake ataishia tu kuongeza deni la taifa maradufu.
Hizo ndege wapande wana ccm sitii mguu.
 
Ndugu yangu tunashukuru kwa taarifa yako. Lakn taarifa hii ina mapungufu fulani japo ni muhimu kuyaweka sawa.
Hebu fafanua na tuwekee hapa data zinazoonyesha hiyo hasara imetokanaje, sio kututajia amount tu ambazo hatujui zimetokana na hasara ya nmna gani.
Kamat ya Bunge ya uwekezaji (PIC) ilishaweka wazi wiki hii inayoisha
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Why? Could it be because of Faru Yohana Konyagi's dictatorship behaviour?
Not because of our president it os because of our constitution faulty that give absolute power to the president to act above the law by giving him immunity against unlawful action committed by him.
 
hiyo ni lazima wapate hasara coz walikuwa hawana marubani wameajiri Sana wanejipanga Sana so kwa kutegemea input ya ndege mbili lazima wapate hasara
 
Not because of our president it os because of our constitution faulty that give absolute power to the president to act above the law by giving him immunity against unlawful action committed by him.
Even though, he seems to lack wisdom and patience
 
Back
Top Bottom