Bomba la mafuta kutoka Uganda kuingiza bilioni 4.8 kila siku

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga ukikamilika utaliingizia Taifa Sh4.8 bilioni kila siku.

Amesema fedha hizo zitatokana na usafirishaji wa mapipa 200,000 kila siku yatakayotozwa dola 12.2 (zaidi ya Sh24,000) kila moja.

Profesa Muhongo alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala ambako Rais wa Uganda, Yoweri Museveni juzi alitangaza kuwa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Hoima, Ziwa Albert litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga.

Alisema katika kujipanga kwa ajili ya mradi huo, tayari Serikali imetoa kibali kwa wanafunzi 22 ambao wamepelekwa nje ya nchi kusomea masuala ya mafuta na gesi katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu.

“Bomba litakamilika Juni 2020 na itakuwa ni zawadi kwa Rais John Magufuli kabla hajarudisha fomu ya kuomba tena kugombea awamu ya pili ya urais.Lakini tutajitahidi likamilike kabla ya muda huo,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema utakapokamilika, yatahitajika magari 100,000 ya kutolea mizigo katika Bandari ya Tanga.

Juzi, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ilieleza kuwa Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wa kutumia Bandari ya Tanga.

Rais Museveni alitangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika jijini Kampala juzi na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga na Profesa Muhongo.

Chanzo:
Mpekuzi
 
Hongera Muhongo,waziri wa mambo ya nchi za nje na timu zao kwa kazi kubwa iliyotukuka kwa taifa.Hizi ndizo habari za maana tunazopenda wananchi kuzisikia sio zile za Sijui UKAWA wasusa bunge SIJUI UKAWA WAZOMEA SPIKA hatutaki habari za kijinga kama hizo.
 
Wandugu,
Mbona hatuongelei kabisa bomba la mafuta la TAZAMA kwenda Zambia?
Hili nalo huko mbele lisije likageuka na kuwa kama hilo la TAZAMA ambalo kwa sehemu kubwa sasa ni a white elephant.
Tusikimbilie tu miradi mipya huku ya zamani tunaiua.

Fufueni na TAZAMA tuachane na malori yanaharibu barabara.
 
Bomba la TAZAMA kazi yake ni kusafirisha mafuta yasiyosafishwa toka Dar es salaam kwenda Zambia.Malori ya mafuta yanabeba mafuta yaliyosafishwa kama petrol,diesel na mafuta ya taa kupeleka mikoani na nchi jirani .Mafuta yasiyosafishwa yanatumia bomba wakati malori yanatumia barabara.Unaongelea vitu viwili tofauti mkuu!!!!
 
Ndio, Prof. Muhongo ni jembe, ni presidential material, ni asset kubwa kwa taifa hili. Natamani baada ya JPM Prof. achukue kijiti. Au age itam-limit?
 
Wandugu,
Mbona hatuongelei kabisa bomba la mafuta la TAZAMA kwenda Zambia?
Hili nalo huko mbele lisije likageuka na kuwa kama hilo la TAZAMA ambalo kwa sehemu kubwa sasa ni a white elephant.
Tusikimbilie tu miradi mipya huku ya zamani tunaiua.

Fufueni na TAZAMA tuachane na malori yanaharibu barabara.
TAZAMA unapga kazi
 
Nimeskia pia kuwa Rais Uhuru kenyata alikuwepo wakati Yoweri Museveni akipitisha uamuzi huo.Ila Prof.Muhongo "Alisema utakapokamilika, yatahitajika magari 100,000 ya kutolea mizigo katika Bandari ya Tanga",hapa sijapaelewa vizuri ni mizigo gani itakuwa ikitolewa hapo Tanga au ni hayo Mafuta na itakuwa ikipelekwa wapi?
 
Hongera Muhongo,waziri wa mambo ya nchi za nje na timu zao kwa kazi kubwa iliyotukuka kwa taifa.Hizi ndizo habari za maana tunazopenda wananchi kuzisikia sio zile za Sijui UKAWA wasusa bunge SIJUI UKAWA WAZOMEA SPIKA hatutaki habari za kijinga kama hizo.

wewe zetazeta unajua kuwa kuna Bomba la TAZAMA
 
Hongera Muhongo,waziri wa mambo ya nchi za nje na timu zao kwa kazi kubwa iliyotukuka kwa taifa.Hizi ndizo habari za maana tunazopenda wananchi kuzisikia sio zile za Sijui UKAWA wasusa bunge SIJUI UKAWA WAZOMEA SPIKA hatutaki habari za kijinga kama hizo.

ukawa lazima wawepo ili upate woga muda wote si unaona mwenyewe faida moja wapo ya ukawa unaandika kumpa pongezi mhongo lakini kwnye akili yako unawaza vp kuwakwepa ukawa huo tayar ni woga ambao unapelekea rasimali za taifa kuwa salama mana lazima mtaogopa jamaa wakajiu watasema tu hamtajichukulia hovyo.

pia changamoto lazima wapewe sio habari za kijinga hizi sio zama za fikra za mwenye kiti zidumu bunge lazima liwe moto si unakumbuka wakina wasira walivokuwa wanalala je wakibak peke yao si ni mwendo wa kugonga meza tu.

mwisho napongeza kwa hatua hizo za muhongo kwa maslahi makubwa ya taifa.
 
