Bollen Ngetti: Dk. Bashiru, Membe si size yako, kaa kimya

s
Naona umeweka wosifu wa mh Membe..sio tatizo..
Lakini haibadilishi lolote..kila zama zina watu wake na yeye kashakuq zilipendwa hatakama mkilia vipi ndio ukweli mchungu..

Ccm ya sasa ni kazi tuu sio maneno matupu mliokua nayo kwenye the previous regime

Mkia ushakatwa subirini uote kama kunahiyo miujiza.
2020 expect unexpected !
 
Mku umeeleweka vizuri na ushauri tauzingatia kwani ni dozi
 
🤔🤐 Dah, Bollen umeandika vitu vizito sana, sasa si ungesubiri Katibu Mkuu wetu afungue, au unataka afungue kwa lazima, huu ujumbe mzito sana..!! Mm CCM from flesh to blood, nime save huu ujumbe aisee..!!
 
Sure.Kwa muda mrefu sana sijasoma uzi wa maana jf kama huu zaid ya hiz nyuz za watoto wa kidato cha 6 waliomaliza paper.Shukran bwana Ngeti Bollen
 
THE DIFFERENCE IS THE SAME

Video imerekodiwa kumuonyesha R akimshauri B mwisho wa mwaka 2018. Alierekodi video ni shirika M ambao Ni marafiki Sana na B ambae anasemwa kwenye video.

Mwaka uliofuatia May 2019, Shirika M linaachia video kwa Public, Kesho yake B anajitokeza kujibu video ambayo alikuwa anajua ipo tangu mwisho wa mwaka 2018, anajibu anajifanya amepanic, ameumia sana

Alafu anatokea Kiongozi mkubwa wa chama KM anamjibu B.

Watu wanaibuka kushangilia kwamba Sasa B amepatikana, R amemtoa B mafichoni kilichobaki Ni kumponda kichwa afe.

HAIKO HIVYO.

Sisi tunaopenda kushirikisha akili zetu kwenye maamuzi tunaona picha tofauti kabisa, tunaona maigizo makubwa, yaani picha inaanza staring anakufa kwenye majani.

Picha yangu inanionesha kwamba R alitekodi ile video kwa maana Maalum kabisa, na B hakuijibu kwa wakati mpaka akamilishe Jambo ambalo alikuwa anapambana nalo Sana au mkakati aliokuwa anakamilisha, baada ya kuweka mambo sawa mwaka unaofuata Sasa ndo anajitokeza kujibu kwa kuumia na kupanic ili kuwapoteza wananchi.

Hayo Ni mawasiliano ya Hali ya juu Sana, inakuwa Kama ishara ya Jambo fulani kuanza au kuingia hatua inayofuata. Kuna codes nyingi Sana za mawasiliano.

Wajuvi wa mambo wanaona Kama R, B na KM wote ni sehemu Moja, wote ni watu wenye akili nyingi Sana, sio wa kupuuzwa kabisa. Kinachoonekana kwa watu wa kawaida ni maluelue na mazingaombwe tu.
 
SHIKAMOO Mwalimu Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM. Nina hakika una afya njema hapa Lumumba ukiwa juu ya kiti chako cheusi cha kuzunguka zunguka ukipitia mafaeli mbalimbali ya kiutendaji.

Naomba umuagize Esther akuletee juisi baridi sana kama haujafunga ukae kwa utulivu mkubwa kusoma waraka huu mchungu!

Ninajua vijana wenzangu hawapendi kukuambia maneno haya machungu kwa hofu ya nafasi zao, kwa nidhamu ya woga, au kwa kujipendekeza tu kuwa karibu na "high table" kuokoteza masazo. Kwa bahati mbaya sina sifa hizo zote. Kwa hiyo licha ya kupuuza mitandao ya kijamii lakini ninajua basi hata wasaidizi Wako watakusimulia japo kwa ufupi!

Naanza! Dk. Bashiru, wewe ni miongoni mwa wasomi wachache sana hapa nchini waliopata kuheshimika sana na kada ya wanazuoni hasa pale ulipokuwa kinara wa Kigoda cha Mwalimu. Kila neno lililotoka kinywani mwako halikutoroka, ulilitafakari kwanza ndipo ulisema jambo ambalo ni sifa ya msomi yeyote. Ilipotangazwa mdahalo wowote watu waliposikia atakuwepo Dk. Bashiru kama mchokoza mada nani alithubutu kukosa?

