Bolton kukutana na Israel juu ya suala la majeshi ya Marekani kuondoka Syria

SECRET AGENT

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
252
488
Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani anajaribu kuiondolea Israel wasiwasi kuhusu uamuzi wa Rais Donald Trump wa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Syria.

John Bolton anakusudia kukutana na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na viongozi wengine hapo kesho Jumapili. Bolton pia anatarajiwa kuitembelea Uturuki wiki ijayo.

Amri ya Trump kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Syria aliyoitangaza mwezi uliopita inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha wiki kadhaa lakini itacheleweshwa kutokana na Trump kukubali maombi kutoka kwa wasaidizi wake, washirika na wabunge wanaotaka amri hiyo ifanyike kwa kufuata utaratibu mzuri.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa sasa hakuna ratiba maalum na hivyo majeshi ya Marekani yatabaki kwa muda katika kituo cha msingi cha kijeshi cha al-Tanf, kusini mwa Syria. Marekani iliwapeleka askari wake kwa ajili ya kupambana na wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS na kuzuia kuongezeka kwa ushawishi wa Iran katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom