TangataUnyakeWasu
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 1,268
- 1,587
Kuanzia January Mosi 2017 bodi ya mikopo inakusudia kuchapisha sura za wadaiwa SUGU waliojinufaisha na mkopo wa Elimu ya juu.
BODI YA MIKOPO KUFANYA MSAKO WAAJIRI SUGU WOTE NCHINI WASIOWASILISHA MAKATO NA MAJINA YA WANUFAIKAJI
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru ameunda kikosi maalumu (Task force) kwa ajili ya msako wa kuwanasa waajiri sugu wote nchini wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo ya bodi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Badru amesema kikosi kazi hicho kitaanza kazi Januari 2, mwaka 2017 na kitafanya kazi hiyo kwa siku 14 mfululizo wakipita ofisi moja baada ya nyingine.
Chanzo: Mwananchi