Bodaboda 600 wahitimu mafunzo wilayani Tarime Mara

jaffari yogo

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
685
148
Bodaboda 300 Kati ya 600 waliohitimu mafunzo ya udereva wilayani Tarime wamekabodhiwa vyeti na mkuu wa wilaya hiyo mh Luoga siku ya Ijumaa 03.02.2017.
Mkuu wa wilaya aliongozana na OCD na DTO ambapo aliwaomba bodaboda hao kuwa waalimu wazuri mitaani na kuonyesha mfano mzuri wa utii wa sheria. Vile vile aliwaomba kushirikiana na jeshi la polisi kufichua wahalifu. Pia aliwaomba kuwa makini sana wanapokata bima maana zipo feki na akawaomba kushirikiana na jeshi la polisi kuwaumbua hao wenye bima feki. Vile vile aliwaambia watafute pesa kwa ajili ya leseni na ambao wamesoma hawatakamatwa na polisi ndani ya miezi miwili kwa ajili ya leseni ili waweze kujipanga kupata leseni maana wameonyesha nia nzuri.
Katika Risala iliyosomwa na katibu wa bodaboda wilaya, walimuomba OCD kuwakamata wale wote waliokaidi kwenda kwenye mafunzo.
414b77dfbf55b28ea231272ab7d6ab0d.jpg
3b674f8ab8e65621ad6ee6516f3b9a51.jpg
de19bd1ad92a0a80d1962667f3a9fc7e.jpg
f5055fc440fee041e9f9528d8bc824ae.jpg
c39829d1a63f27c0e320bf9a06efe53e.jpg
501a0b889ab331c4564d37986c0b5cd5.jpg
a54b0a2a7e0cd5cf54dbc777dd5c9c55.jpg
97949ef43c7e1e820baf1df14138f90d.jpg
IMG-20170203-WA0029.jpg
 
Back
Top Bottom