Ukumbi wa Nkuruma ulijaa kwa mvuto Wako na wanazuoni wenzio kina Prof Shivji nakadhalika. Vijana wengi (nikiwemo) walivutiwa na fikra zako za Kiafrika, Umajumuhi na Uzalendo ukipinga kila aina ya ubaguzi katika jamii. Kilichovutia ni kwamba ulifanya haya yote kwa ujira mdogo, mishahara ya UDSM inajulikana, hukuwa na gari ya V8, hukuwa na dereva wala mlinzi. Lakini ulikuwa "role model" wa vijana wengi!

Vijana wale wanajiuliza hivi huyu Bashiru ambaye ni SG wa CCM ndiye yule wa UDSM au ni ndugu wanaofanana? Hawapati majibu. Lakini wakiamini kuwa ni yuleyule basi wakubalie wakutambue kama msaliti wa Taifa lao.

Nivumilie tu mtani wangu maana tusiposema Leo wanetu watakuja kutandika viboko makaburi yetu kwa nini hatukusema haya.
Ndg Bashiru, ulipopewa nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CCM ukawa sawa na mtu aliyebadili dini. Ulisema, "mimi ni mtendaji wa chama, sitokuwa mwanasiasa wa majukwaani na ni marufuku watendaji kupiga siasa". Katika gazeti la Raia Mwema nikakuhoji, "Bashiru Ally utayaweza usemayo? Unakijua CCM?" Hukunijibu maana Bollen Ngetti ni mdudu gani?

Ndg Bashiru, umeshindwa kukaa ofisini kuwa Mtendaji na badala yake umeingia kwenye mtego wa kupiga siasa za mipasho na majibizano na wanasiasa. Labda akili yako inakutuma kuamini kuwa huo ndio utendaji wenyewe. You are very wrong brother. Here we go!

Jana umejitokeza hadharani ukasema maneno yafuatayo:

"Kazi ya Mwana-CCM halisi ni kusema kosa na kutoa namna ya kutatua kosa hilo. Anayesema kosa halafu anatumia misamiati isiyotambulika ni Mwana-CCM nyemelezi. Mwana-CCM halisi anaruhusiwa kukosoa Serikali na chama kwa adabu. Haijalishi una mkia au hauna mkia".

Ndg Bashiru Ally (mpya) bila kupepesa macho na kuacha unafiki ujumbe wako ulimlenga Mwanadiplomasia Bernard Membe. Ukibisha shindana na nafsi yako katika mwezi mtukufu!

Membe kama mwanasiasa asiye mtendaji wa chama kama wewe anao uhuru wa kufanya siasa kwa namna anavyoona inafaa na kila jukwaa analopata. Na kama ambavyo tunaweza kuzuia ndege asitue juu ya kichwa chako lakini hatuwezi kumchagulia pakujenga kiota chake ndivyo ilivyo ngumu kumchagulia maneno ya kutumia mwanasiasa asiye mtendaji maana kwa maneno yake mwanasiasa hufa au huishi kisiasa.

Akimjibu rafiki yake jasusi na mafia wa kiuchumi Rostam Abdulaziz, Membe alimwambia, "Rostam wewe ni mchumi, tuzungumzie masuala ya uchumi, tuzungumze kwa nini biashara ndogo na kubwa zinafungwa, kwa nini uchumi wetu umefikia hapa, usijifanye wewe ni christian than Romans, Rostam wewe na mimi sote tumekatwa mikia hata ukijifanya kuwa karibu namna gani mkia ukikatwa hauoti. Usijifanye wewe ni mzawa mimi na wewe sote ni watoto wa kambo".

Ndg Bashiru, kupitia kwa maneno hayo ya Membe ndio ulipoona kuna wana CCM halisi na nyemelezi. Kwamba "Nyemelezi" ni wanaokosoa Serikali bila adabu. Membe anahoji kwa nini biashara ndogo na kubwa zinafungwa, kwa nini uchumi umefika hapa? Ingekuwa ni Bashiru wa UDSM ungejua maana ya maswali ya Membe kwa Rostam lakini kwa kuwa unaendeshwa ndani ya V8, unaye mlinzi, mpishi, nyumba, mshahara mnono na marupurupu kibao huwezi kuona maana ya "kwa nini uchumi wetu umefikia hapa?"

