martial jb
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 864
- 1,464
Habari wakuu
Kila mwaka serikali inatenga bajeti maalum kwa ajili ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kupitia taasisi yao(HESLB) ambapo kila mwaka wanafunzi si chini ya 150,000 wanakuwa wakinufaika na mikopo hiyo.
Bila ubishi mikopo ya elimu ya juu imeanza kuwa changamoto kwa wanufaika wa mwaka wa masomo 2021/2022, hii inatokana na mikopo hii kutokidhi vigezo vya walengwa au wanufaika, nadhani hili halina ubishi kwani mwaka huo wanafunzi wengi nchini wamekuwa wakilalamikia mikopo hiyo na hata idadi ya waliofanya appeal nadhani ilikuwa kubwa tu!
Ajabu sijaona mabadiliko yeyote makubwa na yenye tija yaliofanywa katika bajeti ya mwaka 2022/2023 ya mkopo kutokana na malalamiko hayo zaidi ya kuongezeka kwa bilioni 3 ( kutoka bilioni 570 kwenda 573 )
hii inamaanisha malalamiko ya wanafunzi hao hayakupewa kipaumbele chochote.
Mbali na hilo hii sera yenu ya mikopo kwa wanafunzi wote naona kama haina tija, ni sawa na kumwaga mtama kwenye kuku wengi, kwani toka awali mikopo ilikuw ikipewa kipaumbele kwa wanafunzi wa hali ya chini ambao wengi waliangaliwa wale waliosoma shule za kata na wale waliojikita na masomo ya sayansi, hii ilisaidia na ilipunguza malalamiko kwa mikopo hiyo kwani ilienda kwa wahitaji.
Serikali inapaswa kufahamu kuwa ni kundi kubwa la wanafunzi wa hali ya chini linaloshindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu, kutokana na mikopo duni inayotolewa kwa wanafunzi, naomba hili suala liangaliwe sana maana ishakuwa changamoto kubwa.