Bodaboda mnawahi wapi?

Wewe kazi gani hulipwi mpaka upumuliwe kisogoni.Lema alikuwa sahihi bodaboda ni LAANA.
 
Ni hatari kwa Taifa. Mimi ninadhani pikipiki zipandishiwe ushuru mara nne ili ziwe ghali kama bajaji au zaidi ili kupunguza madhara kwa jamii.

Kabla ya Mchina kumwaga pikipiki nchini Mjapani ndiye alikuwa anaongoza kwa kuuza Yamaha kwa bei sawa na gari ndogo na kipindi hicho usafiri wa pikipiki uliheshimika kama wa gari.
 
Tatizo na serikali yenyewe ndiyo inapata unafuu kwa kiasi fulani. Maana hawa watoto wasingekuwa na shughuli za kufanya, wengi wao wangekuwa ni vibaka na wezi mtaani.

Mimi nashauri wangepewa semina za mara kwa mara ili wajitambue. Maana wengi wao wakishapata tu hesabu yao ya siku; basi kinachofuatia kuanzia hapo ni kuchezea tu mafuta, kunywa pombe na kuvuta bangi.

Ni bodaboda wachache sana ndiyo wana malengo. The rest ni vurugu tu mtaani.
 

Hiyo semina hawawezi kuelewa kwa sababu kitendo cha kuendesha pikipiki muda mrefu ni ulevi tosha.

Petroli inavuja kupitia mfuniko wa tenki na kuingia puani kisha kichwani na kuwalewesha ndiyo maana wengi wana wenge. Muda mwingi wamekaa kwenye pikipiki hata kama wamepaki.
 
Mr Devil 😂
 
Wewe mwenyewe hujui kwamba kamati ya waganga wanakupakua kila usiku
Unayeamini waganga wanaweza kukupakua usiku na mimi nayejua 100% hakuna watu kama hao hapa duniani ni nani mjinga?
 
Haha
 
Hv hawa jamaa kwa nini huwa wanang'oa hizo side mirrors? Cha ajabu na polisi wa usalama barabarani wanawatazama tu
Lakini kwenye gari Hata kama side mirror ina kreki ndogo tu faini
 
Unajuaje labda huyo msamaria mwema ni yeye ila hakupenda kujianika utambulisho wake?
Umeona kaficha namba ya gari?
Kwaiyo wewe huna usamaria wema uongo? Uliona kupakia huo mzoga kwenye hicho ki rahum chako kwamba kingeisha mafuta au unakuja kueleza unoko hapa,hata picha hujaweka....
 
Bodaboda wengi mama zao ni vijana.
Wao wakifa mama zao watapata mimba nyingine(replacement)
 
Serikali haiwezi fanya chochote kuhusu bodaboda, kwasababu haya yanayotokea ndio hasa serikali inachotaka.

Boda boda priority zao ni ;
1. Kupata hesabu
2. Kubeti
3. Pombe
4. Ulevi mwingine kama bangi
5. Mademu
6. Matumizi yasiyo ya msingi.

Hawafikirii maendeleo ya maisha yao au maisha yao ya baadae.

Mwisho kabisa, hawafikirii maendeleo ya taifa lao maana muda huo hawana na pia sio priority yao. Total mind distraction.

Hebu fikiria hawa boda boda wote wangekuwa hawana ajira, wako mitaani wanapigwa na njaa kali ya maisha, katiba mpya ingekua haijapatikana mpaka leo? njaa zingewafungua akili wangedai haki zao, hata mapinduzi wangefanya amini nakwambia, maana asilimia kubwa ya idadi ya watu Tanzania, ambao ni wapiga kura ni vijana.

Kwaiyo hapo serikali haitafanya lolote, na wataendelea kupagawa na kupoteza maisha tu, kwasababu hicho ndicho serikali inataka.

Huo ndio ukweli wenyewe.
 
Nabwanawake ndio wateja wao wakubwa, unakuta kidada kiko kwenye bodaboda kimetulia wala hakina habari, kinachart na simu mda wote kikiwa na uhakika kiko salama!! Boda ni usafiri hatarishi mda wote
 
Tatizo la bodaboda kule kupatia mara moja wanafikiri mara zote wataendelea kupatia
 
Unajuaje labda huyo msamaria mwema ni yeye ila hakupenda kujianika utambulisho wake?
Umeona kaficha namba ya gari?
Sie tunamfahamu huyo mwamba kwa post za majigambo na spika alizonazo,hawezi kukusaidia asijitangaze/asikutangaze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…