Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ina Walakini

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ina Walakini

Sophist

Platinum Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
4,486
Reaction score
3,411
Imported from a FB Friend
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUNA WALAKINI
Tunaweza kusema kuwa ni upungufu wa kawaida tuliouzoea miongoni mwa viongozi, maofisa na watendaji wa serikali. Tunaweza kusema ni upungufu katika wizara ya elimu, teknolojia na ufundi. Tunaweza kupigia mstari mahali popote kuonesha upungufu wa serikali kusimamia na kuendesha elimu ya juu, teknolojia na ufundi nchini. Hata hivyo mimi ninaelekeza maoni yangu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Katika gazeti la Mwananchi (uk.3), la leo Oktoba 31 kuna habari inayowanukuu watendaji wa Bodi ya Mikopo kuwa na mipango ya kupitia upya (review) na pengine kubatilisha mikopo iliyokwishatolewa kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo. Haya yanaweza kuwa maamuzi ya hovyo kabisa kuwahi kutolewa na Bodi ya Mikopo.

Kwa kuwa sitaki kuchagiza wadau, ninashauri kabla ya kuchangia maoni, tafadhali someni hiyo habari halafu tuweze kujadiliana.
Kwa maoni yangu ya awali, hii menejimenti ya Bodi ya Mikopo ni zero kabisa. Haina uwezo hata kidogo kuishauri serikali na taifa kufikia malengo yanayokusudiwa. The HESLB management is grossly incompetent.

Juzi juzi tu watendaji wa Bodi waliwataka wanafunzi walioomba mikopo wapeleke nyaraka ambazo awali hawakuwa wameziorodhesha katika form za maombi ya mikopo.

Vigezo walivyoviweka kubaini na kutambua wahitaji wa mikopo siyo vya kitaalam bali hisia. Badala ya kusisitiza academic competence kwa wahitaji wa mikopo, bodi inaleta hisia kuwa wanafunzi wakisoma shule za sekondari za binafsi inabainisha (automation) uwezo wao kujigharimia elimu ya Chuo Kikuu. Hii ni dhana ya ajabu kabisa. Hukuna kigezo cha kisayansi hapo isipokuwa hisia kuonesha kuwa Bodi inawaonea huruma wanafunzi waliosoma shule za sekondari za serikali/umma. Kuna masuala mengi ya kujadili kuhusiana na kigezo hiki butu (crude/rudimental thinking of stone age) cha Bodi ya Mikopo. Elimu ya juu siyo mali binafsi; ni rasilmali ya umma inayotakiwa kugharimiwa na umma. Comptetent humanware ni primary goal kwa taifa kufikia maendeleo. Sasa kwa nini maendeleo ya umma/taifa yagharimiwe na watu binafsi tu badala ya serikali?

Lakini pia, nchi haiwezi kuendeshwa kwa sera za kibaguzi. Kwamba serikali itoe mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi waliosoma shule inazomiliki peke yake, wakati elimu katika ujumla wake hapa nchini, shule za umma na binafsi sawia, husimamiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Hii haikubaliki hata kigogo. Serikali inawajibika kuhakikisha shule za umma na zile zinazomilikiwa na waendeshaji binafsi zinatoa elimu bora. Hapa kuna masuala mengi ya mjadala wa maendeleo pia.

Wanafunzi waliopata elimu bora katika shule za umma na binafsi waachiwe washindane kupitia ufaulu wa mitihani kisha wapewe mikopo kuendelea na elimu ya juu siyo upendeleo mwingine. Ni wasomi mahiri tu watakao liwezesha taifa hili kufika kilele cha maendeleo. Bodi ya Mikopo inatakiwa kuacha uswahili na kuishauri serikali ipaswavyo – bila kupepesa macho!

