Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,915
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Bodi hiyo inapinga taarifa zinazosambazwa ambazo pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma na kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Jerry Sabi amesema taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wadau wote wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Amesema baada ya kukamilika kwa taratibu, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz).
Chanzo:Mwananchi online