Mie farkhina katika vyakula vilivyonishinda biriyani inachukua namba, nimekula mpaka ya wale wanaosifiwa kwamba ni Wataalam wa kupika biriyani lakini mhhhhh!!! Bokoboko sikujua kama ni mapishi rasmi ya chakula hicho nilidhani mpishi kakosea ndio maana chakula kikaitwa bokoboko, "leo Tamara mkono umeteleza katupikia bokoboko" Nimejifunza kitu leo.
Hahahahaha sasa biriani imekushindia nini? Labda nkupikie yangu pengine utaipenda lol
Kuna mapishi rasmin yanaitwa bokoboko...very healthy
Nipe mlango ninakuja sasa hivi kuila Bokoboko muache BAK apoteze wakati.
Hata sijui rafiki na si mimi tu nawafahamu watu wengi tu ukiweka biriyani, pilau na ubwabwa lol!!! basi biriyani ndio itayoguswa na wachache zaidi ukilinganisha na hivyo vingine. Mie nikapata ugali na samaki ya kukaanga na mchicha pembeni na pilipili ya kumwaga basi roho nyeupee lol!!! 🙂🙂
Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.
Dr kula kwa watu tabia mbaya. Hujafunzwa kwenu? Lol
Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.
Wali bondo? Means wa maji mengi?
Ukiwa hujauzoea mchele au kwa first time kupika kwa vile hujui kiwango cha maji kiasi gani unahitaji...pendelea kuuchemsha kwa maji mengi kidogo ukikaribia kuiva uchuje alafu ukaushe utaendelea kuwiva kwa mvuke...
Mmmh. Sasa nikishachuja utamu utatoka wapi? Hahaha.
Yaani nasema mie sijui kupika bokoboko. Manake mchele nisioujua naweka maji kidogo tu. Ila kuna mtu ananiambia yeye apenda bokoboko. Na mie huwa sili bokoboko.