Bodi ya mikopo imeshindwa kukusanya fedha kwa wadaiwa au inaihujumu serikali?

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kwa elimu yangu ndogo tu ya diploma ya Uongozi ninauwezo wa kuifanya bodi ya mkopo ianze kupokea asilimia 100 ya watumishi wa serikali na angalau 70 ya waajiliwa binafsi.

Kwanza ningetoa wiki mbili tu kwa wadaiwa waajiliwa wa serikali kujisalimisha kwa maafisa utumishi na wasipofanya hivyo wangejivua kwenye utumishi wa umma kwa kosa la kutokuwa waaminifu na kuihujumu serikali. Mbona ajira za sayansi mmeomba vyeti kwa wiki moja tu mkavipata.

Ni aibu sana kwa bodi ya mikopo kuendelea kuwadai watumishi wa uma wenye miaka mingi kazini na kushindwa kujua walipo.

Ndani ya wiki moja watumishi wote wenye shahada lazima ningewajua na wangeanza kukatwa. Kama taasisi za kukopesha zinapitia kwa afsa utumishi basi kupitia maafisa utumishi ningewatambua wawjiliwa wenye shahada ya kwanza nakupata uhakika kama wamekopa na kuanza kuwakata lazima
waajiliwa wa kampuni binafsi na waliojiajili wangetakiwa kujisalimisha kwa afsa elimu mojawapo wilayani (kuna maafisa wengi wasio na kazi kama afsa elimu sayansi kimu)na kuorozeshwa sehemu walipo na kujua kama wanaweza kulipa au la, kama wanauwezo wa kulipa waanze kulipa na kama anauwezo na anachenga kulipa atakamatiwa vitu vyao kama nyumba na magari.

Na ambae hatajisalisha na anadaiwa sheria iwepo ya kuwalazisha kulipa kwa mkupuo moja na riba ya 20% la sivyo vitu vyake vipigwe mnada kulipa fedha hizo.

Kuwapata wadaiwa wanaojificha au kudanganya taarifa zao ni kwamba taarifa za wadaiwa ambao hawaanza kulipa walipo na shuguli wafanyazo zitakuwa wazi ili ambaye kadanganya akitokea mtanzania atakaeisaidia bodi kumpata na kupata taarifa zake sahihi atapewa zawadi ya 150,000/- au asilimia 2 ya deni analodaiwa mdaiwa na hiyo fedha yote italipwa na mdaiwa punde atakapokamatwa.

Natamani wadogo zangu wasikose mikopo ila bodi naona kama inahiujumu serikali. Rais niteue mimi na diploma yangu nikusaidie kuiongoza bodi. Naona bodi inarukaruka na mikwala kwenye midia ila utekelezaji hakuna
 
Back
Top Bottom