Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Madereva wa bodaboda na bajaji wa Wilaya na Mkoa wa Singida wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani na utulivu, hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, kwa kutambua kuwa shughuli zao hutegemea uwepo wa usalama na utulivu nchini.
Wito huo umetolewa Oktoba 17, 2025 na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Singida, ASP Theresia Mdendemi, katika mkutano uliofanyika eneo la Kindai Garden, ambapo aliwasihi madereva hao kutoshiriki kwenye makundi ya uchochezi, kutumia mitandao ya kijamii kwa maadili, kuwa wamoja, na kutoa taarifa sahihi za uhalifu.
ASP Theresia pia aliwataka kutumia nafasi yao ya kukutana na watu wengi kila siku kueneza ujumbe wa amani na kushirikiana na Jeshi la Polisi kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa za matukio au wahusika ili hatua zichukuliwe kisheria.