Usidhani bobi wine yuko pale bila sababu maalum. Waganda wamemchoka m7 big time na wengine wamepambana sana kumtoa kupitia box la kura mpaka wamechoka wenyewe. Mmojwapo ni Besigye. Jamaa amepambana sana, ameteswa sana, kaenda jela sana, kapigwa sana, hata kutembea kwenda kazini kwake (katika biashara zake esp zile petrol stations zake kampala) ilikuwa shida hata kwenda kanisani hatakiwi hata kwenda Maana raia wamemchoka m7 wakimuona tu hata kama anajipitia tu njia ktk gari yake cz inajulikana.polisi wamefika wanamzingua. alikosa uhuru wa kufanya hata yake ya kijamii mpaka kaamua kachoka kabisa kaacha siasa.
Pia siasa za uganda kabila kubwa ni wabaganda kutoka central ndo wengi so ni makabila yanapambana wanyankole kutoka western (kabila la m7) wamejaa ktk serikali, jeshi nk bobi wine hayuko pale kama mwehu wengi wamepambana wamechomoa njiani bila kupenda. yeye kajivika mabomu sasa ulitaka familia yake iteketee ili ufurahi au? Kumbuja juzi juzi tu alikoswa koswa na bomu/risasi ambayo ilijeruhi walinzi wake akawa anavaa bullet proof jacket hadi ktk kampeni. majuzi tena mlinzi wake frank kauawa live.kabisa achia mbali wamefungwa wako detained wengine kibao lina Nubian Li etc
kwa taarifa yako bobi yuko nyuma ya watu wengi mpaka ndani ya buganda kingdom yeye kajivika mabomu tu ila kikiwaka kitawaka sana. Anaweza asiwe mtu sahihi sana lakini n mtu hata ukimsikiliza anajua.anachokiongea. na trust me support ataipata kubwa tu toka central. M7 anategemea police n jeshi tu otherwise angekuwa amesharudi kwao huko kuchunga ng'ombe akaachana na ikulu ya nakasero