kimaus
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 582
- 707
Mi ni mnufaika wa mkopo wa Elimu ya juu toka HESLB na nilimaliza chuo cha umma mwaka 2011 kwa kozi ya miaka mitatu hapa nchini. Tuition fee ilikuwa around 1.2m kwa mwaka, meal na accommodation allowance ilikuwa Tsh 5000 kwa siku maana yake ni 150k kwa mwezi na 600k kwa Semester sawa na 3.6m kwa miaka mitatu. Mafunzo kwa vitendo ni 10k kwa siku sawa 560k kwa siku 56 za mwaka wa kwanza na 560k kwa mwaka wa pili. Na research project pamoja na special faculty requirements hazifiki hata 1m kwa miaka mitatu yote. Ukipiga mahesabu hapo utapata less than 9m. Sasa nimeanza kukatwa mwaka jana mwishoni na deni kwenye Salary slip so far ni zaidi ya 19m! Tafadhali anayejua sababu ha hii au Loan board watueleze, hata kama ni penalty ndio izidi hata deni lenyewe?