Bodaboda: Japo mnatukamata, lakini bila sisi musingewakamata

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Ni maneno ya waendesha bodaboda wa mzinga kongowe baada ya kufanikisha Kuwauwa majambazi. Baada ya purukushani ya barabarani kati ya pikipiki ya maaskari na Pikipiki ya majambazi.

Bodaboda walitoa msaada mkubwa baada ya gari ya police kushindwa kuingia katika Barbara ya kisasa iliyo na mashimo na Kuwaambia bodaboda wa mzinga "jamani majambazi Yale" na police kudandia bodaboda zilizopo mgundini na safari kuanza kuelekea kisasa hadi chulwi walipo wauwa majambazi wawili na mmoja kutokomea baada ya boxer yao kuanguka ktk mchanga na kuwabwaga wanzake nayeye kukimbia.

Kabla ya hapo majambzi yalichapuka na kuingia njia ya vumbi baada ya kuona cruiser ya police iliyokuwa ikitokea kufanya doria kongowe ikiwa haijui nini kinaendelea.

Bodaboda: Msitupige virungu tuwapo mijini nasi tuna msaada mkubwa katika kuhakikisha usalama unapatikana.
 

Attachments

  • 4.jpg
    4.jpg
    10 KB · Views: 31
  • 01.jpg
    01.jpg
    10.8 KB · Views: 36
Kweli hawa watu wana umuhimu wao bhana.
Nifah kila mtu ana umuhimu wake. Pia jukumu la kulinda usalama ni la kila raia ikijumuisha na hao bodaboda. Na katika kutekeleza hilo jukumu la kulinda usalama hauwezi kuvunja sheria zingine zilizopo kwa kudai kwamba wewe ni muhimu na unatoa msaada fulani. Kwa hiyo kama kuna sheria inayowakataza bodaboda kuingia mjini na pikipiki zao basi wanatakiwa kuheshimu hilo.
 
Halafu majambazi ni kati ya hao hao boda boda!!

Si kweli. Nakama kweli basi tuseme wengi wa wachagga ndio majambazi sababu ujambazi ukithiri sana wakati wa sikukuu za pasaka na xmass japo hazina uhusiano na wachagga.
 
Back
Top Bottom