Bodi ya Mikopo kuwakopesha waliopitishwa TCU, NACTE

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL), imesema kuwa itatoa mikopo kwa wanafunzi wenye udahili ulioidhinishwa na Kamisheni ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE) na kufuata mwongozo wa serikali wa mwaka 2008/2009.

Taarifa ya bodi inafuatia baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IMF) na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM) kuandamana hadi ofisi za bodi wakishinikiza, pamoja na mambo mengine, kwamba bodi ilipe ongezeko la ada katika vyuo hivyo.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, George Nyatenga, bodi haitatoa hata senti tano nje ya viwango vilivyowekwa na serikali.

“Katika mwongozo tulioutoa kabla ya kuanza kutoa fomu za kuomba mikopo kwa mwaka 2010/2011 tulifafanua kuhusu ada kwamba kutokana na ongezeko la mahitaji ya mikopo ya wanafunzi ikilinganishwa na ufinyu wa bajeti, HESLB itaendelea kutumia viwango vya ada ya mwaka wa masomo 2008/2009 kwa mwaka mpya wa masomo kwa waombaji wapya na wale wanaoendelea na masomo hadi hapo serikali itakapoamua vinginevyo.

“Hivyo hatua ya wanafunzi kuandamana haitasaidia kitu chochote na wala bodi haitatoa hata senti tano nje ya viwango vilivyoelekezwa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imeendelea kueleza: “Pamoja na maelekezo ya serikali yaliyowasilishwa na ya Elimu na Mafunzo kwa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ya kutopandisha ada, baadhi ya vyuo vimekaidi agizo hilo na vimewapandishia ada maradufu na kisha kuwasukuma wanafunzi wao kuja bodi ya mikopo kudai nyongeza za ada hiyo, badala ya kuwadai wanafunzi wao.

Vyuo hivyo vinafanya makusudi kwa sababu ya urahisi wa kudai nyongeza hiyo kutoka bodi au serikali kuliko kuwadai wanafunzi.”

Kuhusu wanafunzi waliodahiliwa chuo zaidi ya kimoja, taarifa hiyo imesema Bodi haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye udahili katika zaidi ya chuo kimoja na imewataka wanafunzi wenye tatizo hilo kuwasiliana na TCU.

Aidha, taarifa hiyo inasema kwa wanafunzi waliohama vyuo walivyopangiwa na TCU awali, kusubiri hadi fedha zao za mikopo zirudishwe na vyuo hivyo ndipo bodi iweze kuzielekeza huko walikohamia sasa.

Katika hatua nyingi, Bodi haitatoa mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao Bodi haijapokea matokeo yao ya mitihani kwa mwaka wa masomo uliopita na kuwataka
wanafunzi husika kufuatilia na vyuo kupeleka matokeo ili kuondoa usumbufu kwa bodi.
 
Mimi naona ili suala la mikopo ya wanafunzi alijachunguzwa kwa makini. Kwanza iki kigezo cha kuunganisha utoaji wa mkopo na ufaulu wa mwanafunzi katika mtihani wa kidato cha sita siyo tu cha upumbavu bali kinaonyesha ubinafsi uliokidhiri. Ni cha upumbavu kwasababu mikopo haipashwi kutolewa kama tuzo ya ufaulu. Mikopo inapashwa itolewe kwa wale wanafunzi waliofanikiwa kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu lakini kutokana na hali duni kiuchumu yao wenyewe na wazazi/walezi wao hawana uwezo wa kumudu gharama husika. Hivyo suala hapa si mwanafunzi huyo amefaulu kwa kiwango gani bali ni je amefanikiwa kupata nafasi katika vyuo husika. Ni ubinafsi kwasababu sote tunajua vijana wengi wanaofaulu katika daraja la kwanza na la pili wanatokea kwenye shule binafsi zinazotoza karo ya mamilioni ya fedha. Hivyo wengi wa wanafunzi hao wanaweza kumudu kujilipia bila mkopo. Ufumbuzi wa matatizo yote haya ni kutoa mkopo kwa asili mia kwa kila mwanafunzi anayeitaji mkopo.Jambo hili linawezekana iwapo serikali itajiepusha na anasa na kukusanya madeni sugu kutoka kwa vigogo na wanafunzi waliokwisha maliza masomo yao.
 
Back
Top Bottom