Bodi ya Kampuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi ya Kampuni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by iMind, Jan 22, 2012.

 1. i

  iMind JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Wandugu, naomba mwenye uelewa hili hili swala anijuze. Nafahamu mashirika ya umma na taasisi mbali mbali za umma huwa na kitu kinaitwa Bodi ya wakurugenzi, ambao huteuliwa na Waziri husika na Mwenyekiti wa Board huteuliwa na Raisi. Hilo halina tatizo kwangu. Shida yangu iko kwenye kampuni binafsi. Je board members ni lazima wawe wanahisa. Kama siyo wanahisa wanalipwaje? Na kazi zao hasa ni zipi?

  Nauliza hivi kwa sababu nafikiria kuunda bodi ya kikampuni changu. Hiki kikampuni tulianzisha na mke wangu, sasa kimeanza kunona kidogo na naona ni wakati muafaka kuwa na kitu kama board na kujaribu kukiendesha kama taasisi ili hata kama mimi au mke wangu hayupo, mambo yaendelee kama kawaida. Je nianzie wapi kuunda hiyo bodi, na vigezo gani nitumie kuchagua wajumbe na mweyeketi? Je ni lazima hiyo board iwe inalipwa mshahara au tunagawana faida? Tafadhali naomba mnijuze.
   
 2. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Höngera mjasiriamali wangu, Nami nasubir majib ya wataalam hapa!
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapa tunatatizo, majibu yote hayo ulitakiwa utupe wewe.
  Iko hivi, kabla ya usajili wa kampun kunamchakato wa kutengeneza memarts (yaan memorandum and articles of association). Sasa kwenye articles of association ya kampuni kuna vifungu vinavyoelezea kuhusu Directors, Idadi yao, wanavyopatikana, wanavyolipwa, utendaji kazi wao na wanavyofukuzwa. Isome utapata majibu, tatizo ninaloliona ni kwamba Memarts nyingi zimeandikwa kwa kingereza na si kweli kwamba wamiliki wote wa makampuni Tanzania wanajua lugha hiyo.

  Kimsingi kuna wale Directors ambao ni waanzilishi ambao si lazima wawe na shares (hawa huchaguliwa na subscribers wa kwanza but mara nyingi hujichagua wenyewe wenye hisa- si unajua suala la hela halafu kampuni mpya) na kwa case yako ni wewe na mkeo. Sasa kama mlishawakaribisha subscribers wengine itabidi mkae kama mkutano mkuu (AGM) ili mteue hao members wengine kuwa Directors. Swali ni wangapi waoruhusiwa kisheria- Jibu lipo kwenye memarts yako. Ambacho ninaweza kukuambia kwa sasa ni kwamba LLC haiwezi kuwa na subscribers zaidi ya hamsini (50)

  Katika subscribers ndio inapatikana Board of Directors kwa kuchaguliwa na mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM). Lakini ni vizuri ukijua kuwa kadri BODI inavyokuwa kubwa ndivyo gharama za uendeshaji zitakavyozidi. Kumbuka katika kila kikao cha Kampuni lazima mje na Board Resolution (kimaandishi zaidi) na inakuwa signed

  Ngoja nikupe mfano wa hiyo provision

   
 4. i

  iMind JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Mkuu Enterprenur asante kwa ufafanuzi. Memarts yetu inasema madirector hawatapungua 2 ingawa haiweki ukomo. pia inasema kuwa remuneration za directors zitaamuliwa na AGM. Nilitaka kujua best practise, kwanza ya kuwakaribisha hao maderectors na namna ya kuwalipa, na kuhakikisha wanasaidia kampuni. Thanks
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Minimum number of membership for a private company is two and maximum is fifty (hii ni kisheria zaidi). Cheki hapa BRELA, halafu uende kipende (a). Lakini kuna regulation ya mwaka 2008 inayoruhusu Single share holding kwenye LLC (ila sidhani kama BRELA wameshaanza kutumia).

  Sasa turudi kwenye mzizi wa fitina

  Hili somo ni refu kidogo itabidi tena turudi kwenye authorised shares an issued shares. Kifupi ni kwamba Private companies are normally formed by persons with prior relationships e.g. Father and son's and or daughters, friends, business partners etc. Kwa hiyo unaweza ukaangalia watu walioko kwenye network yako (yaweza kuwa ndugu, marafiki au business partners) kisha ukawakaribisha wawe subscribers (kumbuka, itabidi nao wachangaie mtaji) halaf kwenye AGM ndio mnachagua Directors, majukumu na malipo mtakubaliana huko kwenye AGM.