Ndg Bashiru, Membe ametembea katika maneno ya Mwenyekiti Magufuli aliyefananisha wanaCCM wanaohama na kurudi sawa na ng'ombe waliokatwa mikia zizini utawatambua kama Lowassa, Waitara, Makongoro, Wasira nakadhalika. Lakini na wewe badala ya kufanya kazi ya kuwaunganisha wanachama ukidai Membe kutumia misamiati isiyotambulika (sijui ni ipi inayotambulika) na wewe umeongeza jambo. Kumbe kuna CCM Halisi na CCM Nyemelezi.

Kina Membe na Rostam ni Nyemelezi. Kwako misamiati hii ndiyo inayotambulika (sijui utambuzi unafanyika na taasisi gani). Kwa maneno mepesi yasiyohitaji utambuzi Ndg Bashiru umeshindwa kuwaunganisha wana CCM na badala yake sasa tunaanza kuulizana "wewe ni halisi au nyemelezi?"

Nape Nnauye amehoji, "fedha zinakwenda wapi? Tumebana matumizi, tumeondoa wafanyakazi na wanafunzi hewa, fedha ziko wapi? Tunawekeza kwenye vitu badala ya maendeleo ya watu". Bila shaka Nape sasa ni Mwana CCM Nyemelezi maana mstari unaotenganisha maswali yake na Membe ni mwembamba sana!

Ndugu Bashiru, ni adabu gani unaotaka CCM nyemelezi watumie kuhoji Serikali? Ulitaka Membe na Nape wakuandikie barua kuuliza kwa nini biashara ndogo na kubwa kufungwa na ziliko fedha? Kwani hujui nchi hii ni ya raia wote? Lakini pia kwa nini unadhani ni WanaCCM halisi pekee ndio wanastahili kukosoa Serikali na si upinzani? Unakwama wapi mtani wangu mpendwa?

Hebu tazama, ulipomwita Membe hadharani ukiwa Chato na kumtaka afike haraka sana ofisini kwako kujibu kwanini "anahujumu" Serikali ya JPM wewe pale ulitumia adabu kumwita na hivyo wewe ni Halisi? Membe alikujibu kwamba inaweza ni uchanga na ugeni katika ofisi kubwa kama ya CCM, huo ugeni haujaisha? Huu woga kwa Membe unatokana na nini? Mbona parandesi moja tu ya maneno kiti kimekuwa cha Moto?

Dk. Bashiru Ally, naomba nikutambulishe kwa Membe: unapambana na kachero mbobezi wa kimataifa, unapambana "battle plan master" vita vya Kagera, unapambana na Mwalimu wa makachero wa Scotland Yard, unapambana na mtu wa karibu wa Papa, unapambana na mshauri wa marais 5 Afrika katika masuala ya diplomasia na usalama, unapambana na mcha Mungu halisi, unapambana na kada mwandamizi wa CCM anayekijua chama na tendegu zake! Hizo ni baadhi tu ya wasifu wa binadamu!

Labda, nikukumbushe tu kidogo mtani wangu. Unakumbuka ulipoagizwa kumwita Membe ukauliza ushahidi upo? Je, baadaye mliupata huo ushahidi? Au bado mnausubiri uje kutoka Afrika Kusini?

USHAURI: Kwa kuwa umetutaka wanaCCM halisi kutoa maoni namna ya kutatua tatizo, na mimi sitaki kuwa "nyemelezi" natoa maoni. Unganisha chama na wanachama. Usiwagawe. Hayo ya halisi na nyemelezi tuachie sie huku kijiweni wewe hustahili. Pili, rejea Ubashiru wa Kigoda cha Mwalimu. Acha demokrasia ichanue ndani ya chama.

Wana CCM sisi ni watu wa kujimwahimwahi na kuwa huru. Wewe simamia haki, utu, usawa, achana na mambo ya "utamaduni wetu" wewe na nani? Nakutakia Mfungo Mwema!