Sote tunajua kuwa wizi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio chanzo cha kuporomoka kwa shule za umma/serikali. Kinachoitwa vigezo vya Bodi ya Mikopo vinavyobadilika badilika kila wakati, hakiwezi kurejesha umahiri wa kitaaluma katika shule za umma. Hapa kuna mfano hai. Shule ya sekondari ya Azania nilikosoma mimi darasa letu (wanafunzi 35) la form four commerce (1985) sote tulichaguliwa kwenda kidato cha tano isipokuwa mwanafunzi mmoja (ingawa naye alifaulu daraja la 3). Hali ilikuwa hivyo kwa wanafunzi waliokuwa madarasa ya Sayansi I-IV. Ninawakumbuka akina Arch. Honest Kahumba, Eng. Feruzi Uddy, Dr. Alex Baluhi (yuko Rusia) na wengineo. Tulifundishwa, kujisomea na kuwa mahiri kitaaluma katika shule ya umma/serikali – kigezo kikuu kilichotumika kutuwezesha kuendelea na elimu ya juu/Chuo Kikuu.

Ufukara wa wazazi wetu haukutumika kamwe kuamua utaratibu wa kugharimia elimu ya juu. Sote tunajua kuwa serikali haikuwekeza tena shule ya Azania. Katika matokeo ya mitihani ya kidato cha IV/2015 yaliyotoka Machi mwaka huu, shule ya Azania ile ile ni miongoni mwa shule 10 za mwisho kwa ufaulu kitaifa. Hapa sera sahii inayotakiwa si kupendelea wanafunzi waliosoma shule ya Azania kupata mikopo ya elimu ya juu bali kuwekeza ili Azania irudie miaka ile ya akina Hashim Mroso, Hussein Ali Hassan Mwinyi, Hassan Hassan, Kamuhanda Tibesigwa, Benjamin Mchwampaka na wengineo.

Hadi sasa tunaweza kusema kisayansi [hapa nchini kwetu] kuwa kigezo kikuu kitaaluma kwa mwanafunzi kuendelea na elimu ya juu ni ufaulu wa mitihani kiwango kinachotakiwa, basi. Baada ya kukidhi kigezo hicho mamlaka husika inaweza kuanza kuangalia vipaumbele (variables) vya maendeleo kama mahitaji ya humanware ambavyo hubadilika kila wakati. Vipaumbele hivi vinatakiwa viashiriwe kisayansi, vitangazwe, vijulikane na kuoanishwa na maudhui ya elimu inayotolewa mashuleni katika vipindi vya muda wa kati au muda mrefu. Bodi haipashwi, muda mfupi kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo, kuleta vitu vya kufikirika na kuviita viapaumbele vya mikopo. Hii haikubaliki!

Nina mashaka iwapo calibre hii ninayoiona ikisimamia Bodi ya Mikopo inaweza kuishauri serikali kufikia malengo ya maendeleo ya taifa hili, zaidi mapendekezo ya posho na mishahara ya watendaji.

Lakini kama fununu nilizopata mwaka juzi kuwa Bodi ya Mikopo inatuma pesa zaidi kujiendesha (administrative cost) badala ya kutoa mikopo kwa wanafunzi (core business) ni sahihi (sina sababu ya kutoamini hivyo), tunaweza kuona chanzo cha incompetence ya HESLB. Inashangaza zaidi kuona Bodi ya Mikopo ya wanafunzi inawekeza kujenga jengo la (limejengwa pale Mwenge, DSM) badala yak u-maximize utoaji mikopo. Kitaalam, Bodi ya Mikopo inayotambua core business yake haihitaji kumiliki jengo wala kuwa na lundo wa wafanyakazi – maofisa na kacheku sawia. Muundo na mfumo wa uendeshaji Bodi ya Mikopo unahitaji mjadala mpana pia.

Tusipokuwa makini na kufanya prompt intervention, kinachoonekana kuwa ni vigezo vya Bodi ya Mikopo kutekeleza mipango/mikakati yake kinaweza kuwa mbegu ya ubaguzi katika taifa hili linalohitaji kuendeleza umoja na umahiri kitaaluma na kiutaalam.
 
waanze kuwasaka mijizi ya Dowans, Epa, Richmond then ndo wafuatilie ya heslb
 
Back
Top Bottom