  Kumbuka huu mchakato unaenda sambamba na na kuupdate company file pale BRELA ili liendane na wakati. Vilevile suala la kukusanya fedha kutoka kwa wanahisa wapya lazima liendane na Authorised Shares. ( Yaani huwezi kukusanya mitaji ukazidi kile kiwango kilichoruhusiwa wakati unasajili kampuni. Kitu kizuri ni kwamba hizo Memarts sio msahafu au Biblia, unaweza ukaufanyia mabadiliko na kuongeza hicho kiasi cha Mtaji.

  Mkishachagua Directors kwenye AGM, itabidi wajaze form zipo hapa kisha mnazipeleka kwa registrar ili watambuliwe kisheria
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama ENTREPRENERS alivyo kijibu hapo juu ni sahihi kabisa, ila nataka kuongezea vitu vichache.

  Kuna aina mbili za kampuni mkuu.

  1. Private company

  2. Public company

  3. PARASTATOR (mashirika ya umma)

  Mashirika ya uma(PARASTATORY) muundo wake ni tofauti na kampuni binafisi, haya mashirika yana madirecter ila si waamuzi wakuu kwa sababu hili ni shilika la nchi,
  Ndo maana waziri huteua bodi ya wakurugenzi ili wawe wanafanya maamuzi mbalimbali ya shirika tena hata wao hawawezi fanya maamuzi bila kushauriana na waziri husika au raisi wa nchi, SO MASHIRIKA YA UMA SI MAKAMPUNI MKUU HAYA MEET VIGEZO VYA KUITWA MAKAMPUNI

  PUBLIC COMPANY

  MAKAMPUNI KAMA CRDB, NMB, TBL NA KAZALIKA HAYA YANAITWA PUBLIC COMPANY KUTOKANA NA KUWA NA WANAHISA WENGI SANA NA YAMEJIORODHESHA KWENYE SOKO LA HISA.

  Moja ya mashariti ya kuorodheshwa kwenye soko la hisa ni lazima kampuni yako iwe public company, kwamba kila mtu anaweza kuwa na umiliki wa hiyo kampuni, so makampuni yote yaliyoko kwenye soko la hisa ni PUBLIC COMPANY

  Pamoja na kuwa public company kuna wale wamiliki halisi wa kampuni, MFANO:
  TBL NI PUBLIC COMPANY BUT wale makabulu wa south africa ndo wenye usemi wa mwisho kutokana na kuwa na share nyingi sana na hawa huwa na uwezo wa kumteua Mkurugenzi mkuu wa TBL ila wanahisa wengine wanaishia kumteua MWENYEKITI WA BODO,

  - That is why MWENYEKITI WA BODI YA TBL NI MSUYA but MKURUGENZI MTENDAJI NI KABULU WA SOUTH AFRICA.

  BACK TO THE TOPIC

  Mkuu sijajua kama unampango wa kujiorodhesha kwenye soko la hisa au la make kama kampuni yako ni ndogo hakuna haja ya kuwa na wakurugenzi wengi, ni mzigo mkuu, wakurugenzi wengi ni kwa kampuni kubwa kama ilivyo TBL NA KAZALIKA

  ANGALIZO

  1. Mkuu unapo ongeza wakurugenzi kwenye kampuni yako hakikisha wewe unamiliki nusu ya hisa za kampuni ili kulinda aidia/wazo lako

  MFANO:
  -Kampuni huwa na share za asilimia 100% so hakikisha weweunamiliki asilimia 51% ya hisa zote,

  KWA NINI HIVYO?

  Mkuu mkigawana hisa let is say

  ukawa na asilimia 30%
  mke wako 20%
  mwingine 5%
  mwingine 10%
  mwingine 5%
  mwingine 5%
  mwingine 10%
  mwingine 5%
  mwingine 10%

  HAPA WEWE UTAONEKANA UNAHISA NYINGI NA UTAKUWA NA FINAL SAY KWENYE KAMPUNI KULINGANA MY B NA MEMO, ILA IKITOKEA UGONVI WA KIMASILAHI NA KIMTAZAMO HAWA WENGINE WANAWEZA UNGANISHA HISA ZAO NA KUMPA MMOJA NA AKAWA NA LETS SAY 50 AU 60 TIYALI HAPA ITAKUWA IMEKULA KWAKO MILELE.

  - SO HAKIKISHA WEWE UWE NA 51% YA HISA NA HIZO 49% NDO WAGAWANE HAO WENGINE, HAPA HAWAWEZI KUKUPINDUA
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Komando umegusia suala la msingi sana, hasa kwenye upande wa decision making (kudos). Cha msingi kama utashindwa kumiliki hiyo 51% personally basi wewe na mkeo au na mwanao mmiliki hiyo asilimia. Now get to work and keep us posted
   
Loading...