MsamiKowalski
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 285
- 53
BW Hamis Chagonja.
Zaidi ya wanafunzi 52,000 wa mwaka wa kwanza watanufaika na mkopo wa elimu ya juu baada ya serikali kuongeza kiasi cha fedha sh 132 bilioni kwaajili ya kugharamia masomo yao ya mwaka wa masomo 2015/2016.
Akizungumza na gazeti la MWANANCHI, kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu(HESLB), Bw Hamis Chagonja alisema bajeti ya sh 341 bilioni ilikua imepangwa kwaajili ya wanafunzi 14,226 wa mwaka wa kwanza.
Hata hivyo, alisema serikali imeongeza fedha hizo hadi kufikia sh 473 bilioni ambazo zinatosha kuwalipa wanafunzi 52,000. Alisema ongezeko hilo litawezasha wanafunzi wengine 37,774 ambao hawakuwapo kwenye bajeti kudhaminiwa na bodi ya mikopo mwaka huu.
"Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni 71,125 hatuna shida nao sana, wao wataweza kupata fedha hizo. Changamoto ilikuwa kwa hawa mwaka wa kwanza,lakini sasa tumepata fedha za kuwalipa" alisema Bw Hamisi Chagonja.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi 8/12/2015.