Ndimi Mjoli wako,
Bollen Ngetti
23/5/2019
Uchambuzi mwafaka!
 
Utakuwa Camillius si kwa povu hili maana Dokta akutaja jina la mtu ungeweka clip tukimuona Dokta Bashiru akimtaja Camillius sio kufitinisha na kulisha maneno.
 
Marhaba.. Asante kwa ujumbe..

Take home
Acha demokrasia ichanue..
 
No comment.

DR BASHIRU usome kwa makini huu ujumbe ni mzuri na utakujenga. Acha habari za UHALISI na NYEMELEZI
 
Sema Tumbo na Ubinafsi ni kitu kingine ushauri safi kbs lkn cha Ajabu na ww ukipewa nafasi utafanya hayo hayo anayofanya Kaka yngu Dk Bushir embu turudi kwa Dk Rioba yule TBC vp khs Prof Mkumbo...
Sijakuelewa
 
Naomba nikushukuru kwa niaba yake Dr. Kweli kama atausoma ushauri huu najua kuna kitu kitamgusa. Nadhani huwa wanapewa rehearsal ya nini cha kuandika, kusema au kuwaza kabla hawajaweka sahihi kuwa wamekubali kuipokea hiyo nafasi.
Namkumbuka ndg Pole, Kitila, Slaa na Lipumba na sasa huyu Dr. Kabla hawajaitwa kula meza ya bwana, yaani tulitamani wawe ndio wakuu wa nchi hii. Lakini walipoitwa mezani pa bwana kula meza ya bwana tu. Ghafla wakawa viumbe wapya.
 
Wasifu wa membe unatisha

Kachero mbobezi
Rafiki wa papa
Kagera War planner
Mshauri wa nchi 5 kiusalama

Duh noma sana
 
THE DIFFERENCE IS THE SAME

Video imerekodiwa kumuonyesha R akimshauri B mwisho wa mwaka 2018. Alierekodi video ni shirika M ambao Ni marafiki Sana na B ambae anasemwa kwenye video.

Mwaka uliofuatia May 2019, Shirika M linaachia video kwa Public, Kesho yake B anajitokeza kujibu video ambayo alikuwa anajua ipo tangu mwisho wa mwaka 2018, anajibu anajifanya amepanic, ameumia sana

Alafu anatokea Kiongozi mkubwa wa chama KM anamjibu B.

Watu wanaibuka kushangilia kwamba Sasa B amepatikana, R amemtoa B mafichoni kilichobaki Ni kumponda kichwa afe.

HAIKO HIVYO.

Sisi tunaopenda kushirikisha akili zetu kwenye maamuzi tunaona picha tofauti kabisa, tunaona maigizo makubwa, yaani picha inaanza staring anakufa kwenye majani.

Picha yangu inanionesha kwamba R alitekodi ile video kwa maana Maalum kabisa, na B hakuijibu kwa wakati mpaka akamilishe Jambo ambalo alikuwa anapambana nalo Sana au mkakati aliokuwa anakamilisha, baada ya kuweka mambo sawa mwaka unaofuata Sasa ndo anajitokeza kujibu kwa kuumia na kupanic ili kuwapoteza wananchi.

Hayo Ni mawasiliano ya Hali ya juu Sana, inakuwa Kama ishara ya Jambo fulani kuanza au kuingia hatua inayofuata. Kuna codes nyingi Sana za mawasiliano.

Wajuvi wa mambo wanaona Kama R, B na KM wote ni sehemu Moja, wote ni watu wenye akili nyingi Sana, sio wa kupuuzwa kabisa. Kinachoonekana kwa watu wa kawaida ni maluelue na mazingaombwe tu.
Aisee

Gotcha you

We unadhan

Anayefuata pale white nyumba ni nan
 
hivi ni kweli membe anaweza kuwa rais 2020
ili swali ni swali ambalo mh. Membe angeulizwa hapa nadhani unapiga ramli. Pia kiufupi wakati wa uchaguzi bado ivo Fanya kazi kuinua kipato chako na uchumi wa taifa kwa nafasi yako. MH MEMBE aachwe na plan zake
 
Back
Top Bottom