Bodaboda mnawahi wapi?

Kwaiyo wewe huna usamaria wema uongo? Uliona kupakia huo mzoga kwenye hicho ki rahum chako kwamba kingeisha mafuta au unakuja kueleza unoko hapa,hata picha hujaweka....
Jiepushe kuiga malimbukeni kwa kuanza sentensi na neno ''kwahiyo''. Halafu mbaya zaidi hata kuandika neno lenyewe wengi hawajui.
 
Kesi za boda boda mi nishamuachia Lucifer aendelee kuwavuna manake hawanaga akili hao utadhani wametengenezwa maabara

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Ni kweli. Utadhani wanatengenezwa maabara au wamepachikwa ubongo uliotengenzwa China ukaletwa na hawa wanunuzi wanaokwenda kununua bidhaa za bei ndogo.
 
Aliingizwa uvungun au?

Leo basi Bodaboda wengi wamekufa
Leo ni Mapinduzi; wacha waisindikize siku wajinga wale! Kuzaliwa na mara moja tu; na kufa vivyo hivyo. Linda sana uhai wako kuliko chochote ulindacho.
 
UMUGHAKA unaitwa utoe utetezi


Mkuu vijana wengi wanaoendesha Bodaboda ni kama huwa hawaelewi sheria na alama za Barabarani,hicho ndicho chanzo kikuu cha Ajali!

Wengi wao wamefanya hata ambao tunafuata sheria na alama za barabarani kuonekana wote ni walewale!
 
Tatizo kubwa ni ufahamu sahihi wa matumizi ya barabara. Tukitegemea wafuate elimu ya matumizi ya barabara kwa njia za kawaida (formal); tutaendelea kuwapoteza na kupoteza nguvu kazi na ustawi wa jamii kwa ujumla wake.
Napendekeza serikali iunde team ya kuwapatia elimu ya matumizi sahihi ya barabara; iwapitie vijiweni kwao, iwe karibu na viongozi wao wa vijiweni kwa kuwaelimisha wao ili nao wakawaelimishe wanachama wao(wapya na wazamani), kuwe na toolbox talk( kukumbushana usalama) angalau kila siku. Viifaa vyao vya usalama (helmet) zisitozwe kodi ili vipatikane kwa urahisi zaidi na kwa bei nafuu, wakipata elimu watatumia tu.
Police waondoe uadui nao kwani boda wengi ukimbia police (tigo) bila kuzingatia usalama wao.
Bodaboda ni, wadogo zetu, watoto zetu, majirani zetu,rafiki zetu, binadamu wenzetu etc, tunawahitaji kwa ustawi wa jamii, wanahitaji msaada, wasaidiwe
 
Chanzo cha hayo yooote ni pombe kali.....vijana tuache pombe.

Yaani unajijua kabisa kwamba wewe huwa unakuwa road masaa labda 15 kati ya 24 ya siku halafu unakunywa pombe wakati huo masaa 9 hayo ndyo ya kupumzika lakini unakuta kijana anayatumia kukesha kunywa pombe,akitoka hapo anaingia road tena matokeo ndyo hayo
 
Mimi siku hizi nawaogopa,maana nimeshawagonga sana,naona wanachonitafutia sasa ni kesi tu.Sasa hivi wamefikia mahali wanatoa taa kubwa ile ya original mbele wanaweka kitaa kimoja kidogo kina mwanga hafifu,yaani hata haijulikani wanataka nini...
Hiv kwann wanatoa ile taa kubwa.. afu wanaweka kataaa kadogoo kenye mwanga ambao hauelewek..
 
Jiepushe kuiga malimbukeni kwa kuanza sentensi na neno ''kwahiyo''. Halafu mbaya zaidi hata kuandika neno lenyewe wengi hawajui.
Wewe mwenyewe hujui kwamba kamati ya waganga wanakupakua kila usiku
 
Wenyewe wakikaaga vijiweni sijui kama huwa wanapeana tahadhari!
 
Unakuta bodaboda anakimbia mwendo kasi kuwahi kubeti au kucheza drafti kijiweni.
 
Kwaiyo wewe huna usamaria wema uongo? Uliona kupakia huo mzoga kwenye hicho ki rahum chako kwamba kingeisha mafuta au unakuja kueleza unoko hapa,hata picha hujaweka....
Ulitaka wagombanie kumbeba majeruhi? Maana umeshaambiwa kuna aliyembeba, tatizo ni kama bodaboda asingepata msaada ungeweza kusema hayo uliyoyasema
 
Hawa watoto wengi wao bangi haziwapendi kabisa. Mtaa ninaoishi wanasumbua mpaka basi. Yaani muda wote ni kelele, na kupita kwa mwendo kasi!!
Na wanakufa kweli kutokana na huu ujinga wao!! Lakini hata hawajali.

Kiukweli kuna bodaboda wachache sana wenye akili timamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…