sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,000
Salaam Wana jukwaa.
Naomba niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu. Mdogo wangu alibahatika kuchaguliwa kusoma shahada ya kwanza katika moja ya campus za chuo kikuu Cha Dar es salaam(UDSM), na kufanikiwa kupata mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
Kijana huyu alipata changamoto ya ugonjwa ambapo ilibidi asimamishe kuendelea na masomo ili akapatiwe matibabu,na kwa uwezo wa Mungu alipata nafuu ambapo alirudi chuoni kuendelea na masomo mwezi Machi mwaka huu.
Tangu arudi chuoni danadana zimekuwa nyingi sana kuhusiana nakurudishwa Kwenye system ya mkopo. Dogo anatoka familia duni hivyo tangu mwezi Machi anatunzwa na wanachuo wenzake ambao nao wanatengemea boom.
Ombi langu kwa bodi, jitahidini kufanyia kazi changamoto za huyu/Hawa vijana kwani wengi wao hawana chaguo lingine.