Boko mnemela na majanga ya maji

Boko mnemela na majanga ya maji

Ndikita

New Member
Joined
Apr 25, 2016
Posts
4
Reaction score
4
ilikuwa January 2019 tulipata ugeni kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha, tukajulishwa kupitia Mwenyekiti wa kijiji na wenyeviti wa Vitongoji, taarifa ilihusu wananchi kujitokeza kwenye mkutano wa Kijiji, tulihudhuria!!

miongoni mwa agenda zilizotajwa kikakoni, agenda kuu ilihusu wananchi kuunganishiwa huduma ya maji kwa mkopo. hiyo ilipita. (sitazungumzia agenda zingine) Baada ya muda fulani kupita hatimaye tukaletewa form na kuzijaza kulinga na vingezo tukapata huduma tukawa tukipata maji kwa masaa 24!! that was absolutely amazing!! tuliipata hiyo huduma ya maji hadi mwaka 2021 mwezi wa tatu (MARCH) mara tu baada ya kifo cha Hayati Rais JPM hazikupita siku nyingi, nakumbuka ilikuwa tarehe 22 au 23, hapo huduma ya maji ilipotea ghafla. Maji ikawa ni anasa!! Watu wa Dawasco Kibaha wakiulizwa wanapita huku wanatokea kule, Diwani akiulizwa hajui, Mwenyekiti na Wenyeviti wa Vitongiji wakawa wanateseka pamoja nasi kwa kutumia maji ya madimbwi. Maji yalipotea tangu 2021 hadi leo 2024.

(MAJI YAMEKATWA KWA MIAKA MITATU MTAWALIA) Sijawahi kuona nahisi msomaji unaweza usielewe, ngoja niweke vizuri. Naongelea kijiji ambacho kimepelekewa bomba la maji ambapo wataalamu wa maji walifanya utafiti, tahmini na idhini ikapitishwa.

Wakati huu tukiwa katika harakati za uchaguzi wa serikali za mitaa maji yanatoka usiku wa manane kwa masaa kadhaa na baadhi ya sehemu. Najiuliza sana tatizo ni nini?? tumewakosea wapi?? Mtu yeyote mwenye Connection na Waziri Aweso am-tag apate hii habari. (yumkini anjua) Watu wanateseka sana wanatumia maji ya madimbwi ambayo maji ya mvua yametuwama kwa muda mrefu (MALAMBO), au mashimo yaliyoachwa baada ya machimbo ya mchanga na maji kutuwama nadani yake.
Wasaalam.
 
Back
Top Bottom