GE2025 Bodaboda watakiwa kulinda Amani Ili kuendeleza shughuli zao kwa Uhuru na Ufanisi

GE2025 Bodaboda watakiwa kulinda Amani Ili kuendeleza shughuli zao kwa Uhuru na Ufanisi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kama mnavyowapa elimu hii kipindi cha uchaguzi kwa nguvu kubwa, basi mafanye hivyo pia kuwapa elimu ya usalama barabarani katika kufuata sheria.

Maana kila siku visa vya bodaboda kupata ajali vimekuwa vingi.
===================
Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wametakiwa kutunza na kuilinda amani iliyopo ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao kwa uhuru, ufanisi na kwa manufaa yao na ya familia zao.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chake Chake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Edward Emanuel Mutailuka, Oktoba 22, 2025, wakati wa utoaji wa elimu kwa madereva hao.

Mutailuka amesema kuwa, bodaboda ni kundi lenye ushawishi mkubwa katika jamii kwa kuwa liko karibu na wananchi, hivyo ni muhimu wakawa mabalozi wa amani na kamwe wasikubali kutumiwa au kutumika kwenye uhalifu.

Screenshot 2025-10-22 222017.png
Screenshot 2025-10-22 222029.png
Screenshot 2025-10-22 222040.png
 
Back
Top Bottom