Hongera Muhongo,waziri wa mambo ya nchi za nje na timu zao kwa kazi kubwa iliyotukuka kwa taifa.Hizi ndizo habari za maana tunazopenda wananchi kuzisikia sio zile za Sijui UKAWA wasusa bunge SIJUI UKAWA WAZOMEA SPIKA hatutaki habari za kijinga kama hizo.
Hahahahahahh ni kweli mkuu, habari njema kama hii hao jamaa huwa hawapendi zitokee maana kiuhalisia huwa zinawanyima raha!
 
Utashangaa umaskini ndipo utakapoongezeka kwa Watz, nchii hii inaingiza Mapato zaid ya hayo lkn mpk Leo hatujui Kwanini Ni masikini?
 
Wandugu,
Mbona hatuongelei kabisa bomba la mafuta la TAZAMA kwenda Zambia?
Hili nalo huko mbele lisije likageuka na kuwa kama hilo la TAZAMA ambalo kwa sehemu kubwa sasa ni a white elephant.
Tusikimbilie tu miradi mipya huku ya zamani tunaiua.

Fufueni na TAZAMA tuachane na malori yanaharibu barabara.

Kwa nini unasema ni white elephant? Halisafirishi mafuta tena?
 
tunataka kujua serikali yetu itapata shilingi ngapi katika hiyo fedha.

lipo tatizo la kuamini katika illusions, kwa ndio mafuta kutozwa dola 12.2 lakini kumbe pengine ni fedha inayolipwa kwa mmiliki wa bomba la mafuta ambaye nchi yetu inaweza kutokuwa mmiliki.

tukaishia kupata tozo ya 4% katika madini maana yake ni katika hiyo dola 12.2 asilimia 4 tu ni sawa na almost cent 50 za kiamerika.

tumewahi kusikia analysis kama hizi kwenye madini kwa kutuambia madini yaliyogunduliwa ayana thamani kubwa na tunaanza kutembea vifua mbele but mbele ya safari tunaingia mikataba ya kipuuzi na kuwa masikini.

tueleze hiyo dola 12.2 inalipwa kwa serikali ya tz au inalipwa kwa mmiliki wa bomba la mafuta then itategemea mikataba ya ujenzi na uendeshaji wa bomba, mitambo ya kusukuma, na bandari?

tunahitaji picha halisi ya mradi sio kutujengea illusions zisizo na tija.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga ukikamilika utaliingizia Taifa Sh4.8 bilioni kila siku.

Amesema fedha hizo zitatokana na usafirishaji wa mapipa 200,000 kila siku yatakayotozwa dola 12.2 (zaidi ya Sh24,000) kila moja.

Profesa Muhongo alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala ambako Rais wa Uganda, Yoweri Museveni juzi alitangaza kuwa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Hoima, Ziwa Albert litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga.

Alisema katika kujipanga kwa ajili ya mradi huo, tayari Serikali imetoa kibali kwa wanafunzi 22 ambao wamepelekwa nje ya nchi kusomea masuala ya mafuta na gesi katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu.

“Bomba litakamilika Juni 2020 na itakuwa ni zawadi kwa Rais John Magufuli kabla hajarudisha fomu ya kuomba tena kugombea awamu ya pili ya urais.Lakini tutajitahidi likamilike kabla ya muda huo,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema utakapokamilika, yatahitajika magari 100,000 ya kutolea mizigo katika Bandari ya Tanga.

Juzi, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ilieleza kuwa Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wa kutumia Bandari ya Tanga.

Rais Museveni alitangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika jijini Kampala juzi na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga na Profesa Muhongo.

Chanzo:
Mpekuzi
 
ki ukweli imefika mahali vitu ambavyo havina tija tuachane navyo mfano TAZARA na TAZAMA sioni kama wa TZ tunafaidika navyo wakati tulitumia gharama na muda mwingi kuvitengeneza.
 
MIMI SIIJUI BANDARI YA TANGA ILIVYO MAANA NAISHIAGA BARABARANI TU, KINACHOFANYA NIWAZE NI UWEZO WA BANDARI YENYEWE KUMUDU MIKIMIKI YA MALORI LAKI MOJA HII SIO MCHEZO. KWA MAANA NYINGINE NINAMAANA INABIDI IPANULIWE KWA KIWANGO KIKUBWA. HONGERA MHESHIMIWA RAIS, HONGERA NYINGI KWA WATENDAJI WOTE WALIOSHIRIKI KWENYE MAPAMBANO HAYA MWANZO MPAKA HAKIKA HII NI NEEMA KUBWA ITASHANGAZA KUSIKIA TENA SHULE FULANI HAINA MADAWATI AUHOSPITALI FULANI HAINA HATA ANGALAU PANADOL YA KUTULIZA MAUMIVU.
 
Back
Top Bottom