Bodi ya mikopo elimu ya juu kuwanyima mikopo waliyosoma private sio sawa huo mkopo ni haki ya Kila kijana wa kitanzania

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,701
3,090
Serikali inatakiwa imshukuru mzazi ambaye amemsomesha Mtoto wake private kuanzia darasa la kwanza hedi kidato Cha sita kwa sababu ameisaidia serikali ukweli ni kwamba watanzania wote wakipeleka watoto wao shule za serikali madarasa yaliopo na resources zingine hazitatosha Sasa badala yakupewa zawadi huyu mzazi anakuja kuadhibiwa kwa kunyimwa mkopo Mtoto wake

Vipato vya watanzania vinafanana mtiririko wake huwa vinashuka kadiri umri unapoenda Kuna uwezokano mkubwa hadi Mtoto anamaliza kidato Cha sita mzazi unakuwa umesha yumba kiuchumi na ndio maana Hawa watoto wanapoteza ndoto zao za kupata elimu ya juu

Hizo pesa za mkopo wa elimu ya juu ni haki ya Kila kijana wa kitanzania na hata huyu mzazi aliyesomesha Mtoto wake private pia michango yake ipo katika hiyo pesa ya mkopo kwa sababu analipa kodi Sasa iweje azuiliwe kufaidi matunda ya Kodi yake aliyekuwa anakatwa

Elimu ya juu sio jukumu tena la mzazi ila ni jukumu la mtoto na ndio maana huo mkopo hakopeshwa mzazi ila anakoposhwa Mtoto kwa hiyo kunyima mkopo Mtoto kwa kusa alilofanya mzazi wake la kumsomesha private school sio sawa

Lakini pia cream nyingi zitapotea katika fani mbali mbali ukweli ni kwamba aliyesoma kayumba kuanzia darasa la kwanza hadi kidato Cha sita na aliyesoma private kuanzia darasa la kwanza hedi kidato Cha sita wanapokutana chuo hawawi sawa na ukitaka kulijua hili kama uliwahi kusimamia interview Kuna tofauti kubwa kati ya waliosoma kayumba na private school hata ukipinga huo ndio ukweli

Pia kama huyu kijana atafanikiwa kupata elimu ya chuo kwa msaada wa baba yake atakuwa hana uzalendo na nchi yake kwa sababu anakuwa amefika hapo alipofika kwa msaada wa baba yake na si serikali yake tena akiwa na kumbukumbu kwamba serikali ilimnyima mkopo
 
Umeongea ukweli sana tegemea mawe mazito kutoka kwa waimbaji wa kaupiga mwingi.

Ubaguzi wa huyu katoka familia gani au kasoma familia gani haupaswi kuwepo.

Pili mikopo mingi ya bodi ya mikopo hailipiki pia kwa sababu wanaokopeshwa ni pamoja na zile familia duni sasa watoto hao wapatapo kazi wanawajibika kuzilea familia zao kuliko kulipa mikopo.
 
Ni vizuri ukaweka hoja kuwa swala la Kupata mkopo chuo kikuu pasiwepo siasa . zozote.
 
Back
Top Bottom